Mgonjwa aliyeahidiwa matibabu na Rais John Magufuli, Chacha Makenge amefanyiwa uchunguzi na majibu ya kipimo cha MRI na sasa anasubiri upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Chacha
aliyekuwa amekwama kupatiwa matibabu kwa kukosekana vipimo vya CT Scan
na MRI, amepatiwa matibabu hayo kwenye hospitali hiyo ya rufani chini ya
uangalizi wa madaktari bingwa.
Akizungumza na mtandao huu
jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi),
Almas Jumaa alisema, Chacha alikuwa mgonjwa wa kwanza kufanyiwa kipimo
cha MRI baada ya kutengamaa Novemba 11, amegundulika kuwa na tatizo
kwenye uti wa mgongo.
Alisema,
awali mgonjwa huyo alifanyiwa kipimo cha CT Scan nje ya hospitali hiyo
na kugundulika ana matatizo kadhaa, lakini MNH ilihitaji kujiridhisha na
ndipo walipogundua mvunjiko katika pingili zake za uti wa mgongo.
“
Kwa sasa, anaendelea vizuri na baada ya vipimo madaktari wamegundua
katika uti wake wa mgongo kuna mahali kulikuwa na mvunjiko na
inavyoonyesha aliupata muda mrefu, alikuwa akiishi na tatizo hilo,
madaktari wameshauri wiki ijayo afanyiwe upasuaji ili kurekebisha tatizo
hilo,” alisema Almas.
Alipotembelewa
katika wodi ya Sewahaji, Chacha aliyelazwa hospitalini hapo Septemba 8,
alisema tangu Rais Magufuli afanye ziara yake, wamekuwa wakitibiwa kwa
wakati kutokana na mashine hiyo kurekebishwa.
“Nimpe
pole na pongezi rais kwa kazi ngumu aliyoifanya, ameunganisha daraja
baina ya MNH na Moi, awali ilikuwa ngumu, lakini sasa kuna urahisi wa
huduma, matengenezo ya vipimo yameokoa wagonjwa wengi.
“Awali,
kupata vipimo nje ilichukua muda ili kukamilika,” alisema Chacha,
aliyedai alisubiri vipimo vya MRI na CT Scan kwa miezi miwili.
Alipoulizwa
hali halisi ya kipimo cha CT Scan, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema bado mafundi kutoka Kampuni ya
Phillips ya Uholanzi wanaendelea na matengenezo ya mashine hiyo.
“Kipimo
cha CT Scan bado kipo kwenye matengenezo na pindi kitakapotengamaa
tutaufahamisha umma na kwa kuwa wanaotengeneza wanatokea Kampuni ya
Muccos, itakapokuwa imeleta shida watakuja mafundi kutoka Uholanzi,”
alisema Aligaesha.
Novemba
9, Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza MNH na kukutana na kasoro
lukuki, zikiwamo za wagonjwa kulala sakafuni, mashine za vipimo na
uchunguzi wa magonjwa kutofaya kazi kwa zaidi ya miezi miwili.
Creadit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment