Saturday, 28 November 2015

Tagged Under:

Watu 3 wauawa katika shambulio Colorado

By: Unknown On: 01:51
  • Share The Gag
  • Mshambuliaji akamatwa Colorado
    Watu 3 wameuawa baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi katika eneo la Colorado Springs nchini Marekani.
    Mtu mmoja aliyeshukiwa kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi ametiwa mbaroni.
    Kituo hicho kinasimamiwa na shirika la kitaifa la afya la Planned Parenthood ambalo limekuwa likilaumiwa na baadhi ya watu kwa kutoa mimba.
    Risasi za kwanza zilisikika mapema asubuhi na kuendelea kwa saa tano polisi wakifyatuliana risasi na mtu huyo.
    Maafisa wa polisi wanaimarisha usalama katika eneo la tukio Wakati huo wote taasisi za kukabiliana na hali ya dharura zilikuwa karibu kukiwa na ambulansi ambazo zilikuwa zimesubiri katika theluji iliyotanda eneo hilo.
    Polisi walifyatuliana risasi na mtu huyo walipokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wamekwama katika jengo hilo.
    Wengine wao walikuwa na majeraha.
    Afisa wa polisi wa kutoa usalama katika Chuo Kikuu, Garrett Swasey, mwenye umri wa miaka 44, alikuwa miongoni mwa waliouawa asubuhi.
    Afisa wa polisi Alifariki na raia wengine wawili.
    Alikuwa na mke na watoto wawili.
    Watu wengine tisa, kukiwemo maafisa wengine watano wa polisi walipelekwa hospitalini na inasemekana kuwa hali yao inaendelea kuimarika.
    Baadaye mwanamume mmoja alijisalimisha na kutiwa mbaroni na kuelekezwa kwenye kituo cha polisi.
    Shambulio la kliniki Colarado Shirika linalosimamia kliniki hiyo ya kupanga uzazi, Planned Parenthood, limekuwa likishutumiwa na baadhi ya makundi yanauyopinga uavyaji mimba kama njia ya kupanga uzazi.
    Hata hivyo kufikia sasa lengo hasa la shambulio hilo halijulikani.

    Credit by BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment