Monday, 30 November 2015

Serikali Yazungumzia Tishio la Marekani Kusitisha Misaada Tanzania

By: Unknown On: 00:55
  • Share The Gag

  • Serikali imezungumzia tishio la Serikali ya Marekani la kusitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania kutokana na mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kukamatwa kwa maofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

    Ofisi ya Ikulu jana ilisema masharti yaliyotolewa na Serikali ya Marekani yanatekelezeka na yatamalizwa kabla ya kikao cha Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) kukaa Desemba, mwaka huu.

    Wiki iliyopita, Serikali ya Marekani iliitaka Serikali ya Tanzania kumaliza haraka mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, vinginevyo upo uwezekano wa kusitishwa msaada wa zaidi ya Dola za Marekani milioni 472 (Sh. bilioni 999.4), za awamu ya pili ya fedha za MCC la nchi hiyo.

    Fedha hizo za MCC awamu ya pili ni kwa ajili ya kuiwezesha Tanzania kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi wengi katika Gridi ya Taifa na uimarishaji wa taasisi zinazohusika na na sekta ya nishati.

    Mambo ambayo Serikali ya Marekani iliitaka Tanzania kumaliza haraka ni suala mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar pamoja na kupata ufafanuzi wa watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni, wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

    Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue jana alisema suala hilo haliisumbui serikali na ni tatizo dogo  ambalo linatatuliwa.

    Alisema serikali ina uhakika wa kumaliza masuala hayo kabla ya kikao hicho cha Bodi ya MCC kukaa ambao masuala hayo yatakuwa yameshatatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.

    Alisema Bodi ya MCC ilikaa kikao chake cha kwanza Septemba, mwaka huu na inatarajia kukaa tena kikao chake Desemba, mwaka huu.

    Alisema serikali ina uhakika Bodi ya MCC ikikaa kikao cha  Desemba, mwaka huu itapitisha pasipo na shaka yoyote.

    Aliongeza kuwa suala la sheria ya makosa mtandaoni, kuna watu walikamatwa na watafikishwa mahakamani ambapo mahakama yenyewe ndiyo itakayotoa hukumu na kama wana makosa watahukumiwa na kama hawatakutwa na makosa basi wataachiwa huru.

    Balozi Sefue alisema suala hilo ni la kisheria, watu wametuhumiwa na wamepelekwa mahakamani ambako itaamua.

    Kuhusu mgogoro wa Zanzibar, Balozi Sefue alisema kuna vikao vinavyoendelea vya kupata muafaka na mgogoro huo nao utamalizwa kwa haraka zaidi.

    Marekeni ilieleza kuwa mambo hayo iliyotaka ipatiwe ufumbuzi, yataiwezesha MCC kuipima Tanzania katika sifa za kupata fedha hizo.
    Credit; Mpekuzi blog

    Njia 10 Zinazotumika Kukwepa Kodi Bandari ya Dar es Salaam

    By: Unknown On: 00:47
  • Share The Gag


  • Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha.

    Hata hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam.

    Mosi, ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’. 
     
    Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.

    “Tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa E-Payment ni mpya (umeanza Julai) na umefungwa kwenye benki moja tu iliyopo ndani ya eneo la Bandari… ule wa zamani unaendelea kutumiwa na wajanja hucheza na maandishi ya kujaza kwa mkono kuhujumu mapato ya serikali,” chanzo kimeeleza.

    Njia ya pili ya kuhujumu mapato bandarini hapo, imetajwa kuwa ni ya kushirikiana na maafisa wa benki. Hii ina uhusiano mkubwa na njia ya kwanza inayohusisha matumizi ya mfumo wa malipo wa zamani usiokuwa wa kielektroniki. 
     
    Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.

    “Huwa kuna ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa benki na mfanyabiashara husika. Baada ya kontena kutolewa bandarini, hamisho la fedha (transaction) huondolewa katika mfumo kwa maelezo kuwa halikuwa sahihi,” chanzo kimedai, huku kikisisitiza kuwa ushirikiano huo huhusisha pia watu wa Bandari na TRA ambao mwishowe hugawana malipo kadri wanavyokubaliana.

    Tatu, ni mwanya wa uvushaji wa makontena yenyewe yasiyolipiwa ushuru kupitia mageti maalum yanayofahamika kwa kazi hiyo, hasa geti Namba 3 ambalo chanzo kimedai ndilo linaongoza kupitisha mizigo ya ‘dili’.

    “Kwa ujumla yapo mageti matano ya kupitisha bidhaa mbalimbali, baadhi yakiwa ni ya kupitihia mafuta, nafaka na magari. 
     
    "Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.

    Njia ya nne ya kuhujumu kodi ya mapato ni ya kuwatumia watu wanaoendesha bandari kavu (ICD’s). Inaelezwa kuwa hivi sasa kuna bandari kavu 12, ambazo kila meli inapoingia hujulikana kila mzigo husika unapelekwa kwenye bandari ipi kati ya hizo. 
     
    Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.

    “Awali kwenye ICD’s kulikuwa na askari wa mmiliki wa ICD’s na siyo wa TPA… huyu alikuwa akiangalia malipo ya bosi wake tu ambayo ni gharama za kuhifadhi mzigo na hivyo TPA na TRA huambulia patupu,” chanzi kimeeleza, kikiongeza kuwa hivi sasa walau kuna nafuu kwani kwenye ICD’s kuna walinzi wa TPA lakini hilo limefanyika baada ya watu kuwa tayari wameshaiba sana.

    Njia ya tano inayotumiwa kukwepa kodi ni ya kubadili taarifa, hasa kupitia watu wenye wajibu wa kufanya tathmini. Kwamba, badala ya mzigo kukadirwaa kodi kwa kiwango sahihi, wahusika ambao zaidi huwa ni watu wa TRA hukadiria fedha kidogo baada ya kujihakikishia kuwa nao wanapewa mgawo na wafanyabiashara.

    “Hapo utakuta kontena la kodi ya milioni 80, mteja anaambiwa alipe milioni 40 tu … na wakati mwingine kiasi hicho pia hakiandikwi balki huandikwa cha chini zaidi kama milioni 5 tu…hii ni njia nyingine inayoligharimu taifa mabilioni ya fedha,” chanzo kimeeleza.

    Njia ya sita inayofanikisha ukwepaji kodi ni mtandao mpana wa baadhi ya vigogo wa maeneo mbalimbali Bandarini na TRA, ambao hawa huhakikisha kuwa wanakuwa na timu ya vijana wao wa kazi karibu katika kila eneo ili kufanikisha mipango yao.

    “Hii ndiyo njia kubwa ya hujuma. Kama utakumbuka aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisambaratisha baadhi ya mitandao kwa kuwagusa vigogo 27…  ile ilikuwa kuvunja mtandao uliokuwapo. Hilo lilisaidia kiasi, lakini sasa ipo pia mitandao mingine ambayo uchunguzi ukifanyika utabaini kuwa mambo yameanza kurudi kama zamani,” imeelezwa.

    Njia ya saba ya ukwepaji kodi ni kwa baadhi ya vigogo wa Bandari na TRA kuanzisha kampuni zao za uondoaji mizigo bandarini. Inaelezwa kuwa hizi hutumiwa sana kufanikisha ‘dili’ za ukwepaji kodi na ndiyo maana haishangazi kusikia kuwa kuna makontena zaidi ya 300 hayaonekani kwenye kumbukumbu za TRA.

    Njia ya nane ya ukwepaji kodi ni kuonyesha kuwa kontena linapelekwa nje ya nchi, kwa mfano Malawi, wakati ukweli ni kwamba huishia hapahapa nchini.

    “Utakuta kontena linadaiwa kupelekwa Malawi, lakini linachukuliwa na gari kukuu linaloonekana wazi kuwa haliwezi kufika hata Kibaha… njia hii pia hutumiwa sana kuikosesha serikali mapato,” chanzo kingine kilisema

    Njia ya tisa ya ukwepaji kodi  ni ucheleweshaji wa makusudi wa utoaji makontena. Kwamba, mteja anapotaka kutoa mzigo wake kwa kufuata njia halali zilizopo, huishia kuzungushwa kila uchao ili akubali kutoa rushwa na mwishowe kulipishwa kiwango pungufu cha kodi au kulipa fedha zisizoingia kabisa kwenye mikono ya TRA.

    Njia ya kumi ni ubabaishaji unaofanyika katika kuorodhesha idadi ya makontena inayotolewa bandarini kwenda kwenye bandari kavu. Hapa, kama makontena yanayotolewa ni 12, basi huandikwa kuwa ni 10 na mengine mawili huishia kuondolewa bila ya kuwa na kumbukumbu zake kwa ajili ya kulipiwa kodi.

    Pamoja na kuwapo kwa njia zote hizo, chanzo kimedai kuwa sababu kubwa ya kufanikiwa kwa ukwepaji kodi ni mtandao mpana unaoundwa na vigogo mbalimbali na ndiyo maana taarifa mbalimbali za wakaguzi wa ndani na wa nje katika Bandari ya Dar es Salaam huishia kubaki kwenye makabrasha bila ya kuwapo kwa utekelezaji wowote wa vitendo juu ya yale yanayopendekezwa na wataalamu.

    Chanzo: Nipashe
    Credit; Mpekuzi blog

    Saturday, 28 November 2015

    Papa Francis kumfufua Nyerere

    By: Unknown On: 02:00
  • Share The Gag
  • *Mama Maria Nyerere atangulia Uganda
    NA MWANDISHI WETU
    ZIARA ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis nchini Uganda imetajwa kuwa itafufua mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu.
    Kwa mujibu wa mtandao wa ETN wa nchini Uganda, ziara hiyo ya kitume ya Papa Francis itamfikisha katika eneo la Namugongo ambalo mashahidi wa imani ya dini ya Kikristu walichomwa moto.
    Ni katika eneo hilo la Namugongo ambako Hayati Nyerere alitangazwa kuwa Mwenyeheri huku mchakato wa kumtangaza mtakatifu ukiwa ulianza miaka tisa iliyopita.
    Namugongo ndiko ambako pia waumini wa dini ya Kikristu wa Afrika Mashariki na sehemu nyingine duniani hufika kuhiji.
    Taarifa ya ETN imeeleza kuwa ziara ya Papa Francis Namugongo itasaidia kufufua mchakato uliodumu kwa miaka tisa sasa wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa mtakatifu.
    Tayari mjane wa Hayati Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere yuko nchini Uganda ambako amekwenda kujumuika na waumini wengine wa dini ya Kikristu kumpokea na kushiriki ibada itakayoongozwa na Papa Francis.
    ETN imemkariri Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akisema kuwa mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu umetokana na mchango wake wa kuhimiza heshima na usawa kwa binadamu ambao aliutoa wakati akiwa kiongozi.
    Kwa mujibu wa ETN, Rais Museveni amesifu mchango wa Hayati Mwalimu Nyerere ambao haukuwa tu wa kuunganisha Watanzania bali alifanya kazi kwa kujali utu wa Waafrika.
    “Hayati Julius Nyerere alikuwa mwanaharakati wa Afrika ambaye alimpenda Mungu na alijali utu, aliwaunganisha Watanzania wa dini zote na alisaidia ukombozi wa mataifa mengine ya Afrika kama vile Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini na Uganda,” alisema Museveni.
    Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu hilo, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, alisema mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu unaendelea vizuri.
    Alisema suala la kuendesha mchakato huo ni jukumu la Tanzania na si Uganda hivyo jina la Hayati Mwalimu Nyerere linaweza kuibuka katika ziara ya Papa nchini Uganda kwa kutajwa tu, kwa sababu Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, amekuwa na mazingira ya karibu na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere.
    “Jukumu la kuendesha mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa Mtakatifu ni letu na linaendelea vizuri. Kuna mambo mengi ya kuchunguzwa mpaka mtu kutangazwa kuwa mtakatifu, inawezekana Papa akamzungumzia Mwalimu kwa sababu ya Rais Museveni mara kwa mara ameonyesha kuguswa na mwenendo wa mchakato huo,” alisema Askofu Kilaini.
    Papa Francis aliwasili nchini Uganda jana jioni saa 4:50 na kulakiwa na Rais Museveni na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo.
    Kwa mujibu wa ziara yake nchini humo iliyotolewa na Kanisa Katoliki la Uganda leo anatarajiwa kufanya ziara ya kitume katika miji ya Munyonyo, Nikiyanja, Nalukolongo, Namugongo, Kalolo na Rubaga na kesho atamaliza ziara yake nchini humo na kusafiri kwenda nchini Afrika ya Kati (CAR).
    Taarifa kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa ulinzi umeimarishwa na Serikali imeandaa wahudumu wa afya 400 na magari 38 ya kubebea wagonjwa ambayo yamepelekwa maeneo yote ambayo Papa atayatembelea.
    Papa Francis atakuwa Papa wa tatu kutembelea taifa hilo ambapo mwaka 1969, Papa Paul VI alitembelea nchi hiyo akifuatiwa na Papa Paul II mwaka 1993.
    Kampeni za urais zasimama
    Katika hatua nyingine wagombea urais wa vyama vyote wamelazimika kuahirisha mikutano yao ya kampeni kwa ajili ya kupisha ziara ya Papa Francis nchini humo.
    Rais Museveni ambaye anawania urais kwa muhula mwingine, aliwaambia wafuasi wa chama chake kuwa atamuomba Papa asaidie kutangaza utalii wa taifa hilo.
    Akemea ukabila na rushwa nchini Kenya
    Awali kabla hajaondoka nchini Kenya, Papa Francis alihutubia maelfu ya vijana katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambapo aliwahimiza vijana wa taifa hilo wasijihusishe na ukabila.
    Alisema vijana wanaweza kuchangia katika kukabiliana na changamoto za ukabila ambazo zimekuwa zikikwamisha maendeleo ya mataifa ya Afrika.
    Aliwashauri viongozi wa Serikali kuhakikisha vijana wanapata elimu na ajira kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kuwazuia kujiingiza katika makundi yenye itikadi kali za kigaidi.
    Kabla ya kuhutubia vijana katika Uwanja wa Kasarani, Papa Francis, alitembelea Mtaa wa Kangemi ambako wanaishi watu masikini na kukemea dhuluma ya huduma bora ambazo wanatakiwa wapatiwe masikini.
    “Ninafahamu kuhusu tatizo kubwa linalosababishwa na wawekezaji wasio na sura ambao hujitwalia ardhi na hata kujaribu kunyakua viwanja vya kuchezea watoto wenu shuleni. Hili ndilo hufanyika tunaposahau kwamba Mungu aliwapa watu wote ardhi waitumie kwa maisha yao bila kutenga au kupendelea yeyote,” alisema Papa Francis.

    Created by Gazeti la Mtanzania.

    Ukawa kumuaga Mawazo kwa saa tano

    By: Unknown On: 01:58
  • Share The Gag
  • * Wapigwa marufuku kula, kunywa wakati wa kuaga *Lowassa, Mbowe na Sumaye kuongoza waombolezaji

    NA BENJAMIN MASESE, MWANZA
    HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela imetoa saa tano kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutumia Uwanja wa Furahisha kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
    Akitoa ratiba mpya ya kuaga mwili wa Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Geita mjini hapa jana, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu, alisema shughuli  hiyo itafanyika katika uwanja huo na kuhudhuriwa na wabunge wa vyama vinavyoundwa Ukawa na watajitahidi kuzingatia maelekezo hayo ili watoe heshima zote zinazostahili.
    Pia alisema shughuli hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
    “Kiongozi mkuu atakayeongoza shughuli za kuaga mwili wa Mawazo atakuwa Mbowe, lakini katika shughuli hiyo kutakuwa na viongozi wa kitaifa ambao ni aliyekuwa mgombea nafasi ya urais kupitia Chadema, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, wabunge wa Ukawa na watu wengine maarufu.
    “Sasa kutokana na kupewa saa tano za kutumia uwanja huo, tutakuwa na makundi maalumu ya watu katika kupewa nafasi ya kuzungumza ili kuwawakilisha wengine, tunaomba wananchi watakaohudhuria pale waepuka kula chakula ovyo au kunywa, isije ikatokea mmoja akatapika, kuugua  tumbo wakasingizia mkusanyiko wetu.
    “Tambueni tulikuwa tumepewa saa tatu, ikabidi tuzungumze na Mkurugenzi wa Ilemela, John Wanga, ili kuongeza muda, natumia nafasi hii kuwataarifu Watanzania kwa ujumla kuwa Mawazo ataagwa kwa awamu nne, tunaaga hapa Mwanza kama kitaifa, kisha Geita Mjini sehemu ya mkoa  aliokuwa akiongoza.
    “Pia tutaaga Katoro kama sehemu ya Jimbo la Busanda alilogombea ubunge na mwisho atazikwa kijijini kwao Chikobe  Jumatatu ya Novemba 30, mwaka huu, ambapo wananchi wa pale watapewa nafasi ya kumuaga,” alisema Mwalimu.
    Kwa mujibu wa ratiba aliyoisoma, inaonyesha mwili wa Mawazo utaondolewa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza leo kati ya saa 2:30 – 3:00 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwa Mchungaji Charles Lugiko, ambaye ni baba yake mdogo eneo la Nyagezi-Sweya na utaagwa kwa taratibu za mila na desturi.
    Pia ratiba hiyo iliyonyesha kuwa kati ya saa tano asubuhi hadi saa sita mchana, mwili wa Mawazo utakuwa njiani kuelekea Uwanja wa Furahisha kwa ajili ya kuagwa kitaifa na inakadiriwa kufanyika kuanzia saa 6:30 hadi saa 8:00 mchana kabla ya kuanza safari ya kwenda Geita Mjini na waombolezaji watalazimika kulala hapo.
    Ratiba hiyo inaendelea kuonyesha kuwa kesho asubuhi mwili wa Mawazo utaagwa tena Geita Mjini katika Uwanja wa Magereza, kabla ya kusafirishwa hadi Katoro ambako utaagwa tena kama sehemu ya jimbo lake na baadaye kuupeleka kijijini kwao Chikobe na mazishi keshokutwa asubuhi.
    Katika hatua nyingine, Mwalimu alitoa shukrani kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, kupokea hukumu bila kinyongo na kuahidi kutoa ushirikiano katika ulinzi wakati wa shughuli za kuaga na kusafirisha mwili huo.
    Alisema tayari baadhi ya viongozi wa Chadema wametangulia mkoani Geita kwa ajili ya kuonana na polisi ili kupanga namna ya kufanikisha shughuli hiyo.
    Mawazo aliuawa Novemba 14, mwaka huu mkoani Geita na watu wasiojulikana baada ya kumvamia akiwa njiani na kumkata kwa mapanga na shoka na kusababisha kifo chake.
    Created by Gazeti la Mwananchi.

    Kutimiza agizo la Rais: Maelekezo ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kwa Balozi zote

    By: Unknown On: 01:53
  • Share The Gag

  • Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

    Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

    Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

    Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

    Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

    Imetolewa na:
    Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

    Credit; Mpekuzi blog

    Watu 3 wauawa katika shambulio Colorado

    By: Unknown On: 01:51
  • Share The Gag
  • Mshambuliaji akamatwa Colorado
    Watu 3 wameuawa baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi katika eneo la Colorado Springs nchini Marekani.
    Mtu mmoja aliyeshukiwa kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi ametiwa mbaroni.
    Kituo hicho kinasimamiwa na shirika la kitaifa la afya la Planned Parenthood ambalo limekuwa likilaumiwa na baadhi ya watu kwa kutoa mimba.
    Risasi za kwanza zilisikika mapema asubuhi na kuendelea kwa saa tano polisi wakifyatuliana risasi na mtu huyo.
    Maafisa wa polisi wanaimarisha usalama katika eneo la tukio Wakati huo wote taasisi za kukabiliana na hali ya dharura zilikuwa karibu kukiwa na ambulansi ambazo zilikuwa zimesubiri katika theluji iliyotanda eneo hilo.
    Polisi walifyatuliana risasi na mtu huyo walipokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wamekwama katika jengo hilo.
    Wengine wao walikuwa na majeraha.
    Afisa wa polisi wa kutoa usalama katika Chuo Kikuu, Garrett Swasey, mwenye umri wa miaka 44, alikuwa miongoni mwa waliouawa asubuhi.
    Afisa wa polisi Alifariki na raia wengine wawili.
    Alikuwa na mke na watoto wawili.
    Watu wengine tisa, kukiwemo maafisa wengine watano wa polisi walipelekwa hospitalini na inasemekana kuwa hali yao inaendelea kuimarika.
    Baadaye mwanamume mmoja alijisalimisha na kutiwa mbaroni na kuelekezwa kwenye kituo cha polisi.
    Shambulio la kliniki Colarado Shirika linalosimamia kliniki hiyo ya kupanga uzazi, Planned Parenthood, limekuwa likishutumiwa na baadhi ya makundi yanauyopinga uavyaji mimba kama njia ya kupanga uzazi.
    Hata hivyo kufikia sasa lengo hasa la shambulio hilo halijulikani.

    Credit by BBC Swahili.

    Wazazi wapongeza kasi ya Magufuli

    By: Unknown On: 01:48
  • Share The Gag
  • Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdalla Bulembo.

    RAIS John Magufuli amepongezwa kwa kasi ya utendaji kazi wake sambamba na maelekezo kadhaa ambayo amekwisha yatoa katika muda mfupi aliokuwa madarakani. Pongezi hizo zilitolewa jana na Jumuiya ya Wazazi CCM ambao amepongeza hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa na Rais Magufuli katika kipindi cha wiki tatu toka kuapishwa kwake ambapo jumuiya hiyo imesema ni imani yao kuwa nchi imepata kiongozi shupavu mwenye kusimamia kauli zake.
    Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema kuwa Jumuiya ya Wazazi inapongeza maelekezo mbalimbali ambayo yametolewa na Rais Magufuli ambayo yanajenga msingi bora wa mafanikio.
    “Chama kimepata kiongozi bora lakini pia nchi imepata Rais bora na hili linaendelea kujidhihirisha katika mambo ambayo yameanza kufanywa na Rais wetu na pia katika maelekezo yake kwa viongozi wa chini, sisi umoja wa wazazi tunapongeza sana kwa hayo,” alisema Bulembo.
    Bulembo alisema amefanikiwa kuwa karibu na Rais Magufuli katika kipindi chote cha kampeni kitu ambacho amekiona ni kuwa Rais ni mtu anayesimamia wakati wote na kauli zake.
    “Muda tuliokuwa na Rais katika kipindi cha kampeni tumejifunza kitu kwake, huyu ni mtu ambaye akisema jambo ndilo hilo hilo na analisimamia watu wasiwe na hofu naye hana nguvu ya soda,” alisema Bulembo.
    Baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na Rais Magufuli ni pamoja na kufanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa maelekezo ya kuboresha huduma katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kufanyiwa matengenezo kwa kipimo cha MRI, ziara ya ghafla Wizara ya Fedha, kufutwa kwa sherehe za Uhuru Desemba 9 mwaka huu na pia Siku ya Ukimwi, Desemba Mosi.

    Created by gazeti la Habarileo.


    Zitto Kabwe 'Akaabwa Koo' Zanzibar......Apewa Siku 14 za Kuomba Radhi Kwa Kumhusisha Dr. Shein na Makosa ya Uhaini

    By: Unknown On: 01:40
  • Share The Gag



  • Mbunge wa Kigoma Mjini  kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo,  Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini.

    Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu.

    Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar  na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio.

    Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani  yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. 
     
    "Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14  na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka." alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.

    Katika sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya uhaini Rais wa Zanzibar.

    Alisema iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga kauli ya Zitto.

    Khatib alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba.

    "Kumdhalilisha Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba," alisema Khatib
     
    Viongozi hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar  kwani walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya uhalifu wa uhaini.

    Katika mkutano wake na wandishi wa habari hivi karibuni, Zitto alisema kwa sasa Zanzibar haina serikali na mtu yoyote anayejiita rais wa Zanzibar  kikatiba amepindua nchi na katika hali ya kawaida anapaswa kushitakiwa kwa uhaini.
    Credit; Mpekuzi blog

    Kesi ya Ubunge wa David Kafulila Yaahirishwa Hadi Jumatatu Novemba 30 Baada ya Mlalamikiwa Kutofika Mahakamani

    By: Unknown On: 01:38
  • Share The Gag

  • Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, kupinga matokeo ya ubunge yaliyomtangaza mshindi Husna Mwilima, katika jimbo hilo, imeahirishwa hadi Novemba 30, mwaka huu.
     
    Kesi hiyo ipo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, John Utamwa.

    Jaji Utamwa alisema mlalamikiwa (Mwilima), katika madai hayo, hakupelekewa wito wa mahakama, hivyo anaamuru wito utolewe ili mlalamikaji aende mahakamani kujibu madai hayo ambayo anatetewa na mwanasheria wa serikali, Juma Masanja.

    Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Wakili wa mlalamikaji, Daniel Rumenyela, alidai mlalamikiwa (Mwilima), hakupatikana kwa ajili ya kuitwa shaurini hata akipigiwa simu hapokei.
     
    “Kutokana na mlalamikiwa wa kwanza kutopatikana, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inatoa siku tatu hadi Novemba 30, mwaka huu, (Jumatatu), ajibu madai hayo,” alisema Rumenyela. 
     
    Kesi hiyo namba 2 ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo, pia ina washtakiwa wengine ambao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza ambaye alikuwa Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

    Katika kesi hii ndogo ya awali kabla ya kesi ya msingi, Mahakama itaamua gharama ambazo Kafulila atatakiwa kulipa kama gharama za dhamana ambayo kisheria kwa washtakiwa watatu haizidi Sh. milioni 15.

    Katika kesi ya msingi, Kafulila anaomba Mahakama imtangaze mgombea aliyepata kura nyingi kwani aliyetangazwa siye mbunge halali kutokana na kupata kura chache.

    Katika shauri hilo, Kafulila alimtaja Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mrisho Gambo, kama wahusika waliofikisha ujumbe huo toka juu Oktoba 28, mwaka huu, saa 8:00 mchana kwa Msimamizi wa Uchaguzi kushinikiza matokeo batili kutangazwa.
    Credit; Mpekuzi blog

    Majipu Matano SUGU Anayotakiwa Kuyatumbua Rais Magufuli

    By: Unknown On: 01:35
  • Share The Gag

  • Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.

    Majipu (mambo matano) hayo ni;
    1.Kudhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
    2.Kukomesha rushwa na ufisadi.
    3.Kufumua mtandao wa majangili.
    4.Kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na 
    5.Kuua ‘mchwa’ unaoitafuna fedha za Serikali.

    Maoni yaliyotolewa na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida yanaonyesha kwamba kufanikiwa kwake kutategemea aina ya ushirikiano atakaoupata kutoka kwa wananchi na wanasiasa na hasa wa kutoka chama chake.

    Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elijah Kondi alisema Dk Magufuli anahitaji kupigana vita kali kufanikisha ahadi zake na akaonya kuwa hawezi kusimama mwenyewe na kushinda vita hiyo bila kuungwa mkono na wananchi hasa chama chake, CCM.

    “Vigogo wengi ndani ya chama chake wamekuwa wakihusishwa na majipu hayo. Hivyo, kufanikisha azma hiyo, kutategemea wingi wa wanaCCM watakaomuunga mkono, lakini kama watakuwa wachache, itakuwa vigumu. Hilo hata yeye (Magufuli) analifahamu ndiyo maana anasema vita hiyo ni kubwa,” alisema Kondi.

    Pia, alisema kushughulikia mtandao wa dawa za kulevya, ujangili na kuanzisha mahakama ya mafisadi kutategemea ushirikiano atakaoupata kutoka kwa watendaji na baraza lake la mawaziri.

    Kondi alisema kushindwa kwa Rais mstaafu Kikwete katika mambo hayo kulitokana na udhaifu wa baraza lake la mawaziri na watendaji wa taasisi za Serikali. 
     
    “Rais anaweza kuwa na dhamira njema, lakini je, atapata mawaziri wazuri wa kumsaidia? Hao mawaziri watakuwa na ari gani ya kushiriki vita hiyo?” alihoji na kuongeza:

    “Kwa sababu anaweza kuanzisha mahakama ya mafisadi lakini ikashindwa kuonyesha uhai kama anavyotarajia. 
     
    "Jaribio la kutumbua majipu hayo itategemea ushirikiano wa chama chake, mawaziri atakaowateua na watendaji wa Serikali.”

    Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema kilichosababisha marais waliomtangulia kushindwa kutumbua majipu hayo ni utofauti mkubwa ulioonekana kati yao.

    “Utofauti katika uwezo wao ukoje? Dhamira zao zinatofautianaje? Lakini hata kiwango cha utashi wa kushughulikia hilo jipu kinatofautianaje na uongozi uliopita. Ukisikiliza kauli ya Rais Magufuli anaonyesha matumaini,” alisema Mbunda.

    Meneja wa Soko la Machinga Complex, Nyamsukura Masondore alisema kupandishwa mahakamani kwa vigogo wa Serikali katika kashfa ya EPA ni sehemu ya juhudi zilizoonekana kwa uongozi uliopita.
     
     “Hivyo, hakuna kitakachoshindikana kwa Rais Magufuli endapo watendaji wa chini watakuwa tayari kubadilika na kutoa ushirikiano wa kushinda vita ya majipu hayo,” anasema

    Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema ana imani Rais Magufuli anaweza kushughulikia changamoto hizo sugu ambazo ameziita majipu kutokana na historia ya utendaji wake. 
     
    “Rais Magufuli atafanikiwa kazi hiyo kutokana na historia yake ya kutojihusisha kwa karibu na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na nje,” alisema.

    Profesa Shumbusho alisema kuwa endapo ataendelea na msimamo huo, changamoto ya ukwepaji kodi, misamaha ya kodi, biashara haramu ikiwamo ya dawa za kulevya zitakoma.

    Dawa za kulevya
    Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alinukuliwa Agosti 2013 bungeni akikiri kuwapo baadhi ya majina ya wabunge miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini alisema Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.

    Hata Kikwete wakati wa awamu yake ya kwanza, aliwahi kusema anawajua wauza dawa za kulevya lakini tatizo hilo limeendelea kuwa sugu hadi anamaliza kipindi chake cha pili.

    Mwaka huohuo, Umoja wa Mataifa (UN) ulitoa ripoti inayobainisha Tanzania kuwa kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki. 
     
    Kuanzia 2010 hadi 2013 ilipitisha tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine na ikitaja Bandari ya Tanga kuwa njia kuu ya upitishaji huo.

    Je, baada ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za Kulevya ya mwaka 2015, Rais Magufuli ataweza kusimamia mapambano dhidi ya vinara wa biashara hiyo?

    Ujangili wa tembo
    Kabla ya kuondoka madarakani, Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa Februari 2014 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) akikiri kuwatambua majangili 40 wa meno ya tembo na kwamba kiongozi wao anaishi Arusha. Pia, alikiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu.

    Vilevile, Mei 2014, ripoti iliyoitwa ‘Ivory’s Curse: The Militarization and Professionalization of Poaching in Africa’, ilieleza kuwa tangu mwaka 2000 wizara inayohusika na utalii ilikuwa imetawaliwa na kashfa za rushwa. Ripoti hiyo ilifafanua jinsi vikundi mbalimbali vya waasi barani Afrika vinavyoendesha shughuli za ujangili.

    Katiba ya Jaji Warioba
    Oktoba 2014, Bunge Maalumu la Katiba lilipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa tofauti ya kura mbili tu zilizonusuru kukwamisha Katiba hiyo kwa upande wa Zanzibar. Mvutano kati ya CCM na upinzani wakati wa upitishaji wa Katiba hiyo ulitokana na tofauti za itikadi na sera kuhusu muundo wa Muungano.

    Wajumbe wa CCM walipigania sera yao ya muungano wa Serikali mbili wakati wenzao wa wapinzani walipigania muundo uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba wa Serikali Tatu. Hadi sasa haijapigiwa kura ya maoni.

    ‘Mchwa’ Serikalini
    Kila mwaka, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa akikagua na kuibua ufisadi mkubwa katika Serikali Kuu, Idara za Serikali na mashirika ya umma. 
     
    Ripoti iliyotolewa mwaka huu inaonyesha ukaguzi ulifanyika katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109. 
     
    Kikwete amewahi kupangua baraza lake la mawaziri na kuwafukuza kazi watendaji lakini bado ufisadi umeendelea katika nyanja tofauti kama ulipaji mishahara hewa na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.

    Mahakama ya mafisadi
    Moja ya ahadi kubwa za Rais Magufuli wakati wa kampeni na Novemba 20 alipozindua Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano ni kuanzisha Mahakama Maalumu ya kushughulikia mafisadi.
     
     Tayari mchakato umeanza lakini wachambuzi wanasema kinachotakiwa ni kuipa meno Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili iweze kufanya kazi zake bila kuogopa mtu.
    Credit; Mpekuzi blog

    Tuesday, 24 November 2015

    Marekani kuwekea vikwazo wakuu wanne Burundi

    By: Unknown On: 02:16
  • Share The Gag
  • Machafuko yamekuwa yakiendelea Burundi tangu Aprili
    Marekani imesema itawawekea vikwazo maafisa wakuu wanne wa sasa na wa zamani Burundi kuhusiana na machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo.
    Wanne hao ni pamoja na waziri wa usalama wa umma na naibu mkuu wa polisi.
    Mali ya wanne hao itazuiwa na pia watanyimwa viza.
    Marekani inasema hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kusisitiza aongoze kwa muhula wa tatu imezidisha machafuko hayo ambayo yamesababisha kuuawa kwa watu zaidi ya 240 tangu Aprili.
    Visa vya mauaji vimeongezeka wiki za hivi karibuni na miili inapatikana mara kwa mara barabarani.
    Watakaowekewa vikwazo na Marekani ni:
    • Waziri wa usalama wa umma Alain Guillaume Bunyoni
    • Naibu mkuu wa polisi, Godefroid Bizimana
    • Mkuu wa zamani wa ujasusi Godefroid Niyombare
    • Waziri wa zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye
    Bw Niyombare na Ndayirukiye waliongoza jaribio la mapinduzi ya serikali Mei mwaka huu Rais Nkurunziza alipokuwa ziarani Tanzania.
    Ikulu ya White House imesema imepokea habari za kuaminika za visa vya watu kukamatwa, kuteswa na kuuawa na vikosi vya usalama pamoja na ukiukaji wa haki unaotekelezwa na magenge ya vijana wenye uhusiano na chama tawala.
    Aidha, wale wanaopinga serikali ya Nkurunziza wamekuwa wakitekeleza mashambulizi dhidi ya wafuasi wa serikali.
    Created by BBC Swahili.


    Mgogoro wa Zanzibar Watua IKULU ya Marekani

    By: Unknown On: 02:04
  • Share The Gag


  • Na Swahilivilla, Washington 
    Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).


    Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
     
    Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.

    Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.
     
    "Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwingine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.

    Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
     
    Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema;
     
    "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" 
     
    Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.

    Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.
     
    Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."
     
    Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao"

    Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.
     
    Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
     
    Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo. 

    Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.
    Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti nchini Marekani wakionyesha mabango yao
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.
    Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia
    Wapenda amani na Demokrasia wakiwa na mabango yao Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
    Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
    Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)
    Mpenda amani na Demokrasia Bwana Thuweni akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
    Mpenda amani na Demokrasia  Yussra Alkhary akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
    Credit; Mpekuzi blog

    Lowassa Awatembelea Wahanga Waliookolewa Mgodini Baada ya Kufukiwa Kifusi Kwa Siku 41

    By: Unknown On: 02:00
  • Share The Gag

  • Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa Jana alitoa shilingi milioni mbili kwa wahanga waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

    Akikabidhi fedha hizo kwa wahanga hao, Lowassa alisema ametoa fedha hizo kama msaada ili ziwasaidie kwa matibabu kwa muda wote watakapokuwa hospitalini hapo, ambapo kila mmoja amepatiwa shilingi laki tano.

    Mmoja wa wahanga hao, Joseph Burule alisema kitendo cha Lowassa kuwatembelea hospitalini hapo kimewapa faraja kubwa, kwani tangu waokolewe na kuanza kupatiwa matibabu hakuna kiongozi mkubwa aliyefika kuwajulia hali pamoja na kuwapa pole.

    Burule alisema kitendo hicho kinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi pindi linapotokea jambo la kusikitisha kama hilo, na kusema kuwa fedha hizo zitawasaidia kujikimu hospitalini hapo.

    Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA Salome Makamba aliwaambia wananchi waliojitoza kumsabahi Lowassa kuwa, Lowassa amekuja kuwapa pole wahanga hao na hakuja kwa masuala ya kisiasa.

    Novemba 15, 2015 wahanga 5 kati ya 6 waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya nyangalata wilayani kahama waliokolewa wakiwa hai baada ya kukaa ndani ya mashimo kwa siku 41, ambapo juzi mmoja kati yao alifariki dunia.

    Ni hivi karibuni baada ya kuokolewa mmoja wa wahanga hao alikaririwa akimuulizia Lowassa kama alishinda urais wa  Tanzania kwenye uchaguzi na baada ya kuambiwa hakushinda alikosa raha.
    Credit; Mpekuzi blog