MKAZI wa Mondo katika Kijiji cha Kitumba wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa, tukio hilo
lilitokea Juni 23, mwaka huu, saa 8:00 mchana kitongojini humo.
Msangi
alieleza kuwa, baada ya kufika nyumbani kwa Daudi Mtula anayeuza gongo
kwa siri Magola alikunywa pombe hiyo kupita kiasi akaishiwa nguvu na
kupoteza maisha.
“Mtu
huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,” Kamanda Msangi
alisema na kuongeza kuwa, baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka na
kuuacha mwili wa marehemu nyumbani kwake.
Alisema kuwa Polisi inamtafuta kwa ajili ya kumchukulia hatua za kisheria.
“Tulipata
taarifa kutoka kwa raia mwema na tulipofika nyumbani kwa mtuhumiwa
tuliupata mwili na tayari umekwishafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa
familia kwa ajili ya maziko,” alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kuiunga Polisi mkono kudhibiti biashara ya pombe hiyo haramu.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment