Kundi la wapiganaji la Islamic State
limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa
usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais Hollande ameelezea
mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao
alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi.Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.
Wakuu wanasema paspoti ya Syria ilionekana karibu na mwili moja.
Watu kama 80 walikufa katika tamasha la muziki wa roki - ambako washambuliaji waliwakabili mateka wao na kuwapiga risasi.
Hapo awali, watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi nyingi dhidi ya mikahawa iliyo karibu na kusababisha hasara kubwa.
Wengine waliripua mabomu karibu na uwanja wa michezo wa taifa, ambako Ufaransa ikicheza mechi ya kandanda na Ujerumani.
Created by BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment