Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Suleiman Kova amesema kati ya masuala ambayo yaliliumiza kichwa Jeshi la Polisi ni maagizo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa wafuasi wao.
Kova
alisema suala ambalo liliwanyima zaidi usingizi ni maagizo ya
maandamano baada ya uchaguzi pamoja na wananchi kutakiwa kulinda kura
zao mita 200, kutoka katika vituo vya kupigia kura.
“Lakini tunashukuru kwa kumaliza Uchaguzi Mkuu salama na hakuna aliyeyapokea maagizo hayo,” alisema.
“Lakini tunashukuru kwa kumaliza Uchaguzi Mkuu salama na hakuna aliyeyapokea maagizo hayo,” alisema.
Akizungumza
katika hafla maalumu ya kuwapongeza askari wake kwa kusimamia vema
kampeni na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Kova alisema maagizo ya kulinda
kura mita 200 na suala la maandamano bila kikomo yaliumiza vichwa jeshi
hilo.
Kova
alisisitiza kwamba japokuwa usimamizi wa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa
mgumu na wa hatari tofauti na mwingine wowote uliowahi kufanyika nchini
tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, walitoa
nafasi sawa za ulinzi na uongozaji wa misafara ya wagombea wote bila
kutoa upendeleo, hivyo kuonyesha mfano.
Alisema
kwa mara ya kwanza uchaguzi umemalizika salama bila kuwapo kwa vifo au
majeruhi yaliyosababishwa na polisi, kutokana na askari kutambua wajibu
wao kwa wananchi na kutumia muda mwingi kutoa elimu zaidi bila ya
kutumia nguvu.
Kova
alieleza kuwa japokuwa kulikuwa na mazingira ya kuchokozwa kwa
makusudi, polisi waliweza kuvuka kizingiti hicho na kusimamia vema
uchaguzi huo.
Alisema
hatua inayofuata ni kuhakikisha askari hao wanalipwa stahili hasa posho
zao ambazo hawakulipwa wakati wote wa kampeni na kusimamia uchaguzi.
Alisema agizo hilo amelitoa kwa wahusika na kwamba limeanza kufanyiwa kazi. Kamanda Kova alisema sasa wanajielekeza kupambana na uhalifu.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment