Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Sharif Hamad aliwasili mjini Zanzibar jana baada ya kumaliza ziara ya
kichama katika mataifa mbalimbali ya Magharibi.
Katika ziara ya takriban wiki mbili, Maalim Seif na ujumbe wake akiwamo Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, walitembelea Canada, Marekani na Umoja wa Mataifa, jijini New York.
Katika ziara ya takriban wiki mbili, Maalim Seif na ujumbe wake akiwamo Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, walitembelea Canada, Marekani na Umoja wa Mataifa, jijini New York.
Maalim Seif aliwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Abeid Amani Karume, Kisauni mjini hapa saa 11 za alasiri na
kupokewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF
Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui.
Katika salamu zake fupi, Maalim Seif alisema ripoti ya uchaguzi iliyowasilishwa juzi kwa Rais John Magufuli na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haiwezi kuwa na jawabu la mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, kwani waliosaidia kuuvuruga ndio walewale waliojidai kuwasilisha ushahidi, jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Alisema tatizo la Zanzibar bado lipo na dawa yake ni kuirejesha haki ya
kidemokrasia ya wananchi walioamua kupitia masanduku ya kura ya Oktoba
25, 2015.
“Hili, chama cha CUF kilikwishalitolea maamuzi kupitia
maazimio ya Baraza Kuu, kama mnakumbuka, nayo ni pamoja na kutoitambua
Serikali ya Dk Shein na kuendelea kuikataa kwa vitendo na nafsi na pia
kuendelea kudai haki ya maamuzi ya wananchi hadi pale itakapopatikana,”
alisema.
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali
iliyopita alisema; “kwa hili watawala wasijisumbue, wananchi hawajalala
na katu hawatorudi nyuma, wewe wacha watoe tu hizo ripoti zao... msimamo
wetu upo palepale”.
Kuhusu ziara yake, Maalim Seif alisema ilikuwa ya
matumaini na mafanikio makubwa katika kufanikisha juhudi za kutetea na
kupigania haki ya kidemokrasia ya wananchi na kwamba muda ukifika
ataweka bayana zaidi mafanikio hayo.
Katika ziara hiyo Maalim Seif aliwasilisha mada ya ‘Chaguzi za Zanzibar: Haki iliyocheleweshwa’, katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa taasisi za kimataifa za taaluma za siasa, stratejia na demokrasia za NDI, IRI na CSIS za Marekani.

Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment