Klabu ya soka ya Leicester City wameshinda taji la ligi kuu England
katika historia inayovutia kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata
Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio
hayo makubwa kuwahi kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.
Leicester walianza kampeni zao za ubingwa huku
wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji la ligi na pia
wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja.
Lakini wamepoteza
michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na
ushindi wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu
Spurs,Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi
msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa
ligi.
''Kwa kigezo cha soka la ndani,Leicester City kushinda
taji la ligi kuu ni mafanikio makubwa sana katika historia na haiwezi
kusahaulika'' kiungo wa zamani wa Leicester Robbie Savage ameiambia
BBC.''Ni jambo la ajabu.Hii ni hatua ya mageuzi katika historia ya Ligi
Kuu."
Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni kama hadithi za kale.
Chanzo BBC Swahili.
Monday, 2 May 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment