Rais wa Argentina
Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa
lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la
kimataifa.
Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake
kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku
akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya penalti.-
Messi ajiulu baada ya kukosa penalti Copa America
''Amemwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa
kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku
akimtaka asisikilize maneno ya watu'' alisema msemaji wa rais Macri.
Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment