Ndege za kijeshi za Uturuki zinaripotiwa kudungua ndege ya kijeshi isiyojulikana karibu na mpaka wake na Syria.
Afisa
wa jeshi la Uturuki ameambia shirika la habari la Reuters kwamba ndege
za kijeshi za Uturuki aina ya F-16 zilishambulia ndege hiyo baada ya
kuionya kwamba ilikuwa imeingia anga ya Uturuki bila idhini.Runinga ya taifa ya Uturuki imepeperusha ukanda wa video unaoonyesha ndege ikianguka milimani karibu na mpaka wake na mkoa wa Hatay.
Ndege za kijeshi za Syria na urusi zimekuwa zikishambulia wapiganaji wa Kiislamu pamoja na waasi wanaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi eneo hilo.
created by BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment