Tuesday, 3 May 2016

Tagged Under:

Waliofariki mkasa wa jengo Nairobi waongezeka

By: Unknown On: 23:05
  • Share The Gag
  • Siku tano zimepita tangu kuporomoka kwa jumba hilo
    Idadi ya watu waliofariki baada ya jumba la ghorofa sita kuporomoka Ijumaa imeongezeka baada ya miili zaidi kupatikana kwenye vifusi.
    Maafisa wa uokoaji walipata miili mitatu zaidi na kufikisha 26, idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa huo uliotokea baada ya mvua kubwa kunyesha.
    Watu 93 bado hawajulikani walipo kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu.
    Maafisa wa uokoaji bado wana matumaini ya kupata manusura hasa baada ya kupatikana kwa msichana wa umri wa miezi sita kwenye vifusi usiku wa kuamkia jana, siku nne baada ya kutokea mkasa.
    Maafisa wa baraza la jiji wanasema jumba hilo halikufaa kuishi watu.
    Ndugu wawili wanaoaminika kuwa wamiliki wa jumba hilo walifikishwa kortini Jumanne na kushtakiwa kuhusiana na kisa hicho.
    Mahakama inatarajiwa kuamua Jumatano iwapo wataachiliwa huru kwa dhamana.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment