Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema hayo jana ofisini kwake kuwa tukio la kula muhogo unaosadikiwa kuwa na sumu lilitokea Juni 18, mwaka huu saa 9 alasiri kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.
Matei alitaja waliofariki katika tukio hilo ni Omary Mohamed aliyefariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini wakati pacha wake Hamis Mohamed alifariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Alitaja mwingine aliyefariki ni Daud Herman (31), mkazi wa Kauzeni aliyefariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Mzinga iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Kamanda huyo alisema watu hao walifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na kuwa miongoni mwa watu watano waliokula muhogo huo, ambao wawili walinusurika baada ya kupatiwa matibabu.
Alitaja walionusurika kifo ni Amos Kunambi (30), mkazi wa Kauzeni aliyetibiwa na kuruhusiwa baada ya hali yake kuwa nzuri wakati Joshua Msiani (24) anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa.
Alisema miili ya marehemu hao watatu, imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, huku uchunguzi wa kitabibu ukiendelea ili kubaini uhalisia wa ukweli juu ya muhogo huo kuwa na sumu.
Mmoja wa manusura Joshua Msiani aliwaambia waandishi wa habari hospitalini jana kuwa akiwa na wenzake watano, walikuwa wakifyatua matofali eneo la kata ya Kauzeni Manispaa ya Morogoro.
Msiani alisema akiwa eneo hilo, wenzake walileta muhogo na kumkaribisha kula, ingawa aliwajibu kuwa ameshiba lakini walizidi kumlazimisha ili kula muhogo huo wa kuchemsha. “Nikaona wananilaumu sana, ikabidi nichukue kipande kimoja nikala, na ndipo muda mchache nikapoteza fahamu hadi nilipokuja kuzinduka nikiwa hospitalini Mzinga,” alisema.
Katika tukio jingine, watu wawili wa familia moja wamekufa baada ya mmoja wao anayesadikiwa kuwa na ugonjwa wa akili, kumchoma na mkuki tumboni mdogo wake, Raymond Melikioni na kufa papo hapo Juni 17, mwaka huu tarafa ya Mgeta wilaya ya Mvomero.
Chanzo HabariLeo.
0 comments:
Post a Comment