Monday, 20 June 2016

Tagged Under:

Trump amtimua meneja kampeni wake

By: Unknown On: 23:18
  • Share The Gag
  • Mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican,Donald Trump, amemtimua kazi meneja kampeni wake.Corey Lewandowski ni mfuasi wa bwana Trump tangu alipotangaza nia ya kugombea urais na kupata ridhaa ya chama chake, kuchaguliwa kuwa mgombea rasmi nchini humo.

    Lakini mwandishi wa BBC aliyeko mjini Washington anasema kwamba bwana Lewandowski amekuwa katika wakati mgumu wa kupambana na timu mpya iliyoajiriwa hivi karibuni na Donald Trump kwa lengo la kuweka sawa oparesheni zake kuelekea uchaguzi mkuu.
    Mwandishi wa BBC,anaendelea kueleza kwamba nao wanachama wa Republican siku za hivi karibuni wamekuwa na wasiwasi juu ya matamshi ya Trump hasa alipozungumzia mauaji yaliyotokea mjini Orlando kwamba yanaweza kupunguz aidadi ya wapiga kura.

    Chanzo BBC.

    0 comments:

    Post a Comment