Maafisa wa polisi
waliokuwa wakiutafuta mwili wa mvulana wa miaka 2 aliyenyakuliwa na
mamba katika bustani ya shirika la Walt Disney World mjini Florida
wameupata mwili wake.
Mkuu wa kaunty ya Orange Jerry Demings amesema kuwa jina la mvulana aliyetoweka na mamba huyo ni Lane Graves kutoka Nebraska.
Tangu shambulio hilo mamba watano walikamatwa na kuuawa kwa lengo la kutafuta mabaki ya mwili wa kijana huyo.
Mwili uliopatikana majini bado haujatambuliwa rasmi lakini maafisa wa polisi wana imani ni ule wa Lane.
Mapema siku ya Jumatano maafisa wa polisi walisema kuwa hakuna tashwishi kwamba mvulana huyo alifariki.
Chanzo BBC.
0 comments:
Post a Comment