Mkazi
wa Temeke Ramadhani Kusena (48) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu
jela baada ya kupatikana na hatia ya kushindwa kuzuia wizi usitokee
katika Wizara ya Ujenzi, wakati akiwa mlinzi wa eneo hilo.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Catherine Kioja alisema jana kuwa
mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia ushahidi wa
mashahidi wanne.
Mbali
na kifungo hicho, mahakama pia imemuamuru mshtakiwa huyo kulipa fidia
ya Sh500,000 kwa kushindwa kuzuia wizi wa kiti na kompyuta katika chumba
namba 303 kilichopo katika ofisi za wizara hiyo.
Hakimu Kioja alisema mshtakiwa huyo anaweza kukata rufaa kama ataona hajatendewa haki na mahakama hiyo katika hukumu hiyo.
Hakimu Kioja alisema mshtakiwa huyo anaweza kukata rufaa kama ataona hajatendewa haki na mahakama hiyo katika hukumu hiyo.
Awali,
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na
Wakili Grace Mwanga uliomba mahakama kutoa adhabu kulingana na shtaka
hilo. Hata hivyo, Mahakama ilimpa nafasi mshtakiwa ajitete kwanini
asipewe adhabu.
Akijitetea,
mshtakiwa huyo aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anategemewa
na familia. Wakili Mwanga alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 7,
2014 katika ofisi za wizara hiyo Mtaa wa Samora Dar es Salaam.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment