Asilimia kubwa ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya maoni wakiitaka ijiondoe kwenye muungano wa bara Ulaya EU.
Huku
asilimia kubwa ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, asilimia 52% ya
raia wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani
ya EU uliodumu miaka 43.Huko Wales wapiga kura 854,572 (52.5%) waliamua kujiondoa huku wengine 772,347 (47.5%) wakipiga kura kusalia katika muungano huo.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Msemaji wa chama cha Wales Conservatives na mmoja wa wanaharakati wakuu wa kujiondoa Uingereza Andrew RT Davies anasema kuwa kuanzia leo siasa za Wales zimebadilika kabisa.
Wapinzani wao hata hivyo wanadai kuwa Uingereza sasa imeingia katika awamu yenye misukosuko ya kiuchumi na kisiasa.
Kati ya maeneno 17 ya uwakilishi nchini Wales maeneo 5 pekee ndio yaliyopiga kura ya kutaka kusalia kwenye muungano huo.
Maeneo ya uwakilishi ya Gwynedd, Cardiff, Ceredigion, the Vale of Glamorgan na Monmouthshire ndio yalitaka kusalia kwenye mwavuli huo uliodumu kwa miaka 43.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment