Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Inapenda kutoa taarifa kwa Umma
na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa
mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31
Julai 2016.
Katika
kipindi hicho waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo
wa utoaji mikopo na ruzuku uliopo kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz
ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo
kwa njia ya mtandao.
Utoaji
wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya
16 na 17.
Kwa
taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo
kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya
kuomba mikopo ni Julai 31, 2016.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 24 JUNI 2016.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment