Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewatoa wasiwasi
watanzania juu ya kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na
simu za mkononi kwamba haitawaathiri wao ila makampuni ya simu.
Mhe.
Mpango ameyasema hayo Jana mjini Dodoma alipokuwa akitolea ufafanuzi
taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu
namna Serikali itakavyotekeleza Bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitiswa
jana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kwa
sasa sheria inatamka kwamba ada itatozwa katika kutuma fedha tu, hata
hivyo baadhi ya kampuni za simu na benki zimekuwa zikitumia mwanya wa
sheria hiyo kupunguza wigo wa kodi kwa kutoza ada wakati wa kupokea,” alisisitiza Mhe. Mpango.
Mhe.
Mpango aliendelea kufafanua kuwa, kwa kuwa makampuni ya simu na benki
yamekuwa yakitoza ada wakati wa kupokea fedha huku serikali haiwatozi
kodi kwa fedha zinazopokewa, hivyo basi Serikali imeamua kutoza ushuru
kwenye ada ya kutuma na kupokea fedha au vyote kwa kadri itakavyotozwa.
Aidha
Mhe. Mpango alisisitiza kwa kusema kuwa ushuru huo utalipwa na benki na
kampuni ya simu na siyo mtumiaji au mpokeaji wa fedha katika miamala
itakayofanyika.
Hivyo
basi Waziri Mpango ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki
Kuu ya Tanzania (BOT) kuhakikisha kwamba tozo hiyo inaendana na uhalisia
wa huduma inayotolewa kwa kufanya ukaguzi wa miamala ya makampuni ya
simu kabla na baada ya tozo ili yasihamishie mzigo kwa mtumiaji wa
mwisho.
Kuhusu
suala la kulipa kodi Mhe. Mpango amewasisitiza wananchi kulipa kodi
kama inavyotakiwa ili Taifa liweze kujenga uwezo wa kujitegemea na
kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli kwa kuwa hiyo ndio dhamira ya
Serikali ya Awamu ya Tano.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment