UMOJA wa Vijana wa Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) umelaani matukio ya kikatili yanayoendelea kufanyika Zanzibar.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Zanzibar, Mahmoud Mahinda, Katibu Mtendaji
JUVICUF alisema kuwa matendo hayo yamewafanya wananchi kukosa imani na
vyombo vya dola hususan jeshi la polisi.
“JUVICUF
tunalaani vikali vitendo hivyo vya hujuma vinavyoshamiri kila uchao
katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar na inaichukulia hatua hii ya
vyombo vya Ulinzi na Usalama, kukiuka taratibu zake za utendaji na
kutekeleza uhuni dhidi ya raia wanyonge,” amesema.
Alisema
kuwa unyama wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, yanadhihirika katika
matukio ya hivi karibuni yaliyofanywa na askari wa jeshi la Polisi dhidi
ya raia wasiokuwa na hatia katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya
Zanzibar.
“Kwa
mfano, usiku wa tarehe 19 Juni, 2016 askari wa Jeshi hilo lilivamia
kisiwa cha Mtambwe na kuwashambulia raia wa kisiwa hicho kwa mfululizo
wa mabomu ya machozi usiku kucha,” alisema.
Aidha,
alisema JUVICUF inamhakikishia Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia likuwa
mgombea urais visiwani humo kwamba utaendelea kupigania haki yao.
“JUVICUF
tunamhakikishia Maalim Seif Sharif Hamad kutumia ushawishi wetu
tulionao kwa idadi kubwa ya vijana wa nchi hii kupigania haki zetu na za
wazanzibari wenzetu licha ya kuwepo kila aina ya njama za kutufunga
midomo zinazofanywa na watawala waovu kwa kuwatumia vibaraka wao walio
katika maeneo na mamlaka mbali mbali za nchi yetu,” alisema.
Mahinda
alisema JUVICUF haitotetereka wala haitokubali kurejeshwa nyuma kwa
vitimbi vya watawala waovu vyenye lengo la kuzima sauti na madai dhidi
ya haki zao.
Na
kwamba badala yake, JUVICUF itaunganisha nguvu za vijana madhulumu wa
Zanzibar na kutumia ari na nguvu zao kuhakikisha waliyemuita mtawala
muovu anang’oka katika khatamu za Dola ya Zanzibar kwa kutumia njia za
kidemokrasia zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria za nchi.
“Msimamo
huu wa JUVICUF hautokani na khulka ya ubishi, ubabe, ama kibri
kinachotokana na nguvu, bali silka ya uzalendo wa kuitetea nchi yetu na
kupigania haki zetu za kiraia zilizoorodheshwa katika Katiba yetu,” amesema.
Credit; Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.