Wakati
vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani
Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo
zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White
House).
Mnamo
tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana
hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati
wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo
Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi
za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika
kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.
Aliendelea
kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack
Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani
Afrika.
"Katika
hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema
mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza
haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya
hivyo, hata kama wakati mwingine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana
Ali.
Aliongeza
kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya
nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu
lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia
kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari
zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa
ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua
hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali
alisema;
"Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru"
Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.
"Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru"
Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.
Katika
maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia
kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango
yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi
ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.
Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."
Akizungumza
na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano
hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi
na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu
wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa
alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono
Wazanzibari katika kudai haki yao"
Itakumbukwa
kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka
huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha
Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo,
kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na
Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi
wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya
matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa
urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim
Seif Shariff Hamad.
Kitendo
cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani
waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa
visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili
kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti nchini Marekani wakionyesha mabango yao
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.
Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia
Wapenda amani na Demokrasia wakiwa na mabango yao Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia Bwana Thuweni akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Mpenda amani na Demokrasia Yussra Alkhary akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment