Saturday, 14 November 2015

Tagged Under:

Walimu waagizwa kufuata kasi ya Rais

By: Unknown On: 10:26
  • Share The Gag

  • Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini

    WALIMU wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi, ubunifu na maarifa kuendana na kauli mbiu ya Rais John Magufuli ya Hapa Kazi tu ili wanafunzi waelewe kinachofundishwa darasani bila ya kutegemea masomo ya ziada.
    Mwito huo umetolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati wa mahafali ya 23 yaliyofanyika katika Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo.
    Sagini alisema walimu wengi wamekuwa wakilalamikia maslahi yao na kuanzisha masomo ya ziada kwa wanafunzi ambapo wazazi na jamii kwa ujumla wamekuwa wakilalamika.
    Alisema walimu wanapaswa kufanya kazi bila ya visingizio kwa kuwa serikali inaboresha maslahi yao na kuongeza kuwa watumishi wa umma wamekuwa wakilalamikiwa na jamii kutofanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa.
    Sagini alisema utamaduni huo haukubaliki na unakemewa kwa nguvu zote ili mtumishi asiyetaka kufanya kazi kulingana na matakwa ya sheria, aache kazi na wachukuliwe watu wengine wenye moyo wa kujituma.
    “ Wahitimu hawa wanataka vyeo lakini haviwezi kupatikana ikiwa haujitumi katika kazi zao za kila siku. Kufanikiwa kwako kunatokana na ubunifu, ufanisi na utendaji mzuri,” alisema Sagini.
    Aliongeza kuwa Tamisemi imetoa mwongozo kwa halmashauri zote nchini kuwa na utaratibu wa mpango wa mafunzo na bajeti. Alisema viongozi wa elimu katika halmashauri hizo wanatakiwa kuwalipia ada na kuwaruhusu kuhudhuria katika mafunzo ya mara kwa mara.
    “Wapo watu wachache ambao wanazuia walimu wasiende kwenye mafunzo na kutowalipia ada, hali hii haikubaliki kwa sababu wanachukia serikali. Pia kama mtu anamdhamini wake atuambie ili asome,” alifafanua.
    Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ADEM, Dk Siston Masanja alisema kuwa wanafunzi waliohitimu ni wa kozi ya Stashahada ya Uongozi na Menejimenti ya Elimu (DEMA) pamoja na astashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu (CELMA).

    Created by gazeti la Habarileo.

    0 comments:

    Post a Comment