Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wakati wa
mchakato wa chama kurejesha imani kwa wananchi hali ilikuwa ngumu kwake
hadi kufikia kutishiwa maisha na watu wasiojulikana.
Mbali ya
watu hao kumpigia simu za vitisho nyakati za usiku, pia walikuwa
wakimchafua kupitia mitandao ya kijamii lakini anamshukuru Mwenyezi
Mungu alivuka salama na chama kimevuka salama.
“Tulipoanza
kuzunguka kujenga chama nilitukanwa sana. Watu waliwekeza kunichafua.
Watu hao niliokuwa nawanyooshea kidole hawakufurahishwa na hatua ile
hivyo wakaweka mkakati wa kutaka kunifukuzisha ndani ya chama na ilifika
hatua wakawa wananichafua katika mitandao ya kijamii.
"Nikaamua
kujitoa huko mpaka leo hii nimeamua kujitoa katika mitandao na kubaki
katika twitter pekee kwa kuwa unaweza kutambua mtumiaji,” alisema Nape.
Akizungumza nyumbani kwake mkoani Dodoma, Nape
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na ambaye aliteuliwa
kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 2011 Mwenyekiti wa CCM,
Jakaya Kikwete alipounda sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, William
Mukama alisema watu hao walifikia kudai yeye si mtoto wa Mzee Moses
Nnauye.
Kamati Kuu chini ya Mukama ilipita mikoani na kaulimbiu
ya kuvua gamba iliyoasisiwa na chama kwa lengo la kuwaondoa watuhumiwa
ufisadi lakini iliondolewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 ikaundwa
mpya chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.
Kukata vigogo
Katibu huyo wa uenezi alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ilikuwa kukata majina ya waliokuwa viongozi wa Serikali ambao walijitokeza kugombea nafasi hiyo.
Katibu huyo wa uenezi alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ilikuwa kukata majina ya waliokuwa viongozi wa Serikali ambao walijitokeza kugombea nafasi hiyo.
Nape
alisema kumpata mgombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho kongwe
ilikuwa kazi nzito baada ya viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya
Awamu ya Nne kujitokeza wakiwamo, aliyekuwa Makamu wa Rais Dk Gharib
Bilal, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na aliyekuwa Jaji Mkuu
Augustino Ramadhani.
Vigogo wengine waliowapa wakati mgumu CCM
ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne,
Frederick Sumaye na Edward Lowassa, na mawaziri kadhaa lakini kwa uwezo
wa Mwenyezi Mungu waliweza kutimiza wajibu wao.
“Kuwaondoa
viongozi waliokuwa madarakani ni sawa na kutafuna jongoo kwa meno lakini
hatukutetereka na hatimaye tukapata majina matano ambayo nayo
yalipigiwa kura na kupatikana jina la mgombea mmoja,” alisema.
“Ingawa
vikao vilikuwa vya moto sana na kulazimika kukesha mpaka usiku, kila
mmoja alipata nafasi ya kujadiliwa na kutendewa haki siyo kama
ilivyovumishwa kuwa wagombea wengine hawakujadiliwa,” alisema.
Nape
alisema katika chama chao kila mwanachama ana nafasi sawa hivyo
haikuwasumbua kuangalia majina ya watu hao wala nyadhifa zao badala yake
waliangalia sifa za mgombea mwenyewe ndani ya chama.
Alisema
anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na
kifua cha kuhimili vishindo na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato
huo kwa kuwa ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani
uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia.
Nape alisema itachukua
muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi
iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na wazee
waliorekebisha mambo na kuvuka salama kwa kuwa hali ilikuwa mbaya.
Bunge laivu
Nape alisema suala la kuzuia kurushwa moja kwa moja kwa matangazo ya Bunge si lake na kwamba lilipitishwa na wabunge wenyewe.
Nape alisema suala la kuzuia kurushwa moja kwa moja kwa matangazo ya Bunge si lake na kwamba lilipitishwa na wabunge wenyewe.
“Mimi ni msimamizi wa Serikali. Watu
wanapotosha, nilichofanya ni kulinusuru Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC), kwa miaka 10 mfululizo Bunge lilishindwa kuwalipa fedha zao
ambazo ni Sh4.5 bilioni kila mwaka.
“Hili liwe fundisho kwa
wabunge, kuna vitu wabunge wanapitisha hawavijui baada ya muda wanaona
madhara yake wanaanza kulalamika kumbe walivipitisha wenyewe...Suala la
Bunge kuanzisha kituo cha televisheni pia walilipitisha wenyewe, leo hii
Katibu wa Bunge anavyotumia fedha kama ingekuwa haipo katika bajeti
wasingemwacha,” alisema.
Chanzo Mpekuzi Blog
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
ReplyDeleteKAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.
KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.