Hofu na wasi wasi umezidi kutanda huko mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania baada ya kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana.
Hadi
sasa jumla ya watu saba wamefariki na wengine 21 kulazwa katika
hospital ya mkoa mjini Dodoma baada ya kuzuka ugongwa huo ambao hadi
sasa madaktari haujui tiba yake.Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kutapika, kuharisha, ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuumwa na tumbo.
Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo tayari kumetengwa wodi maalum katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Dodoma katikati mwa Tanzania ambapo pia karantini imewekwa na hakuna anayeruhusiwa kukaribia mahali hapo zaidi ya madaktari ambao nao pia wanaingia kwenye wodi kuwaona wagonjwa kwa tahadhari kubwa.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment