Siku
moja baada ya wakili wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima, Peter Kibatala kuwaandikia barua Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Kamanda Simon Sirro amesema hawafanyi kazi kwa kufuata barua ya
askofu huyo.
Sirro
alithibitisha kupata barua hiyo, lakini akasema kuwa wanaendelea
kumtafuta popote pale alipo na wakifahamu watamtia nguvuni.
Sakata
la kutafutwa kwa kiongozi huyo linazidi kushika kasi kutokana na
sintofahamu ya kubaini alipo, ikiwamo kambi ya muda wa saa saba
iliyowekwa na polisi nyumbani kwa Gwajima, ambayo haikuwa na mafanikio
wiki iliyopita.
Baada
ya sintofahamu ya wiki nzima huku kukiwa na uvumi kuwa yupo nje ya nchi
na wengine wakidai yupo nchini, juzi wakili Kibatala aliwasilisha barua
Polisi akidai mteja wake yupo nje ya nchi na aliposafiri hakuwa anajua
kama anatafutwa na polisi.
Katika
barua hiyo Kibatala alisema ameelekezwa na mteja wake kufikisha ujumbe
huo na akirejea atajisalimisha polisi kuitikia wito huo.
Jana Kibatala alisisitiza kuwa:
“Kwa sasa yupo nje ya nchi akihubiri injili, alisafiri kabla ya kupata
taarifa kuwa anatafutwa na polisi ana mashauri katika Mahakama ya Kisutu
Julai Mosi, hivyo kabla ya hapo atakuwa amesharejea.”
Lakini
Sirro alisema barua hiyo ni kujitetea ambako hakuna maana na
wanachofanya wao ni kuendelea kumtafuta badala ya kusubiri ajisalimishe
kama ulivyoandikwa waraka huo.
“Suala
la kutupa taarifa za kujifanya alikuwa hafahamu kama anatafutwa si
kweli, tukifahamu mahali alipo hata sasa hivi tunakwenda kumkamata,
hatufanyi kazi kwa kufuata maelekezo yake,” alisema Kamanda Sirro.
Sirro
alifafanua kuwa bado wanafuatilia kubaini kama yupo nchini au nje ya
nchi, wakitambua ni nje nchi atakamatwa huko huko kwa msaada wa
Interpol.
“Hatujafahamu
alipo hata huko nje Interpol wapo kuwashughulikia watu kama hawa
wanaofanya ukorofi nchini na kukimbilia nje ya nchi wakidhani wanatatua
tatizo, kumbe wanaliahirisha,” alisema Sirro.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment