Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdalla Bulembo.
RAIS John Magufuli amepongezwa kwa kasi ya utendaji kazi wake
sambamba na maelekezo kadhaa ambayo amekwisha yatoa katika muda mfupi
aliokuwa madarakani. Pongezi hizo zilitolewa jana na Jumuiya ya Wazazi
CCM ambao amepongeza hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na Rais Magufuli
katika kipindi cha wiki tatu toka kuapishwa kwake ambapo jumuiya hiyo
imesema ni imani yao kuwa nchi imepata kiongozi shupavu mwenye kusimamia
kauli zake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema kuwa Jumuiya ya
Wazazi inapongeza maelekezo mbalimbali ambayo yametolewa na Rais
Magufuli ambayo yanajenga msingi bora wa mafanikio.
“Chama kimepata kiongozi bora lakini pia nchi imepata Rais bora na
hili linaendelea kujidhihirisha katika mambo ambayo yameanza kufanywa na
Rais wetu na pia katika maelekezo yake kwa viongozi wa chini, sisi
umoja wa wazazi tunapongeza sana kwa hayo,” alisema Bulembo.
Bulembo alisema amefanikiwa kuwa karibu na Rais Magufuli katika
kipindi chote cha kampeni kitu ambacho amekiona ni kuwa Rais ni mtu
anayesimamia wakati wote na kauli zake.
“Muda tuliokuwa na Rais katika kipindi cha kampeni tumejifunza kitu
kwake, huyu ni mtu ambaye akisema jambo ndilo hilo hilo na analisimamia
watu wasiwe na hofu naye hana nguvu ya soda,” alisema Bulembo.
Baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na Rais Magufuli ni pamoja na
kufanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa
maelekezo ya kuboresha huduma katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na
kufanyiwa matengenezo kwa kipimo cha MRI, ziara ya ghafla Wizara ya
Fedha, kufutwa kwa sherehe za Uhuru Desemba 9 mwaka huu na pia Siku ya
Ukimwi, Desemba Mosi.
Created by gazeti la Habarileo.
Saturday, 28 November 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment