Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena
tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukihama
chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
na kupewa nafasi ya kugombea urais.
Nape
ameeleza kuwa uamuzi huo uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanasiasa
huyo aliyekuwa na nguvu kubwa ndani ya chama hicho alikuwa alama ya
ufisadi kutokana na kukabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi.
“Lowassa
alikuwa alama ya ufisadi, alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu
walikuwa wanahusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikuwa radhi
kuchagua hata jiwe lakini sio CCM,” alisema Nape.
Alisema
kuwa angepata nafasi ya kumshauri Lowassa katika siasa, angemshauri
ajiuzulu siasa kabla hajaondolewa kwa aibu katika medani za siasa.
Kadhalika,
Nape alisema kuwa kosa kubwa ambalo lilifanywa na vyama vya upinzani ni
kumpokea Lowassa ambaye amedai alikuwa amesababisha CCM kupakwa matope
ya uchafu kutokana na kuwa na tuhuma nyingi.
Hata
hivyo, Nape alimpongeza Lowassa kwa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu
kwa kuwa uamuzi huo ulisaidia kuliweka Taifa katika hali ya amani baada
ya uchaguzi.
Lowassa
amekuwa akikanusha tuhuma zote zilizokuwa zikielekezwa kwake hususan
tuhuma za kuhusika na sakata la Richmond lililosababisha ajiuzulu nafasi
ya Uwaziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Alijiunga na Chadema na kugombea nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounda Ukawa.
Alipata
kura takribani milioni 6 na kusaidia kupata wabunge wengi zaidi wa
upinzani akiweka historia ya ushindani mkubwa zaidi kuwahi kutokea
kwenye uchaguzi mkuu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.
Credit; Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.