HALMASHAURI
za jiji la Dar es Salaam zimetakiwa kutenga fungu ili kusaidia
kupunguza michango mashuleni na kuendana na agizo lililotolewa na rais
kuhusu elimu kutolewa bure kuanzia mwaka 2016.
Akizungumza
juzi jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini alisema
ni jukumu la kila halmashauri kusaidia shule zilizopo katika maeneo yao
ili kupunguza michango kwa wazazi.
Alisema
manispaa nyingi zinakusanya kodi mapato ya kodi yanayotokana na
michango ya wananchi na yamekuwa yakiongezeka hivyo ni vyema wakurugenzi
wakatumia busara kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kutoa kiasi
cha fedha kununua madawati, kujenga madarasa na kumlipa mlinzi pamoja
na michango mingine.
“Najua
mnapata fedha nyingi tu tumieni kiasi kidogo kulipia ulinzi wa shule na
michango mingine tuondoe hii kero kwa wazazi na kuendana na agizo la
rais,” alisema Sagini.
Aidha
alisema aina ya michango ambayo kamati zitaamua isiwe ya kumfukuzisha
mwanafunzi shule au kumtoa katika masomo ya ziada ‘tuition’
zisilazimishwe kwa kuwa walimu wanalipwa mishahara na serikali ili
wafundishe.
Alisema
kwa mtendaji yeyote atakayekwenda kinyume na agizo kazi itakuwa
imemshinda na ataondolewa mapema na kuna baadhi ya shule za Dar es
Salaam zimelalamikiwa kuanza kutoza michango kwa wazazi kinyume cha
sheria ya elimu.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment