Thursday, 30 June 2016

Tagged Under:

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Auawa kwa Fimbo

By: Unknown On: 22:12
  • Share The Gag
  • ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 212 kilichopo Milambo mkoani Tabora, ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wafugaji akiwa eneo lake la ujenzi.

    Aliyeuawa katika tukio hilo la juzi katika kijiji cha Usule kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora ni Crius Mkumozi mwenye umri wa miaka 35.

    Mtuhumiwa wa mauaji hayo inadaiwa alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la askari huyo.

    Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema askari huyo alipigwa fimbo kichwani na begani baada ya kujaribu kuondoa ng’ombe waliokuwa kwenye eneo lake.

    Kamanda alisema mtuhumiwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    0 comments:

    Post a Comment