Kamati Kuu ya CCM imeagiza Kamati ya
Wabunge wa chama hicho kuwapa barua za kujieleza wabunge wao
wasiohudhuria, wanaochelewa na wanaondoka kabla ya vikao vya Bunge
kuahirishwa.
Tayari maagizo hayo yamefanyiwa kazi na Katibu wa Wabunge
wa CCM, Jasson Rweikiza ambaye amewalima barua wabunge hao.
Katika barua yenye kichwa cha habari “Maagizo ya Kamati Kuu ya CCM” aliyopewa mmoja wa wabunge wa CCM inaonyesha wametakiwa kujieleza kwa nini siku nyingine walifika wamechelewa na mara kadhaa walitoka mapema kabla kuahirishwa kwa Bunge.
Katika barua yenye kichwa cha habari “Maagizo ya Kamati Kuu ya CCM” aliyopewa mmoja wa wabunge wa CCM inaonyesha wametakiwa kujieleza kwa nini siku nyingine walifika wamechelewa na mara kadhaa walitoka mapema kabla kuahirishwa kwa Bunge.
“Mwenendo huu ni kukiuka kanuni za Kamati ya Wabunge wote wa
CCM hasa kanuni ya 41. Tafadhali andika maelezo kwa nini Kamati Kuu
isichukue hatua? Maelezo yanifikie kabla ya Juni 25 mwaka huu,”
ilisema sehemu ya barua ya mmoja wa wabunge walioandikiwa.
Alipoulizwa
Rweikiza kuhusiana na barua hiyo alisema haitambui na kwamba
imeghushiwa.
“Kanuni zipo zinazoongoza vikao vya Bunge, zipo pia zinazoongoza wabunge wa CCM.
“Kanuni zipo zinazoongoza vikao vya Bunge, zipo pia zinazoongoza wabunge wa CCM.
"Wakitaka kuondoa wabunge wa CCM wanazijua
sana, isipokuwa hatujafikia hatua ya kufundishana kwa kuanza kuandikiana
barua,”alisema.
“Wanajua mbunge hawezi kuondoka bila kwenda kwa Spika
na kuomba ruhusa au kujulisha kwenye chama kwamba anatoka, wanajua,”
alisema Rweikiza na kusisitiza kwamba hata taarifa zinazoonyesha kuna
wabunge wanaotakiwa kujieleza kwake ni majungu tu.
Japokuwa Rweikiza
ameikana barua hiyo, wabunge kadhaa wa CCM walioomba majina yao
yasitajwe wamekiri kwamba barua hizo zimetolewa na kwamba wanabanwa kwa
kutakiwa kujisajili mara mbili; kitabu cha Bunge na cha CCM.
Katika
ukurasa wake wa Facebook uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema wabunge wa
CCM wanalalamikia kulazimishwa kuingia bungeni kwa kuwa Bunge halina
ladha.
Pia, Msigwa alisema wabunge hao wa CCM wanadai Naibu Spika Dk
Tulia Ackson hafuati kanuni na taratibu na kwamba wametakiwa kujieleza
Kamati Kuu ya CCM.
Aidha, baadhi ya wabunge wa CCM walionekana kukerwa
na utaratibu wa kujisajili sehemu mbili yaani Bunge na CCM mara mbili
kwa siku.
“Kuna haja gani ya kutia dole (kusaini kwa utaratibu wa
kieletroniki) halafu tena tuje tusaini kwenye makaratasi ya CCM?,”
alihoji mmoja wa wabunge.
Alisema ili kusaini karatasi hizo inawapasa
wabunge kwenda upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani ambapo wabunge
waliokabidhiwa kazi ya kuzitunza karatasi hizo hukaa kama kambi mbadala
baada ya wabunge wa upinzani kususia vikao vinavyoendeshwa na Dk Tulia.
“Wengine tunaheshima zetu hatuwezi kwenda upande wa upinzani kufuata
makaratasi ya kusaini. Kwanza Bunge lenyewe halina mvuto unakuja hapa
watu wawili ndio wanapewa nafasi ya kuchangia mjadala na baada ya hapo
wanapitisha,” alisema.
Mbunge mwingine wa CCM alisema haoni haja ya
kuwepo ndani ya Bunge kwa sababu hawapewi nafasi ya kutosha ya
majadiliano na hivyo bora kutokuwepo ndani ya ukumbi muda wote.
“Mimi
saa hizi naingia ndani ya ukumbi wa Bunge nasaini natoka naenda zangu
kantini (ya Bunge) kuangalia mpira maana hata nikikaa ndani sitopata
nafasi ya kuchangia,” alisema mbunge huyo.
Alisema haoni haja ya kusaini
mara mbili kwa sababu CCM wanaweza kutumia usajili wa Bunge kufahamu
wabunge waliopo na wasiohudhuria kwa wakati wanaouhitaji.
Alisema orodha hiyo haina mashiko kwa sababu wanazo namba za wabunge wote kama kuna jambo ambalo wanahitaji basi wanaweza kuwataarifu.
Alisema orodha hiyo haina mashiko kwa sababu wanazo namba za wabunge wote kama kuna jambo ambalo wanahitaji basi wanaweza kuwataarifu.
“Hata mimi nimepewa
barua ya kujieleza lakini si kwamba ni mtoro bali tunakuwa na majukumu
mengine ya kibunge nje ya Bunge,” alisema.
Hatua hiyo inakuja wakati
wabunge 118 wa vyama vinavyounda Ukawa, wakiwa wamesusia vikao vya Bunge
vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ya kuongoza
vikao kibabe na kutofuata kanuni.
Hii ni wiki ya nne tangu Dk Tulia
aanze kuendesha vikao vya Bunge peke yake bila kupokewa na wenyekiti wa
Bunge kama ilivyokuwa kabla hajatofautiana na kambi rasmi ya upinzani
Credit; Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.