Sunday, 27 December 2015

Amani yatawala Maulid, Krismasi

By: Unknown On: 00:17
  • Share The Gag

  • IGP Ernest Mangu.

    WAKAZI wa maeneo mbalimbali hapa nchini wamesherehekea sikukuu ya Maulid na Krismasi katika hali ya amani, bila kuwepo na matukio makubwa ya uvunjifu wa amani.
    Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, makamanda wa Polisi wa mikoa ya kipolisi ya Dar es Salaam na Pwani, wamesema kuwa hakuna matukio makubwa yaliyoripotiwa katika sikukuu hizo.
    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ilala, Lucas Nkondya akizungumza na gazeti hili alisema kwa taarifa alizonazo mpaka jana mchana hakuna tukio lolote lililoripotiwa ambalo liliashiria uvunjifu wa amani.
    “Kwa taarifa nilizonazo mpaka sasa huku kuko shwari kabisa hakuna tukio lolote kubwa lililotokea la uvunjifu wa amani, watu wamesherehekea vizuri,” alisema Kamanda Nkondya.
    Aidha alisema katika matukio yaliyoripotiwa ni kukamatwa kwa pikipiki za biashara maarufu kama bodaboda 80 katika maeneo mbalimbali, ambao walipatikana na matukio ya uvunjifu wa sheria ya usalama barabarani.
    Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema pia kuwa hali katika sikukuu hizo ilikuwa ni shwari bila kutokea vurugu zozote kwa upande wa Kinondoni. Kwa upande wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema pia kuwa hakukuwa na tukio kubwa la uvunjivu wa amani isipokuwa matukio ya kawaida.
    “Siwezi kusema kuwa hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani lakini hakukuwa na tukio kubwa kwa upande wa Pwani, matukio kama ugomvi, matusi haviwezi kukosekana,” alisema Kamanda huyo.
    Makamanda hao wamewaomba wananchi waendelee kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya katika hali ya amani kama ambavyo imefanyika kwa Krismasi na Maulid, ili nchi iendelee kuwa na amani.

    Created by Gazeti la HabariLeo.

    Gwajima Amkana Edward Lowassa.....Adai Yeye Hakuwahi Kumuunga Mkono Wakati Wa Kampeni

    By: Unknown On: 00:14
  • Share The Gag


  • Mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima amejitokeza hadharani  na kukana kwamba hakuwahi kumuunga mkono Edward Lowassa wakati wa kampeni za Urais.

    Akiongea katika mahojiano maalumu na kituo cha Azam Tv, Gwajima amesema yeye hakuwahi kuwa mshirika wa Lowassa wala chama chochote, bali aliitwa jijini Arusha na Jangwan Dar es Salaam  kwa ajili ya maombi tu na sivinginevyo....

    Amesema kitendo cha kukubali wito huo wa maombi kimewafanya watanzania wahisi kwamba yeye alikuwa team Lowassa, kitu ambacho sio kweli.

    Amedai yeye alikuwa mfuasi wa mabadiliko ya nchi, alikuwa akiunga mabadiliko ya nchi na SIO  personality ya mtu au chama cha mtu.

    Wakati Gwajima akikana kumuunga mkono Lowasaa, kumbukumbu zinaonyesha kuwa mchungaji huyo alikuwa ni team Lowassa na  alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha mheshimiwa Lowassa anashinda kiti cha Urais.

    Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Gwajima alitumia nguvu kubwa sana wakati wa kampeni kupambana na Dr Slaa ambaye wakati huo alikuwa akishusha makombora mazito kuhakikisha Lowassa hashindi huku akimtuhumu Gwajima kuwa mshenga wa Lowassa aliyemfuata kumpigia debe wampokee Chadema

    Tazama Video hii Kumsikiliza Gwajima 
     
    Credit; Mpekuzi blog

    Magufuli, Shein wakutana Ikulu

    By: Unknown On: 00:10
  • Share The Gag

  • Rais John Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Ikulu).

    RAIS John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo hayo jana, Rais Shein amesema lengo la mazungumzo hayo, ilikuwa kumpa taarifa Rais Magufuli, kuhusu hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu.
    Amesema mazungumzo ya hali ya Zanzibar yanaendelea chini ya Kamati Maalumu yenye viongozi wakuu wastaafu na viongozi wakuu wa sasa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo yeye ndiye Mwenyekiti. Wajumbe Mbali na Dk Shein ambaye ni Mwenyekiti, wajumbe wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
    Wengine ni Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete. Pia yupo Rais mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar, Dk Amani Abeid Karume na Rais mstaafu wa Awamu ya Tano wa Zanzibar Dk Salmin Amour.
    *Kazi yao
    Amesema tayari kamati hiyo imeanza mazungumzo tangu Novemba 9, mwaka huu na yamelenga kujadili hatma ya Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, uliofutwa. Rais Shein amebainisha kuwa mazungumzo hayo bado yanaendelea.
    “Kwa hiyo nimekuja kumpa taarifa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya mazungumzo yetu, ili ajue kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo Zanzibar ni sehemu yake na sisi ni jukumu letu kumpa taarifa hiyo,” alisema Rais Shein.
    Kwa mujibu wa Rais Shein, mazungumzo hayo yatakapokamilika wananchi watajulishwa. Kamati Kuu Katika hatua nyingine, leo Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, inatarajia kukutana, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Shein.
    Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, amesema hayo katika taarifa aliyotuma jana kwa vyombo vya habari. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Jabu, kikao hicho kitafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Ofisi Kuu ya CCM, iliyopo Kisiwandui, Mjini Zanzibar.
    Taarifa hiyo imeeleza kuwa kikao hicho pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili taarifa mbalimbali kutoka idara na vitengo vya CCM, kwa maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla.
    Kikao hicho kwa mujibu wa taarifa hiyo, kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar, iliyokutana Jumatano wiki iliyopita, chini ya Mwenyekiti wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
    Kikao hicho cha Jumatano, kimeelezwa kwamba ndicho kilichoandaa ajenda za kikao cha leo na mpaka jana maandalizi ya kikao hicho cha kawaida cha siku moja, yalikuwa yamekamilika. Magufuli na Seif Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli alikutana na Maalim Seif Ikulu ya Dar es Salaam na kujadili hali ya kisiasa ya Zanzibar.
    Kwa mujibu wa Ikulu, wawili hao walikutana kutokana na maombi ya siku nyingi ya Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF). Ikulu ilieleza kuwa mazungumzo ya viongozi hao, pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
    Taarifa hiyo ya Ikulu, ilieleza kuwa, viongozi hao watatu kwa pamoja walijadili hali ya kisiasa Zanzibar na kufurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. Mbali na kufurahishwa na hali ya utulivu, taarifa hiyo ya Ikulu ilieleza kuwa Rais Magufuli aliwapongeza Rais wa Zanzibar, Dk Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif na viongozi wote ambao wamekuwa wakishiriki mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.
    Rais Magufuli pia aliwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.
    Katika mazungumzo hayo, Maalim Seif alimueleza Dk Magufuli juu ya hali ya siasa Zanzibar kadri anavyoielewa yeye; na Rais Magufuli alimshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri, huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi muafaka upatikane.
    Ikulu pia ilisema majadiliano yanayoendelea, yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi, hivyo viongozi hao kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema.
    Rais Magufuli, alimhakikishia Maalim Seif kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, itahakikisha amani na utulivu inaendelea kudumishwa Zanzibar. Kufutwa Uchaguzi Z’bar Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, mwaka huu ulifutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutokana na kasoro zilizobainika katika upigaji kura.
    Hali hiyo imesababisha sintofahamu kwa muda sasa, ambayo imelazimisha kuwepo na vikao vya kusaka mwafaka kuhusu sintofahamu hiyo, ambayo ilivigawa vyama vikuu viwili vya Zanzibar, CCM na CUF.
    CCM yenyewe iliafiki kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu na kupangwa kwa tarehe mpya ya kurudiwa kwa uchaguzi huo, lakini CUF ikikataa kufutwa kwa uchaguzi huo, huku Maalim Seif akijitangaza mshindi kinyume cha taratibu.Created by Gazeti la HabariLeo.

    Mapato ya gesi sasa hadharani

    By: Unknown On: 00:08
  • Share The Gag

  • Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

    WAKATI eneo la kujenga kiwanda cha kuchakata gesi itakayovunwa baharini likitangazwa kupatikana wiki hii, uvunaji utakapoanza Serikali itapata mapato makubwa kutokana na mikataba minono iliyoingiwa.
    Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili wiki hii, Mkurugenzi wa Utafutaji na Uendelezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Kelvin Komba, amesema mfumo wa sasa wa mikataba, unaihakikishia Serikali kupata mpaka asilimia 85 ya faida yote ya kitalu, baada ya kutoa gharama za uzalishaji na ukataji kodi. Kwa mujibu wa Komba, mwekezaji akigundua gesi au mafuta, anatakiwa kurudisha gharama zake zilizotumika katika utafiti na baada ya hapo, faida hugawanywa kati ya Taifa na mwekezaji.
    Taarifa zinaonesha kuwa mpaka sasa Tanzania kumefanyika ugunduzi wa gesi asilia katika eneo la bahari na nchi kavu, inayofikia takribani futi za ujazo trilioni 55.21. “Hata hivyo utajiri huu ili uwe na tija kwa Taifa ni lazima sheria, kanuni, sera na mikataba iwekwe katika namna ambayo inanufaisha Taifa,” alisema Komba.
    Mgawanyo Akifafanua zaidi, Komba amesema Tanzania kwa sasa inatumia mfumo wa Mkataba wa Ugawanaji Mapato (Production Sharing Agreement-PSA), kati ya Taifa na mwekezaji, ambao mgawanyo wa mapato umewekwa kwa asilimia na hutofautiana kulingana na kiwango cha uzalishaji na maeneo ugunduzi ulipofanyika. Kwa mujibu wa Komba, kama ugunduzi ni wa nchi kavu, basi Serikali itapata asilimia 70 hadi 85 ya faida baada ya kodi kwa mafuta na asilimia 60 hadi 80 ya faida hiyo kwa gesi asilia.
    Kama ugunduzi umefanyika katika kina kirefu cha bahari, Komba alisema mgawanyo unakuwa asilimia 60 hadi 85 ya faida baada ya kodi, ambao huongezeka kwa upande wa Serikali kadri uzalishaji unavyoongezeka. Kwa maana hiyo, mwekezaji baada ya kufanya utafiti, kugundua gesi au mafuta, akianza kuzalisha tu na kurejesha gharama za utafiti, katika faida baada ya kodi ataambulia kati ya asilimia 40, kiwango cha juu na asilimia 15, kiwango cha chini.
    Komba anasema kama uzalishaji ni mkubwa, basi mgao wa Taifa nao huongezeka na kama ugunduzi ni wa mafuta pia mgawanyo wa Taifa huwa mkubwa zaidi. “Taifa huchukua mgawanyo zaidi katika mafuta, kwa sababu mafuta yanauzika kirahisi zaidi duniani kuliko gesi na pia miundombinu ya kuendeleza mafuta, haihitaji mitaji mikubwa kama ilivyo kwa gesi asilia,” alisema Komba.
    Aidha, alisema mpaka kufikia sasa mikataba ya PSA 35 imekwishaingiwa kati ya Serikali, TPDC na wawekezaji na kati ya hiyo, mikataba 22 bado inafanyiwa kazi na kampuni 19 ndizo zinazofanya kazi za utafiti na uendelezaji hapa nchini.
    Faida za mkataba Kupitia mfumo huo wa PSA, Komba amesema kampuni au muwekezaji hutumia fedha zake kufanya shughuli zote za awali za utafiti, ikiwa ni pamoja na kukusanya data mtetemo (seismic), ambazo zingine huuzwa na TPDC, kuzifanyia tathmini na kuchimba kisima cha kwanza cha utafiti (exploration well), hatua ambazo ni za gharama kubwa.
    Kwa mujibu wa Komba, kama itatokea hakuna ugunduzi katika kisima hicho, basi fedha yote ya mwekezaji iliyotumika katika uwekezaji hupotea na hasara huwa ni ya kwake. Lakini ikitokea ugunduzi umefanyika, Komba amesema muwekezaji atajirudishia sehemu ya gharama alizoingia wakati wa utafiti, baada ya kuanza kuingiza fedha kwa kuuza gesi au mafuta aliyogundua.
    Faida nyingine, Komba amesema ni pamoja na rasilimali kubaki kuwa mali ya Taifa, huku kampuni au muwekezaji akibeba hatari ya kuwekeza fedha katika utafiti na kukosa rasilimali. Nyingine, mrabaha hulipwa kwa Serikali mwanzoni kabisa mwa uzalishaji, huku urejeshaji wa gharama za mwekezaji ukiwekewa kikomo cha asilimia 50. “Mfumo huu hutoa fursa kwa Taifa kuanza kupata mapato yatokanayo na uzalishaji wa mafuta au gesi asilia mara tu uzalishaji unapoanza,” alisema Komba.
    Urudishaji gharama “Muwekezaji huruhusiwa kujirudishia gharama zake kwa mwaka bila kuzidi asilimia 50 ya gharama zote na faida hugawanywa kati ya muwekezaji na Taifa,” alisema Komba. Kuhusu uwezekano wa Serikali kubambikiwa gharama ambazo hazikuwepo, ili mwekezaji atumie nafasi hiyo kujinufaisha wakati wa kujirudishia gharama, Komba amesema hiyo haiwezekani.
    Akifafanua zaidi, Komba amesema Taifa kupitia TPDC, hupitia mpango kazi na bajeti ya kila mwaka ya muwekezaji na kutoa idhini ya mpango kazi na bajeti hiyo kutumika. Baada ya kuidhinisha bajeti ya mwekezaji, Komba amesema pia TPDC, hufanya ukaguzi wa gharama zote ambazo muwekezaji ametumia ambazo atahitaji kuzirejesha uzalishaji utakapoanza.
    Naye Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa TPDC, Gabriel Mwero, alisema ukaguzi wa gharama anazotumia mwekezaji katika utafiti, hufanyika kwa kila kampuni iliyowekeza katika utafiti hapa nchini. “Aina ya ukaguzi unaofanyika, ni ule wa asilimia 100 na hivyo kuhakikisha kwamba hakuna gharama ambayo haijaangaliwa. Hivyo kampuni hujirudishia zile gharama ambazo zimekaguliwa na TPDC na kuidhinishwa,” alisema.
    Je uvunaji umeshaanza Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa za TPDC, kampuni zilizofanya ugunduzi mkubwa katika kina kirefu cha bahari za BG na Statoil, kiasi cha futi za ujazo zaidi ya trilioni 47.8, hazijaanza kuvuna gesi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hizo, uvunaji hauwezi kufanyika bila kujenga mtambo wa kugeuza gesi asilia kuwa kimiminika, ili ifae kusafirishwa ndani au nje ya nchi.
    Wiki hii ndio TPDC imetangaza upatikanaji wa hati miliki ya ardhi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mtambo huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG), ili iwe kimiminika. Eneo la ardhi hiyo lipo katika kiwanja Na.1-Kitalu “A”, Likong’o katika Manispaa ya Lindi na lilipendekezwa na kuchaguliwa kwa pamoja kati ya TPDC na wawekezaji wa mradi huo.
    Sheria kali Kuhusu udhibiti wa mapato, tayari Tanzania ina Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015, ambayo imeweka adhabu kwa watakaobainika kuchota fedha katika Mfuko wa Mafuta na Gesi utakaoanzishwa na sheria hiyo. Miongoni mwa adhabu hizo ni pamoja na faini isiyopungua kiasi mtu alichochukua au kupoteza, kifungo cha miaka 30 jela na kufilisiwa mali zao.
    Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Mfuko huo wa Mafuta na Gesi utakuwa na akaunti mbili zitakazotunzwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania. Akaunti hizo ni Akaunti ya Kupokea Mapato na Akaunti ya Kutunza Mapato.

    Created by Gazeti la HabariLeo.

    Saturday, 26 December 2015

    Kiongozi wa kundi la waasi auawa Syria

    By: Unknown On: 01:39
  • Share The Gag
  • Alloush ndiye aliyeanzisha kundi la Jaysh al-Islam
    Kiongozi mkuu wa kundi la waasi la Jaysh al-Islam, moja ya makundi yenye nguvu zaidi Syria, ameuawa kwenye shambulio la makombora.
    Zahroun Alloush, 44, ambaye ndiye mwanzilishi wa kundi hilo aliuawa kwenye shambulio la makombora mashariki mwa Damascus alipokuwa kwenye mkutano.
    Aliuawa pamoja na viongozi wengine wa kundi hilo, habari ambazo zimethibitishwa na makundi ya waasi na jeshi la Syria.
    Urusi na Syria zilikataa kutambua mkutano huo wa waasi Saudi Arabia Kundi hilo linaloungwa mkono na Saudi Arabia ni moja ya makundi makubwa ya waasi wanaopigana na Rais Bashar Assad na ngome yake ni maeneo ya Ghouta, mashariki mwa nchi hiyo.
    Majuzi lilihudhuria mkutano mkuu wa wapinzani wa Bw Assad mjini Riyadh, mkutano ambao ulijadili mkakati wa mazungumzo ya Amani na serikali.
    Makombora kumi yanadaiwa kuanguka eneo ambalo makamanda wa Jaysh al-Islam walikuwa mkutanoni, kwa mujibu wa runinga ya al-Arabiya inayofadhiliwa na serikali ya Saudi Arabia.
    Naibu kiongozi wa kundi hilo pia aliuawa.
    Kundi la Jaysh al-Islam limekuwa likipigana katika mji wa Damascus Jaysh al-Islam baadaye walimteua Issam al-Buwaydani – ajulikanaye pia kama Abu Humam – kuwa kiongozi wake mpya.
    Bw al-Buwaydani anatoka mji wa Douma, mashariki mwa Damascus.
    Jeshi la Syria, kupitia taarifa kwenye runinga ya taifa, limesema ndilo lililotekeleza shambulio hilo lakini baadhi ya wanaharakati wanasema lilitekelezwa na Urusi.
    Duru nyingine zimedokeza huenda jeshi la Syria lilitekeleza shambulio hilo likitumia makombora ya Urusi.
    Urusi, ambayo ni mshirika mkuu wa Rais Assad, imekuwa ikitekeleza mashambulio ya angani dhidi ya wapinzani wa Bw Assad tangu mwisho wa Septemba.

    Created by BBC Swahili.

    Operesheni kuondoa wafugaji yasitishwa

    By: Unknown On: 01:35
  • Share The Gag
  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa jimbo lake.

    MAWAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na wa Maliasili na Utalii, wameonya askari wa Wanyamapori wanaojihusisha na utesaji, unyanyasaji na kujipatia fedha haramu kwa kukamata mifugo au wakulima, waache mara moja badala yake, wazingatie maadili ya kazi yao.
    Aidha, Serikali imetangaza kusitishwa kwa operesheni za kuwaondoa wafugaji kwenye maeneo wanayochungia mifugo ikiwemo mapori tengefu, wakati ukifanyika utaratibu wa kuwawezesha kuendesha shughuli zao.
    Matamko hayo yalitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani, kupitia mkutano uliofanyika kati ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba na wafugaji, wakulima wa Kanda ya Ziwa.
    Tamko la mawaziri hao ambalo ni sehemu ya mikakati yao ya kukomesha kero kwa wakulima na wafugaji, limekuja huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, kuhakikisha wanaongeza udhibiti na usimamizi wa migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao husika.
    Katika mkutano uliofanyika juzi katika uwanja wa Mnadani (Benaco) Ngara, mkoani Kagera, Mwigulu aliongozana na Makani ikiwa ni sehemu ya kusikiliza kero na kutafuta utatuzi wa kudumu wa tatizo la malisho linalowakabili wafugaji.
    Wafugaji kupitia Chama cha Wafugaji wa Kanda ya Ziwa (Chawakazi) walilalamikia uonevu kutoka kwa baadhi ya askari wa Wanyamapori na wakaomba serikali iachane na operesheni ya kuwaondoa wafugaji kutoka kwenye maeneo yanayotumika kuchunga ng’ombe katika pori la Burigi.
    Baada ya kusikiliza malalamiko ya makundi hayo, pia Mwigulu alimuomba Naibu Waziri Maliasili kupitia ofisi yake, kuangalia uwezekano wa kupitia upya mapori tengevu ili baadhi wapewe wafugaji na wakulima kwa shughuli zao.
    Akitangaza kusitishwa kwa operesheni za kuwaondoa wafugaji kwenye mapori, Makani aliahidi ofisi yake itafanya haraka iwezekanavyo utaratibu unaoendelea wa kupitia mapori 17 ukamilike ili kutoa maeneo kwa watu wafanye shughuli zao za kilimo na ufugaji.
    Akisisitiza askari Wanyamapori kuzingatia maadili ya kazi yao, Makani alisisitiza kwamba Serikali itachukua hatua kuhakikisha askari wote wanafanya kazi kwa kuheshimu sheria za nchi.
    Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi hivi karibuni, Waziri Mkuu, Kassim, aliagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, kudhibiti migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
    Waziri Mkuu alisema, “Ardhi ni mali ya Serikali lakini maeneo yanayotwaliwa kwa sababu mbalimbali za maendeleo yasiwe chanzo cha migogoro na wananchi tunaowaongoza.” Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema anatambua kuna mgogoro wa eneo la mgodi katika wilaya ya Ruangwa baina ya wananchi na wawekezaji wa kampuni ya Uranex.
    Na hii ni kwa sababu wao ndiyo waliamua kufanya tathmini ya eneo hilo. “Yale ni makosa kwa sababu aliyepaswa kufanya tathmini ni Halmashauri na siyo mwekezaji,” alisema.

    Created by Gazeti La HabriLeo.


    Picha: Lowassa Aanza Kuchunga Ng'ombe Kama Alivyoahidi

    By: Unknown On: 01:31
  • Share The Gag
  • Aliyekuwa mgombea wa uraisi kwa mwavuli wa UKAWA ndugu Edward Lowasa  akichunga ng'ombe zake huko Handeni mkoani Tanga. 
     
    Lowassa yuko mapumzikoni na familia yake katika shamba lake la mifugo lililopo eneo la Mzeri,Handeni mkoani Tanga

    Credit;Mpekuzi blog

    Utafiti: Mimba nyingi hutungwa Krismasi

    By: Unknown On: 01:30
  • Share The Gag
  • Utathmini wa takwimu kuhusu watoto wanaozaliwa Uingereza umebaini mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi kuliko wakati mwingine wowote ule wa mwaka.
    Takwimu hizo za kipindi cha miongo miwili kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu zinaongeza watoto wanaozaliwa huongezeka sana wiki 40 (miezi 9) baada ya msimu wa sikukuu.
    Hili huenda linatokana na wanandoa kutumia muda mwingi pamoja wakisherehekea, au kulenga makusudi mwanzo wa mwaka mpya wa shule ambao huanza mapema Septemba nchini humo.
    “Ongezeko la watoto wanaozaliwa mwishoni mwa Septemba ni ishara kwamba mimba nyingi hutungwa wiki chache kabla ya Krismasi na kuendelea hadi siku chache baada Krismasi kuliko wakati mwingine wowote wa mwaka,” idara hiyo imesema.
    Kawaida watoto 1,800 huzaliwa kila siku lakini idadi hii hupanda hadi 1,974 siku yenye kuzaliwa watoto wengi zaidi ambayo ni Septemba 26.
    Siku zinazoshuhudia idadi ndogo zaidi ya watoto wanaozaliwa ni siku za Krismasi, Boxing Dei na siku ya Mwaka Mpya.
    Hili sana huenda linatokana na idadi ndogo ya watu wanaopangiwa kujifungua kwa kufanyiwa upasuaji siku hizo, kwani huwa ni siku za mapumziko.
    Profesa wa masuala ya uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield Allan Pacey ameambia BBC: “Wazo kwamba mimba nyingi hutungwa wakati wa Krismasi lina msingi. Nina uhakika sherehe na shamra shamra za wakati huu huchangia.”

    Created by BBC Swahili.

    Utumbuaji majipu wazaa matunda

    By: Unknown On: 01:29
  • Share The Gag
  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipotembelea bandarini na kugundua uozo mkubwa bandarini hapo.

    HATUA anazozichukua Rais John Magufuli, katika kukabiliana na ufisadi ndani ya taasisi na idara za Serikali, zimeanza kuzaa matunda. Hatua hizo ambazo zinafahamika kama ‘kutumbua majipu’, pia zimeonesha kuungwa mkono na wasomi, wananchi, washirika wa maendeleo na mataifa mbalimbali ya nje.
    Mathalani, kutokana na juhudi hizo za Rais, makusanyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yameongezeka kutoka Sh bilioni 900 hadi Sh trilioni 1.3 kwa mwezi. Pia, Serikali imeboresha ukusanyaji wa mapato katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhimiza matumizi ya mfumo wa kielektroniki.
    Kwa upande wa reli, Serikali imetangaza kuwa itaanza kujenga reli ya kisasa (standard gauge) kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Bara hivi karibuni, ili kuboresha usafiri kwa wananchi na kuongeza mizigo inayosafirishwa.
    Hata hivyo, wizara iliyoathirika zaidi na hatua hizo za Rais ni Uchukuzi, ambayo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Magufuli hivi karibuni, Wizara ya Uchukuzi imeunganishwa na Wizara za Ujenzi na ile ya Mawasiliano; na sasa kutambulika kama Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
    Wizara hiyo ya Uchukuzi ilikuwa na taasisi zipatazo 13 zilizo chini yake. Hadi sasa Rais Magufuli ameshashusha rungu kwa taasisi tatu za juu, huku ikitarajiwa rungu hilo kuendelea kuzitafuna idara nyingine.
    Taasisi ambazo zilikuwa chini ya Wizara ya zamani ya Uchukuzi ni Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Shirika la Huduma za Meli (MSCL), Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na TPA.
    Nyingine ni Shirika la Ndege (ATCL), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kampuni ya Reli (TRL), Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Chuo cha Bahari (DMI), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) . Taasisi ambazo zimekamuliwa majipu yake hadi sasa ni TPA, RAHCO na TRL.
    Tayari watendaji wakuu wa TPA na RAHCO, wamesimamishwa kazi na kuvunjwa bodi za wakurugenzi wa taasisi hizo; pamoja na bodi ya TRL na baadhi ya maofisa wake wa juu, wakiamuriwa kuchunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
    Rais alitengua utezi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka kutokana na kushindwa kwake kusimamia vyema taasisi hizo zilizo chini yake na pia alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadhi Massawe.
    Bodi ya TPA ambayo ilianza kazi Juni 2, mwaka huu ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Joseph Msambichaka na wajumbe wake walikuwa Naibu Spika wa Bunge wa sasa, Dk Tulia Akson, Musa Ally Nyamsingwa, Donata Mugassa, Haruna Masebu, Gema Modu, Dk Francis Michael, Crescentius Magori, Flavian Kinunda nayo ilivunjwa.
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye aliwashushia rungu watendaji wengine wa TPA kwa kuwasimamisha kazi, ambao ni viongozi watano wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari bila kulipa kodi pamoja na watumishi wanane wa bandari kavu, ambao walihusika na ukwepaji kwa makontena 2,387.
    Wiki hii Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasimali za Reli (RAHCO), Benhadard Tito na kuivunja Bodi ya Wakurugenzi iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Mwanuzi Fredrick.
    Mkurugenzi wa Rahco, Benhadard Tito mbali na kusimamishwa kazi, lakini Rais Magufuli ameagiza kuchunguzwa kwa kina na Takukuru kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi, uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.
    Majipu yaliyokamuliwa katika taasisi hizo tatu ,yamesababisha hadi taasisi zilizo chini ya wizara nyingine kama TRA iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango na Takukuru iliyo chini ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, nazo watendaji wake kuathirika kutokana na makosa yaliyofanywa na taasisi zilizokuwa Wizara ya Uchukuzi.
    Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade kutokana na ubadhirifu wa mapato katika Bandari ya Dar es Salaam na pia alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah.

    Created by Gazeti la HAbariLeo.


    Rais amzuia mwanamume kujiua Uturuki

    By: Unknown On: 01:26
  • Share The Gag
  • Mwanamume huyo alikuwa anatatizwa na msongo wa mawazo
    Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimshawishi mwanamume, aliyetaka kujiua kwa kujirusha kutoka kwa daraja, kubadilisha nia yake na kutojiua, afisi yake imesema.
    Mwanamume huyo alikuwa amepanga juu ya uzio wa daraja la Bosphorus, linalounganisha Ulaya na bara Asia na alikuwa anatishia kujiua.
    Msafara wa magari ya Bw Erdogan ulikuwa unapita kwenye daraja hilo mjini Istanbul wakati huo.
    Picha zilizoonyeshwa kwenye televisheni zilionyesha wahudumu wa Bw Erdogan wakimsihi mwanamume huyo aliyekuwa akitokwa na machozi kuzungumza na rais.
    Mwanamume huyo alitembea hadi kwenye gari la rais huyo na wakazungumza.
    Erdogan alizungumza naye akiwa ndani ya gari lake, na akiwa ameweka simu kwenye sikio moja Baada ya muda mfupi, alisindikizwa kutoka eneo hilo.
    Mwanamume huyo alikuwa akitatizwa na msongo wa mawazo kutokana na matatizo ya kifamilia, na polisi walikuwa wamejaribu kumzuia asijirushe kwa saa mbili bila mafanikio, shirika la habari la Dogan limeripoti.
    Afisa wa afisi ya rais huyo ameambia shirika la habari la Associated Press kwamba kiongozi huyo aliahidi kumsaidia.
    Polisi walikuwa wamejaribu kumshawishi aondoke bila mafanikio 
     Created by BBC Swahil.


    Magufuli Awakuna Viongozi Wa Dini.....Maaskofu Wahimiza Aombewe Ili Aendelee Kutumbua Majipu

    By: Unknown On: 01:23
  • Share The Gag

  • Viongozi wa makanisa mbalimbali nchini, wametoa salamu za Sikukuu ya Krismasi jana, wakielezea kufurahishwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli. 


    Wamesisitiza waumini wao, kumuombea Rais na kuwataka wananchi kutii mamlaka, kwa kuwa yamewekwa na Mungu. 

    Viongozi hao pia, wamewataka watendaji wa Serikali na wananchi walioshiriki ukwepaji kodi, watubu dhambi zao na kurejesha vyote walivyochukua, ambavyo si halali yao.

    Pia, wamempa moyo Rais Magufuli kuendelea kutumbua majipu, kwani hata Bibilia inatambua kazi hiyo. 
    Mbali na ujumbe huo wa viongozi wa dini kwa waumini wao na kwa Watanzania kwa ujumla, Rais Magufuli mwenyewe alishiriki katika ibada ya sikukuu hiyo katika Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwatakia Watanzania wote Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya na kusisitiza waendelee kumuombea yeye na viongozi wengine.

    Baada ya kuwatakia sikukuu njema Watanzania, Rais Magufuli aliwakumbusha wananchi kwamba ustawi wa nchi, unatokana na watu kufanya kazi, hivyo baada ya shamrashamra za msimu wa sikukuu, warejee kufanya kazi kwa bidii kwa ujenzi wa Taifa. 
    Dodoma wamuombea 
    Mkoani Dodoma katika shamrashamra hizo, Askofu Amos Kinyunyu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Dodoma, aliwataka Watanzania kuzidi kumuombea Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi unaowagusa Watanzania wa hali ya chini.

    Alisema wao kama Kanisa, wataendelea kumuombea ili afanye kazi anayoendelea kufanya sasa hivi, kwani hata vitabu vitakatifu, vinataka usawa katika uchumi na kipato kwa kila mtu. 
    ‘’Tunawaomba Watanzania wazidi kumuombea Rais wetu kasi aliyonayo aendelee kuwa nayo, kwani Mungu anapenda haki katika maisha pamoja na uchumi ulio sawa.

    ‘’Wakati mwingine hii kauli ya Hapa Kazi Tu, inakuwa hata sisi inatuogopesha, lakini Mungu ataendelea kumlinda na kumwongoza,’’ alisema. 
    Ni jibu la Kanisa 
    Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assembles of God la Miyuji Dodoma, Samson Mkuyi alisema utawala wa Rais Magufuli, unaonekana ni jibu la Watanzania wengi pamoja na Kanisa.

    Mchungaji Mkuyi alisema wamefurahishwa na utendaji kazi wake hasa upande wa maadili, ikizingatiwa kuwa Kanisa linataka maadili ya kiroho na kimwili.
    ‘’Tulianza kuomba haya miaka mitano, sisi Kanisa tunamwambia asiogope kwani Mungu yupo pamoja na yeye, tunaendelea kumuombea ili Mungu aendelee kumpa ulinzi,’’ alisema. 

    Atumbue zaidi 
    Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk Dickson Chilongani alisema; ”Rais ameonekana kutumbua majipu yaliyokuwa yamejificha na katika hili tutaendelea kumuombea ili ayatumbue zaidi, pia na kuwafanya watendaji wafanye kazi kwa usahihi,’’ alisema.

    Rais amepatikana 
    Kanisa la KKKT Dayosisi ya Morogoro mbali na kurejea umuhimu wa kumuombea Dk Magufuli, liliwataka viongozi wote walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali, wajitoe kikamilifu kuwatumikia na kuwahudumia wananchi wakiweka mbele maslahi ya taifa. 

    Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob Paulo ole Mameo, wakati wa mahubiri yake alitaka vyama vyote vya siasa, kutanguliza maslahi ya Taifa mbele na kusema mwito wa Kanisa ni sasa tusonge mbele, uchaguzi umemalizika na Rais amepatikana.

    “ Rais wetu ameanza kazi yake vizuri na sasa tumuunge mkono , tushirikiane kwa misingi ya umoja, upendo na amani katika kujenga Taifa na tuliombee lisonge mbele.

     “Wale viongozi waliozoea kutenda uovu sasa waache, wasijiingize tena huko, tunataka wawe mfano mzuri katika kuonesha uadilifu wao kwa kusimamia huduma bora mbele ya jamii,” alisema Askofu Mameo. 


    Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, yeye alisisitiza waumini kuhubiri upendo na kudumisha amani iliyopo.

    Alipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa hatua zake za kuwajali watu wanyonge, ili wapate huduma bora za kijamii ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu, uadilifu na utendaji unaozingatia sheria za nchi. 

    Wakwepa kodi watubu 
    Katika Kanisa la KKKT Usharika wa Maili Moja Kibaha, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Isai Ntele, aliwataka watu waliokuwa wakijihusisha na ukwepaji kodi hapa nchini, kutubu mbele za Mungu na kurejesha kile walichokwepa na kuonesha utii kwa mamlaka iliyopo madarakani, kwani imewekwa na Mungu.

    Mchungaji Ntele alisema Mungu alisikiliza kilio cha Watanzania kwa kuwapa kiongozi ambaye ana uchungu na wananchi wake, kwani ameonesha dhahiri kuwa hataki haki za wanyonge, zipotee kwa kudhulumiwa na wachache.

     “Hata Biblia inasema kila mtu aitii mamlaka iliyo Kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo nimeaminiwa na Mungu, hivyo asiye na mamlaka asipotii, anashindana na agizo la Mungu hivyo watapata hukumu,” alisema.

    Wanatufananisha na mbinguni
     Mkoani Shinyanga, Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, alisisitiza umuhimu wa kumwombea Rais Magufuli aliyeonesha nia ya kuwatumikia wananchi bila upendeleo, ambaye ameonesha wazi wazi kuwa anamtanguliza Mwenyezi Mungu. 

    "Kuna baadhi ya watu wanataka kutusadikisha kuwa Tanzania hakuna amani kwa nia zao wenyewe, labda wakilinganisha Tanzania na mbinguni ni sawa, kwa sababu mbinguni kuna utimilifu wake wote, lakini ukilinganisha Tanzania na mataifa mengine, ndugu zangu tuna amani ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote.

    “Wapo wengi wangetamani tuchinjane hapa nchini, wana wivu na chuki na nchi yetu na pengine wanaweza hata kutumia viongozi mbalimbali kupenyeza mambo yao, ili tuchukiane sisi kwa sisi, tuwakemee watu wanaodharau hii amani iliyopo,” alisema Askofu Sangu. 

    Alisema Tanzania hata bomu likilipuka, watu wanakimbia kwenda kutazama, lakini kwa nchi zenye machafuko, likilipuka bomu hakuna anayekwenda pale kwa kuhofia kifo na hiyo ni dalili tosha kuwa kuna amani.

    Askofu Sangu aliwataka Watanzania kusherehekea sikukuu kwa upendo hususani katika ngazi ya familia na kuhamasisha watu kuishi kwa kupendana na kuepuka vitendo vya kupeana ujumbe wa kujengeana chuki, kwani ndiyo chanzo cha vurugu katika jamii na taifa kwa ujumla.

     Dar na mabadiliko ya kweli
     Mkoani Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema mabadiliko ya kweli yanaletwa na watu ambao wako tayari kufanya kazi kwa dhati usiku na mchana na si matajiri.

    Akitoa mahubiri yake kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph lililoko Posta jijini Dar es Salaam, katika Ibada ya usiku wa Mkesha wa Sikukuu ya Krismasi, alisema katika fikra za mabadiliko, watu wa kawaida waliaminishwa kwamba hawana mchango wanaoweza kuutoa katika mabadiliko. 

    “Mara nyingi sisi watu wa kawaida tulisadikishwa kwamba hakuna mchango tunaoweza kuutoa ili kuleta mabadiliko katika jumuia yetu, tulisadikishwa kwamba watu wanaokuwa na fedha na mali nyingi hao ndio wanaoweza kuleta mabadiliko katika jumuiya yetu,” alisema Pengo.

    Alisema sasa mawazo hayo yamekwishatambuliwa kuwa hayakuwa sahihi, kwani watu wenye mali si wanaoweza kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika jumuiya ya watu. 

    “Watakaoleta mabadiliko ni wale ambao haidhuru nafasi yao ni ipi katika jumuiya, lakini wako tayari kufanya kazi usiku na mchana, ili kuhakikisha kwamba hali ya kibinadamu inakuwa nzuri zaidi na huo ndio ujumbe unaopaswa kupokelewa kutoka kwa malaika aliowaendea wachungaji na kuwaambia msiogope,” alisema Pengo.

    Askofu Pengo alisema na kupitia ujumbe huo wa malaika, Tanzania inaambiwa usiogope, kwani unayo habari njema, ambayo ni kuwa tayari kufanya kila linalokuwa ndani ya uwezo wake ili hiyo habari njema iifikie. 

    Aliwataka Watanzania wamuombe Mungu awajaalie neema ya kutambua kila mmoja anaweza kuwa chimbuko la habari njema na mabadiliko, si tu katika mazingira ya imani ya kidini, lakini katika mazingira hata ya kiuchumi na kisiasa.

    Alisema watu hawapaswi kuogopa, bali kulinda makundi yao wakisubiri habari njema na habari hiyo si kwa ajili ya matajiri wanaoishi katika majumba ya kifahari, bali kwa ajili ya wote, habari ambayo ni ya furaha ambayo ni chimbuko la heri kwa wanadamu wote. 

    “Habari hii siyo kwa ajili ya matajiri, siyo kwa ajili ya wale wanaoishi katika majumba ya kifalme ni habari ya furaha ambayo itakuwa chimbuko la furaha na heri kwa wanadamu wote, Mwenyezi Mungu atujaaliye hilo katika Taifa letu,” alisema Pengo.

    Magufuli asisitiza kazi 
    Wakati viongozi wa dini wakihamasisha Watanzania kumuombea, Rais Magufuli mwenyewe alihudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. 

    Akiwa katika ibada hiyo, alipewa nafasi ya kutoa salamu, ambapo aliwatakiwa Watanzania wote sikukuu njema ya Krismasi na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani wakikumbuka kufanya kazi baada ya shamrashamra za sikukuu.

    Rais Magufuli alisema watu wakumbuke kwamba ustawi wa nchi unatokana na watu kufanya kazi ndio maana anasimamia kaulimbiu yake ya Hapa Kazi Tu.

     “Tunaposherehekea sikukuu hizi, tukumbuke ya kwamba baada ya shamrashamra ni kufanya kazi kwa bidii kwa ujenzi wa Taifa letu,” alisema Rais Magufuli.
    Credit;Mpekuzi blog

    Waziri Mkuu Kesho Kuanza Ziara Ya Kikazi Mkoani Kigoma

    By: Unknown On: 01:18
  • Share The Gag
  • WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliw  (pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma.
     
    Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa kesho majira ya saa tatu asubuhi.
     
    Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.
     
    Baada ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo
     
    Na siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam.
    Credit; Mpekuzi blog

    Friday, 25 December 2015

    ‘Viongozi wa dini pigeni vita dawa za kulevya’

    By: Unknown On: 00:44
  • Share The Gag
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja na baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid baada ya kuhutubia baraza hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

    WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuungana kwa pamoja na kushiriki katika vita ya dawa za kulevya, kwani ushiriki wao utaweza kumaliza vita hiyo, ambayo ni ngumu na inaliangamiza Taifa. Amesema uwezekano wa kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya nchini upo, iwapo viongozi wa dini watakuwa mstari wa mbele kuhubiri madhara ya dawa hizo, ambazo zinaangamiza nguvu kazi kubwa ya taifa.
    Majaliwa aliyasema hayo jana katika sherehe za Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad, zilizoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), zilizofanyika katika viwanja vya Kariamjee jijini Dar es Salaam, ambapo pia viongozi mbalimbali walishiriki.
    Alisema, wazazi na viongozi wa dini, wanapaswa kukemea na kuhubiri juu ya madhara ya dawa za kulevya mara kwa mara ili kuweza kuchangia katika kumaliza vita hiyo ambayo imekuwa ni tatizo linalowamaliza vijana wengi.
    Aidha, Waziri Mkuu alizitaka taasisi za kidini, kuendelea kutoa huduma kwa jamii nzima bila ubaguzi ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo yaliyopangwa, huku wakiifundisha jamii kuwa wachamungu ili kupunguza maovu.
    “Kama kila mmoja atajua umuhimu wa kuwa Mcha Mungu, basi Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani. Mcha Mungu ni mtu ambaye anazingatia maadili na kufuata mafundisho yote ya Mwenyezi Mungu.
    Hatutarajii kuona mcha Mungu anakuwa mstari wa mbele katika kutenda maovu na mambo yasiyompendeza Mungu, tutakapokuwa na wachaMungu wengi, maana yake hata maovu yatapungua,”alisema Majaliwa.
    Alisema, kwa pamoja Tanzania inatakiwa kutokukubali kuwa na jamii isiyokuwa ya wacha Mungu, ambapo aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha wanaiongoza jamii ili iweze kuishi katika uhuru, umoja na mshikamano.
    “Tuna jukumu kubwa la kuhakikisha watu wetu wanaishi kwa uhuru, umoja na mshikamano, kwani hakuna taifa lililoweza kupiga hatua bila kushikamana, kama wanavyosema umoja ni nguvu... tushikamane ili tuweze kufikia malengo ya kuwa na maendeleo,” alisema.
    Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakari Zubeir alisema Bakwata na waislamu wote nchini, wanaunga mkono juhudi na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais John Magufuli katika kupiga vita ufisadi.
    Alisema ufisadi ni jambo ambalo halikubaliki, kwani hata Kitabu Kitakatifu cha Quran, kimeeleza jinsi gani Mwenyezi Mungu anavyochukizwa na watu wanaofanya uharibifu. “Katika Quran....Mwenyezi Mungu kaeleza wazi jinsi anavyochukizwa na uharibifu, na ufisadi ni uharibifu kwa maana hiyo wanaofanya ufisadi wanaenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu,” alisema Sheikh Zubeir.
    Aliwataka waislamu kukumbuka na kuyafuata mafundisho ya Mtume Muhammad, kwani miongoni mwa mafundisho hayo ni tabia njema, maadili na kutenda wema, pia Waislamu kuwa chanzo cha amani na salama mahali popote.
    Alisema Waislamu hawana budi kuendelea kuishi kwa amani na utulivu, kwani vitendo vya chuki si mafunzo ya Kiislamu na yanamchukiza Mwenyezi Mungu. Hata hivyo, aliomba Serikali kutambua mchango wa viongozi na taasisi za dini katika kuchangia, amani, utulivu na maendeleo katika Taifa.
    Pia kutambua dhamana yao katika jamii na kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ili kuepusha migongano katika jamii.

    Created by Gazeti la HabariLeo.

    Waasi waunda vuguvugu dhidi ya Nkurunziza

    By: Unknown On: 00:35
  • Share The Gag
  • Waasi waunda vuguvugu dhidi ya Nkurunziza
    Waasi wanaompinga Rais Pierre Nkurunziza wameungana kuunda vuguvugu moja linalofahamika kama The Republican Force of Burundi, na limetangaza vita dhidi ya kiongozi huyo.
    Kubuniwa kwa vuguvugu hilo kunatukia huku shinikizo kutoka kwa mataifa ya kanda hiyo, zikiongezeka.
    Umoja wa Afrika unaitaka serikali ya Nkurunziza ikubalie walinda amani wa Umoja wa Afrika.
    Hata hivyo serikali yake imekatalia mbali ombi hilo ikidai kuwa, haiko katika hali ya mapigano yawenyewe kwa wenyewe wala hakuna hatari ya kuibuka kwa mauaji ya kimbari kwa hivyo inaichukulia jeshi hilo la kulinda amani kama jeshi la kigeni na "kikosi cha uvamizi".
    Umoja wa Afrika unaitaka serikali ya Nkurunziza ikubalie walinda amani wa Umoja wa Afrika. Tanzania imejitokeza kupinga mpango huo wa AU wa kuwatuma wanajeshi elfu tano, wa kulinda amani wanaopangiwa kwenda Burundi, kusaidia kukomesha ghasia na umwagikaji zaidi wa damu.
    Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga, yuko katika ziara ya kidiplomasia nchini Uganda na kisha Burundi kuhusiana na mzozo huo katika taifa hilomojawepo ya kanda ya Afrika Mashariki.
    Rais wa Uganda anatarajiwa kuongoza mchakato wa amani kuanzia jumatatu Msemaji wa serikali ya Burundi Willy Nyamitwe amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa hofu ya kuibuka kwa kundi lipya la waasi sio tishio katika serikali ya Burundi.
    Nyamitwe anasema kuwa Republican Forces of Burundi, ama "Forebu" haitadumu.
    ''sio mara ya kwanza kwa makundi ya waasi kuibuka hapa Burundi. Tutawakanyaga mara moja''
    Nyamitwe anasema kuwa Burundi ina haki ya kimsingi ya kulinda maisha na usalama wa wananchi wake na kuwa haitachelewa kuwazima mara moja.

    Created by BBC Swahili.

    Serikali Yatangaza ‘Kuminya’ AJIRA za Wageni......Wanaoishi Nchini Bila Kibali Kukiona cha Moto

    By: Unknown On: 00:29
  • Share The Gag

  • Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameagiza waajiri kote nchini kutowapa ajira wageni kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.

    Pia, ameagiza maofisa wa Idara ya Uhamiaji kufanya operesheni maalumu kuwatimua raia wote wasio na vibali vya kuishi nchini ifikapo Januari 31, 2016.

    Kitwanga ambaye alitembelea idara hiyo jana, alisema wizara yake kwa kushirikiana na Uhamiaji imeanzisha operesheni ya kuwakamata raia wote wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria na kuwachukulia hatua stahiki.

    Waziri huyo alisema kutokana na watu wengi kuishi nchini bila vibali, amewapa mwezi mmoja Idara ya Uhamiaji kufanya uchunguzi katika maeneo yote ya kazi na makazi, ili kuwaondoa walioingia nchini kinyemela.

    “Katika operesheni hii, tutahakikisha tunawakamata wote na nimetoa maelekezo kwamba nitakuwa nikipewa ripoti kila Ijumaa kuanzia wiki ijayo, mpaka ifikapo Januari 31 tuwe tumesafisha nchi kabisa,” alisema Kitwanga.

    Alisema kutokana na mpaka wa nchi kuwa mkubwa, Uhamiaji watawezeshwa ili kukabiliana na tatizo la upitishwaji wa wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali, kama ilivyoripotiwa hivi karibuni.

    Pia, alitoa agizo kwa wananchi wa kawaida kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu wahamiaji haramu walioweka makazi katika maghala, kampuni na viwanda bubu ili kumaliza tatizo la wahamiaji haramu nchini.

    Wafanyakazi wageni
    Mbali na maagizo hayo, Kitwanga pia aliagiza wamiliki wa kampuni mbalimbali kuhakikisha hawatoi ajira kwa raia wa nje kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.

    “…Lakini kazi zote ambazo Watanzania wana utalaamu wa kuzifanya zitafanywa na wazawa na si wageni na zile ambazo inaonyesha wazi kwamba Watanzania hawana ujuzi huo, basi zifanywe na wageni,” alisema Kitwanga.

    Kuhusu vibali, Waziri Kitwanga alisema hakuna raia yeyote wa kigeni atakayepata kibali cha kuishi nchini kama hajapata kibali cha kufanya kazi kama amekuja kwa ajili ya kazi. Lakini utaratibu mwingine kama mtu amekuja likizo utaendelea kama kawaida.

    Kitwanga alisema kuanzia Jumatatu ijayo, viongozi wa wizara husika na uhamiaji, wakae wapange utaratibu mzuri utakaoonyesha kwamba hakuna usumbufu kwa raia wa kigeni ambaye anakuja kufanya kazi nchini kwa kuzingatia vigezo.

    Pasi za kusafiria
    Aidha, Waziri Kitwanga alisema mfumo wa uombaji wa pasi za kusafiria na vibali vya ukazi, hivi sasa utakamilishwa kwa njia ya Tehama.

    Alisema mwombaji atatakiwa kufanyiwa mahojiano ya ana kwa ana pindi atakapokamilisha utaratibu wa kujaza na kuzilipia fomu hizo benki, na atapatiwa pasi ya kusafiria baada ya siku tatu huku kibali cha ukazi akikipata baada ya siku tano ili kupunguza urasimu.

    “Tumeafikiana uboreshaji wa namna ya kufanya kazi na kwa mtazamo wa mbali,” alisema.
     Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo.
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi  wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
    Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam jana. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
    Credit;Mpekuzi blog

    Papa awataka Wakristo wasiongozwe na mali.

    By: Unknown On: 00:26
  • Share The Gag
  • Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewashauri waumini 1.2 bilioni kanisa hilo “walileweshwe” na mali na utajiri.
    Akitoa mahubiri yake ya kila mwaka siku ya Krismasi, Papa Francis aliwataka wafanye mambo kwa kiasi. Amesema ulimwengu wa sasa umetawalia na “kutumia mali kwa wingi, anasa na utajiri”.
    Papa alikuwa akiongoza maadhimisho ya mkesha wa Krismasi katika mida ya St Peter's Basilica mbele ya waumini takriban 10,000.
    Baadaye leo Ijumaa, atatoa ujumbe wa kila mwaka wa Krismasi kutoka kwenye roshani ya mida ya kanisa hilo la St Peter's.
    Alipokuwa akiongoza ibada ya misa, Papa alisema Krismasi ni wakati mwingine wa kujitambua na kujitafakari.
    Aliwahimiza waumini kuonyesha maisha ya ukawaida kama alivyofanya mtoto Yesu, “alipozaliwa katika maisha ya ufukara katika zizi la ng’ombe licha ya utukufu wake” kama mwongozo katika maisha yao.
    “Katika jamii hii ambayo kawaida imeleweshwa na mtindo wa kutumia mali kwa wingi, anasa na utajiri, mtoto huyu anatuhimiza tufanye mambo kwa kiasi, kwa njia ambayo ni rahisi, ya kufanya mambo kwa kipimo, na kufanya mambo yaliyo ya muhimu,” alisema.
    Papa Francis amewahimiza Wakristo kuwa wanyenyekevu
    “Katika utamaduni huu wa siku hizi wa kutojali ambao mara nyingi hugeuka na kuwa ukatili, mtindo wetu wa maisha unafaa kuwa wa kujitolea, upendo, kuhurumia wengine na msamaha.”
    Usalama uliimarishwa wakati wa ibada hiyo na polisi walikuwa wakipekua watu na magari maeneo yaliyo karibu na Vatican.
    Wote walioingia kwenye kanisa hilo, ambalo ndilo kubwa zaidi duniani, walilamika kupitia kwenye mitambo ya kupekuwa watu kutambua vyuma.
    Waandishi wa habari wanasema Papa Francis, 79, alitumia mahubiri hayo kuangazia mada kuu ambazo ameangazia katika uongozi wake – msamaha, huruma, kuhisi hisia za watu wengine na kutenda haki.
    Sauti yake ilikuwa hafifu wakati mwingine, kutokana na mafua yaliyokuwa yamempata mapema wiki hii.

    Credit by BBC Swahili.

    Serikali Yapiga Marufuku Matangazo Yote Yanayohusu Tiba asili na Tiba Mbadala Kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii.

    By: Unknown On: 00:04
  • Share The Gag

  • Taarifa kutoka Wizara ya Afya kuanzia tarehe 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

    Wale wote wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

    Utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

    Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia jana Desemba 2015. 

    Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala

    Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia jana  24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote  zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

    Taarifa hii imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu Mkuu.
    Credit; Mpekuzi blog

    Thursday, 24 December 2015

    Serikali Yawapiga STOP Akina Lowassa Na Wenzake Kufanya Mikutano ya Hadhara

    By: Unknown On: 23:59
  • Share The Gag

  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu hawaruhusiwi kuitisha mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa kuwa wanaweza kuvuruga shughuli za maendeleo.

    Waziri Mkuu alisema hayo wakati akilishukuru Jeshi la Polisi wilayani Ruangwa kwa kufanya kazi ya kusimamia Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25 kwa CCM kushinda kiti cha urais na kuzoa takriban viti 180 vya ubunge.

    “Naendelea kuwashukuru kwa mchango wenu mkubwa kiulinzi, lakini pia usimamizi wa zoezi zima la uchaguzi na hatimaye hivi sasa watu wameshapatikana,” alisema Waziri Majaliwa nje ya ofisi za jeshi hilo.

    “Na tumesema, siasa tumeshazimaliza. Sasa tunataka tufanye kazi za maendeleo. Hatuhitaji tena watu kuja kutuvuruga. Mikutano ya shukrani itafanywa na wale tu walioshinda kwenye maeneo yao. Wengine watulie.

    “Vyama sasa viache wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao washukuru, wengine hawa watakuja kuleta maneno ambayo yatatuvuruga. Mimi naamini mko imara.”

    Wakati Waziri Majaliwa akisema hayo, tayari Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea urais wa Chadema na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alishapanga kuanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kuwashukuru wananchi waliompigia kura.

    Hata hivyo, ilipofika siku ya kuanza ziara hiyo, Chadema ilitangaza kuwa imeahirisha hadi itakapotangazwa tena, ikiweka bayana kuwa uamuzi huo hautokani na vitisho vya makamanda wa polisi wa mikoa.

    Awali, amri ya kuzuia mikutano ya kisiasa ilikuwa ikitolewa kwenye mikoa na baadhi ya makamanda wa polisi, lakini tamko hilo la juzi la Waziri Majaliwa linatia msumari marufuku hiyo ya kuendesha shughuli za kisiasa kwa hoja ya kushukuru wananchi.

    Lowassa, ambaye alihamia Chadema siku chache baada ya kukatwa jina lake na CCM mwezi Julai, aliweka rekodi ya kuwa mgombea wa upinzani aliyepata kura nyingi baada ya kupigiwa kura na watu milioni 6.07 ikiwa ni asilimia 39.9, huku mshindi akipata kura milioni 8.88 sawa na asilimia 58.46.

    Tamko hilo la Waziri Majaliwa tayari limeanza kupingwa sehemu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kwenye mitandao ya jamii na vyama vya siasa kutoa matamko.

    “Hii ni kauli ya ajabu kutolewa na mtu anayesimamia utendaji wa shughuli za kila siku za Serikali inayotaka kuwaaminisha (wananchi) kuwa itakuwa tofauti na serikali nyingine zilizopita za CCM,” inasema Chadema katika tamko lake la jana jioni kujibu kauli ya Waziri Majaliwa.

    “Kama wao (CCM) ndiyo walioshinda kama ambavyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema na kwamba wanaendelea kutekeleza wajibu waliokabidhiwa na wananchi, tunahoji hofu yao nini hasa wakiona au wakisikia Chadema wanapanga kwenda kuongea na wananchi? Wanaogopa nini?”

    Taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano, Chadema imesema kuwa waziri Majaliwa ametoa tamko hilo siku chache baada ya kufanya mkutano mjini Lindi uliowabagua wananchi kwa itikadi zao kwa kutoa nafasi kwa chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM kuhutubia na kufanya siasa.

    “Matukio haya yanaanza kumdhihirisha Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi mwenye uelekeo wa namna gani hivyo kuanza kuifunua Serikali ya Rais John Magufuli chini ya CCM kwa miaka mitano ijayo itawapeleka wapi Watanzania,” inaeleza taarifa hiyo.

    “Ni dalili za wazi za watu waliolewa madaraka na kuchoka kuwa viongozi na sasa wanataka kuwa watawala wenye kudhani kuwa fikra zao ndizo zinazongoza nchi badala ya misingi ya inayokubalika miongoni mwa jamii nzima kupitia Katiba, Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali.”

    Naye makamu mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema uamuzi huo ni kinyume na Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa na kwamba Serikali inazuia wapinzani kufanya mikutano ya kushukuru wananchi kwa kuwa inajua watatoa ushahidi wa jinsi kura zilivyoibwa.

    “Wanatuzuia kwa sababu wanajua tutakwenda kutoa ushahidi wa jinsi CCM ilivyoiba kura za urais na ubunge,” alisema Profesa Safari.

    “Kiongozi anaweza kuzuia mkusanyiko iwapo tu nchi itakuwa katika hali ya hatari. Jambo hili hata Rais hawezi kulizua kienyejienyeji tu,” alisema Profesa Safari ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

    Alisema Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 imeeleza wazi majukumu ya vyama vya siasa, kuwa ni pamoja na kufanya mikutano na maandamano.

    Pamoja na tamko la Waziri Mkuu kumruhusu kufanya mikutano kutokana na ukweli kuwa alishinda uchaguzi wa ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alizungumzia marufuku hiyo kuwa ni kauli ya kisiasa isiyo na mantiki.

    “Mikutano inaratibiwa na Sheria ya Vyama vya Siasa. Hii kauli ya Majaliwa naona kama ilikuwa ya kisiasa zaidi. Jeshi la polisi ndilo lenye jukumu la kuzuia mikutano na litafanya hivyo kama kutakuwa na hali ya hatari na si vinginevyo,” alisema Zitto.

    Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alimtaka Waziri Mkuu kujikita katika uwajibikaji badala ya kuingilia vyama vingine.

    “Sheria hairuhusu mtu yeyote kuzuia mikutano ya kisiasa isipokuwa kama kuna tishio la vita,” alisema Sungusia.

    “Kuruhusu baadhi ya watu kufanya mikutano na wengine kuwazuia ni kuwanyima haki watu.”    
    Credit; Mpekuzi blog