Waziri mkuu wa
Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa
kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment