Leo BBC inaanza
msururu wa ripoti tulizokuandalia kuelekea kura ya maoni ya Uingereza
Alhamisi hii itakayo amua iwapo taifa hilo lijitoe au lisalie katika
Umoja wa Ulaya.
Huku siku tatu zikiwa zimesalia kufikia siku ya upigaji wa kura ya maoni ,huku wapiga kura walio wengi wakiwa hawana maamuzi juu ya kura yao itaangukia wapi.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, aliahidi wakati wa kampeni yake katika uchaguzi mkuu nchini humo kutetea kiti chake mwaka 2015 kwamba endapo atashinda,serikali yake itaruhusu kura ya maoni ipigwe ili kuwapa nafasi jumuiya ya Waingereza fursa ya kuamua mustakabali wa baadaye wa taifa hilo katika Umoja wa ulaya
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment