Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
MGONJWA mmoja aliyekuwa akiugua ugonjwa wa ajabu, ulioukumba mkoa wa
Dodoma, amefariki na kufanya idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huo kufikia
saba huku wanaougua wakiongezeka na kufikia 21, kati ya hao wawili ambao
ni watoto wakiwa katika hali mbaya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu alisema hayo mjini hapa jana alipotoa taarifa kuhusu hali ya
ugonjwa huo na hatua ambazo serikali imekuwa ikichukua kukabiliana nao.
Ugonjwa huo kwa mjibu wa Ummy, ulianzia katika wilaya ya Chemba
ambako watu tisa wa familia moja kutoka kijiji cha Mwaikisabe kata ya
Kihama, waliathirika na baadaye wagonjwa wengine walianza kupatikana
kutoka vijiji vya karibu.
Dalili za ugonjwa huo zilionekana kuwa ni kutapika, kuharisha, kupata
rangi ya manjano machoni, kuwa na maumivu ya tumbo na kuvimba tumbo kwa
kujaa maji katika muda mfupi, lakini hawapati joto kali wala harara
katika ngozi.
Taarifa za awali za chanzo cha ugonjwa huo kwa mujibu wa Waziri,
ilitajwa kuwa ni watu hao kula nyama ya ng’ombe aliyechinjwa baada ya
kuvunjika mguu, ingawa baaadhi ya watu waliokula nyama ya ng’ombe huyo
hawajaugua.
Katika familia hiyo ugonjwa huo unaoshika watoto kwa watu wazima, pia
uliua mbwa wakubwa watatu, mbwa wadogo watatu na paka mmoja.
Akizungumzia uchunguzi wa awali uliofanywa na Maabara Kuu ya Taifa, Ummy
alisema umeonesha kuwa si homa ya manjano wakati vipimo vingine
vikifanyika kuona kama ni Homa ya Bonde la Ufa, huku kesho Ofisi ya
Mkemia Mkuu ikitarajiwa kutoa matokeo ya uchunguzi wake.
Tathmini ya taarifa hizo za awali, Ummy alisema inahusisha ugonjwa
huo na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu, ambayo hupatikana katika
vyakula vya aina mbalimbali visivyohifadhiwa vizuri.
Waziri huyo alisema pia tathmini hiyo imebaini kuwa ugonjwa huo si
kimeta kwa kuwa hauambukizi, ila unaonekana unaweza kuwa umetokana na
matumizi ya kitu ambacho ni maarufu kwa kundi hilo la watu.
Tayari kwa mujibu wa Ummy, sampuli za nafaka walizokuwa wakitumia
familia zilizoathirika zimechukuliwa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi ngazi
ya Taifa katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Maabara ya Mkemia
Mkuu na leo mchana, huenda TFDA ikatoa majibu ya uchunguzi wake.
Mbali na sampuli za nafaka walizokuwa wakitumia familia za
waathirika, Ummy alisema sampuli za damu ya wagonjwa, kinyesi,
matapishi, vinyama vitokanavyo na ini, zimechukuliwa na kupelekwa katika
maabara.
Wagonjwa hao kwa sasa wanahudumiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
katika wodi maalumu, huku timu ya awali ya uchunguzi ikiwa imepelekwa
katika wilaya za Chemba na Kondoa kwa uchunguzi.
Jana timu nyingine ya wataalamu iliwasili kutoka Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Ofisi ya Mkemia Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) na TFDA kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Chanzo HabariLeo.
Monday, 20 June 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.