Waendesha mashtaka
wanaouchunguza matukio ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris Ufaransa
wamemtaja mmoja wa washambuliaji 7 wa kujitoa mhanga.
Omar Ismail
Mostefai mwenye umri wa miaka 29 anasemekana kuwa ni raia wa ufaransa
aliyekuwa anachunguzwa na polisi wa kupamabana na ugadi kabla
hajatoweka.Mtu huyo tayari alikuwa na rekodi ya uhalifu.
Omar ametambuliwa kutokana na kidole kilichopatikana katika eneo la tukio.
Uchunguzi pia utalenga kubaini iwapo aliwahi kusafiri kwenda Syria au la .
Wachunguzi hao wanasema washambuliaji hao walijipanga katika vikundi vitatu kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo kwa mabomu na ufyatuaji wa risasi.
Mbali na bunduki washabuliaji hao pia walikuwa na mikanda ya mabomu waliotumia kujilipua katika msururu huo wa mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 129.
Wengi wa waliolengwa walikuwa mashabiki wa tamasha la muziki, wateja katika migahawa ,baa na hata mashabiki wa soka.
Kundi la wanamgambo wa I S wamedai kuhusika na tukio hilo.
Washambuliaji 7 walijilipua huku mmoja wao akipigwa risasi wakati wa operesheni ya kuokoa maisha ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa maonyesho.
Wachunguzi wanasema kuwa wanahofu kuwa washambulizi zaidi waliotoroka na sasa msako unaendelea.
Rais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari na kufunga kabisa mipaka ya taifa hilo.
Created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment