Kufuatia kura ya
maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya
kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa
ushirikiano na Uingereza kiuchumi.
Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.
John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.
Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa dunia kwa ujumla
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment