Thursday, 30 June 2016

Mahakamani Kisutu: Watatu Mikononi Mwa Polisi Kwa Kubeba Mabango ya Kumkashifu Mtukufu Rais Magufuli

By: Unknown On: 22:53
  • Share The Gag

  • Jana wafuasi wa UKAWA walitiwa mbaroni baada ya kutoke mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkashifu Mtukufu Mkuu sana, Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

    Baadhi ya Mabango yalikuwa yanasomeka...

    Dikteta uchwara utashindwa
    Dikteta uchwara nenda Burundi

    Maoni Yangu;
    Kuna msemo usemao Delegatus Non Potest Delegare wakimaanisha la kujitakia halina majuto. Hawa wafuasi naona wamejitakia au wametumwa na viongozi wao uchwara kubeba mabango ya kashfa kwa Rais. Mbowe alikuwepo mahakamani, kwanini yeye hakubeba bango la kashfa? Kwanini awatumie wafuasi wachache wasiojielewa?

    Hivi nalo hili mtalalamika kuonewa?
    Kwanini hamuheshimu Taasisi ya Urais?
    Kwanini hamuheshimu Rais?

    Mnataka nini hasa wana wa upinzani?

    Crrdit; UDAKU SPECIAL

    Jeshi la Polisi Lapewa Siku 90 Kuhakikisha Mitambo ya LUGUMI Inafanya Kazi Vituo Vyote

    By: Unknown On: 22:51
  • Share The Gag

  • Jana akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

    Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

    Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

    Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.



    Credit;UDAKU SPECIAL 

    Shilole Kutafuta Mume Kijijini

    By: Unknown On: 22:48
  • Share The Gag

  • MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amejutia kuwapenda wanaume wa mjini kuwa ni wavivu kila sekta hivyo anajipanga kwenda kijijini kwao Igunga,Tabora kutafuta mume.

    Akistorisha na Showbiz Xtra, Shilole alisema kuwa, hataki tena kujichosha akili kwa wanaume wa mjini kwa vile ni wavivu bora aende Igunga kumpata mwanaume atakayeweza kufanya kazi kutokana na vyakula asili anavyokula.

    “Wanaume wa mjini wamezoea chipsi mayai, hawawezi chochote bora wa kijijini wanakula dona na wana akili za kufikiria,” alisema Shilole.

    Shilole alikuwa akitoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda.

    Credit;UDAKU SPECIAL

    Ungereza na mikataba mipya kibiashara

    By: Unknown On: 22:46
  • Share The Gag
  • Uingereza inaweza kuanza majadiliano ya mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu itakuwa imejitoa kabisa katika umoja huo.
    Kamishina wa biashara wa umoja wa ulaya Cecilia Malmström amesema Uingereza inaweza kuanza majadiliano ya mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu itakuwa imejitoa kabisa katika umoja huo.
    Katika mahojiano na BBC amesema kuna aina mbili za majadiliano ya utekelezaji wa makubaliano hayo.
    "Uhusiano kati yetu na uingereza kwa siku zijazo hautajadiliwa chini ya kifungu cha 50,ambacho ndicho kigezo cha kujitoa.
    Hivyo kuna aina mbili tu za majadiliano,moja unajitoa,kisha unajadiliana namna mpya ya uhusiano,au vyovyote inavyokuwa"
    Bi.Malmstrom ameongeza kuwa mpaka mikataba hiyo isainiwe ndipo biashara inaweza kufanyika chini ya taasisi ya kimataifa ya kibiashara.

    Chanzo BBC.

    Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika

    By: Unknown On: 22:23
  • Share The Gag
  • MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hatimaye wametaja mfanyabiashara ambaye alibainishwa na Rais John Magufuli katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Ikulu Dar es Salaam juzi.

    Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alimtaja mfanyabiashara huyo kuwa ni Mohammed Mustafa Yusuf Ali anayetuhumiwa kuiibia Serikali matrilioni ya shilingi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) ambazo hazijasajiliwa na TRA na kutoa risiti bandia.

    Alisema TRA kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi ili kubaini makampuni yote yanayojihusisha na udanganyifu huu, ambapo hadi sasa jumla ya makampuni manne yamebainika kujihusisha na ukwepaji kodi kwa mtindo huu kuanzia mwaka 2010 hadi 2014; na jumla ya Sh 29,216,900,301.7 imebainika kutokulipwa serikalini na makampuni hayo kwa kipindi hicho.

    Alisema kwa sasa wanaendelea na mahojiano naye zaidi ili kuwabaini wote wanaohusika na mfumo huo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

    Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA, Alfayo Kidata aliyeambatana na Mlowola katika mkutano huo wa waandishi wa habari, makampuni hayo yamekuwa yakinunua risiti za manunuzi bandia kutoka kwa watu wanaomiliki mashine za EFDs ambazo hazijasajiliwa.

    “Makampuni hayo wakishanunua risiti za manunuzi bandia, hatimaye huzitumia risiti hizo kudai marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) bila kuwepo na bidhaa au huduma halisi iliyouzwa au kutolewa na mhusika, kitendo ambacho kinainyima serikali mapato stahiki kwa mujibu wa sheria,” alisema.

    Aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Skol Building Material Ltd ambayo tangu mwaka 2012 hadi 2013 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,464,915,963 na Kodi ya Mapato yenye thamani ya Sh 10,960,787,861 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 16,425,703,824 kwa kipindi hicho.

    Kampuni nyingine ni Farm Plant (T) Limited ambayo tangu mwaka 2010 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 5,930,170,573 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 4,948,393,516 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 10,878,564,089.

    Pia imo kampuni ya A.M.Steel & Iron Mills Limited ambayo kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa jumla ya VAT ya Sh 79,016,112 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 131,693,518 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 210,709,630.

    Kampuni nyingine ni A.M Trailer Manufacturers Limited ambayo tangu mwaka 2013 hadi 2014 haikulipa VAT ya Sh 638,221,034.80 na kodi ya mapato yenye thamani ya Sh 1,063,701,724. 00 ambayo jumla ya kodi inayodaiwa ni Sh 1,701,922,758.00.

    Alisema baada ya kubaini ukwepaji kodi huo kwa kushirikiana na TAKUKURU inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na mara baada ya uchunguzi kukamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukwepa kodi.

    Alitoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutojihusisha na kununua risiti za bandia na kudai marejesho ya VAT yasiyostahili kwa kuwa mamlaka imejizatiti kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

    Aidha alisema uchunguzi wa awali pia umebaini kuwepo makampuni hewa 228 na kusisitiza kwamba wameusimamisha mfumo huo bandia na kutoa siku tatu kwa kampuni zote zinazodaiwa kulipa fedha hizo.

    “Hakuna yeyote anayekwepa kodi atasalimika, wote ni lazima walipe na sasa tumedhibiti mfumo huo bandia,” alisema.

    Juzi Magufuli akizungumza na Ma RC na Ma DC wapya, aliwataka wakasimamie vyema mapato katika maeneo yao kwani kumekuwepo na baadhi ya watu wajanja wanaotumia vibaya taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brela) TRA kujinufaisha wenyewe na kuliingizia taifa hasara.

    Alisema: “Tulikuwa tunafuatilia mashine za EFDs zinazokusanya mapato, yupo mtu mmoja alitengeneza kampuni nyingi zilizokuwa zikimlipa asilimia tano ya VAT na yeye anacheza na TRA halipi asilimia 18 ya kodi hiyo. Alikuwa anaingiza kati ya shilingi milioni saba mpaka nane kwa dakika. Serikali ilipoteza matrilioni ya fedha. Huyu mtu yupo kwenye mikono salama kwa sasa”.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Auawa kwa Fimbo

    By: Unknown On: 22:12
  • Share The Gag
  • ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 212 kilichopo Milambo mkoani Tabora, ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wafugaji akiwa eneo lake la ujenzi.

    Aliyeuawa katika tukio hilo la juzi katika kijiji cha Usule kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora ni Crius Mkumozi mwenye umri wa miaka 35.

    Mtuhumiwa wa mauaji hayo inadaiwa alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la askari huyo.

    Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema askari huyo alipigwa fimbo kichwani na begani baada ya kujaribu kuondoa ng’ombe waliokuwa kwenye eneo lake.

    Kamanda alisema mtuhumiwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Serikali Yamtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Achukue Hatua Stahiki Dhidi ya Aliyemtukana Rais Magufuli

    By: Unknown On: 21:29
  • Share The Gag
  • SERIKALI imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchukua hatua stahiki katika shauri la kesi ya jinai namba 100 ya Jamhuri dhidi ya Isaac Emily aliyeadhibiwa kulipa faini kwa kumtukana Rais John Magufuli mtandaoni.

    Hayo yamesemwa jana bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo ulioombwa na wabunge wa CCM, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba na Livingstone Lusinde wa Mtera, baada ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni. Hata hivyo, hatua stahiki hizo hazikuelezwa.

    Alisema nia ya maagizo hayo kwa DPP ni kulinda dhana na dhamira ya adhabu katika mfumo wa haki jinai ambayo hutaka mhukumiwa kujutia kosa lake na wengine kujifunza kutoka kwake.

    Katika maelezo yake, Waziri Mwakyembe alisema kwa hali ilivyo katika shauri hilo, dhana na dhamira ya adhabu haikuweza kufikiwa kwa mwenendo wa kuingiza siasa katika utekelezaji wa hukumu.

    Alisema serikali imejiridhisha na kilichotokea katika shauri hilo na kauli za wabunge walioomba mwongozo kwamba masharti ya adhabu yalikuwa mepesi mno usiolingana na shauri lenyewe.

    Alisema aliyehukumiwa analifanyia siasa suala hilo na kuigeuza adhabu rafiki aliyopewa kuwa burudani ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.

    “Mheshimiwa spika, nimejiridhisha na kilichotokea. Madhara ya mwelekeo huu mpya katika haki jinai, ni kuchochea vitendo zaidi vya ukaidi kwa mamlaka za nchi na hivyo kujenga msingi wa vurugu. Hili halikubaliki katika utawala wa sheria. Mdharau mwiba mguu huota tende,” alisema..

    Alisema kosa kama hilo lilitokea Kenya mwaka jana ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, Alan Okengo (25) alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya dola 2,000 (Sh milioni 3.2) kwa kumtukana rais wa nchi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

    Alisema pamoja na umri wake na uwezo wake mdogo wa kulipa faini, adhabu ilibaki palepale ili mkosaji ajutie kosa lake asije akarudia na jamii ijisikie salama.

    Alisema pamoja na kutokuingilia mhimili wa mahakama na taratibu zake kitendo cha kuwapo kwa adhabu ambayo haijutiwi inakiuka dhana na dhamira ya adhabu.

    Alisema kwa shauri la Emily, pamoja na kutiwa hatiani wakili wake aliomba mtuhumiwa alipe faini kwa kuwa hakusumbua mahakama na pia ni kosa lake la kwanza na ana familia.

    Alisema wakati hakimu anamuuliza wakili wa serikali aliiachia mahakama kutoa maamuzi ambayo ilimpatia wakili wa utetezi maombi yake.

    Mwakyembe alisema pamoja na maagizo ya serikali kwa DPP amewakumbusha waendesha mashitaka nchini kuwa macho na waweke mbele weledi na maslahi mapana ya taifa na kamwe wasiyumbishwe na mihemko ya kisiasa katika jamii.
     
    Credit; Mpekuzi Blog 

    Nigeria,China zasaini Mkataba wa Mafuta

    By: Unknown On: 21:25
  • Share The Gag
  • Uchumi wa Nigeria unatishiwa na matukio ya mauaji yanayotekelezwa na Boko Haram
    Nigeria imetia saini mkataba wa mafuta na nchi ya China wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 80. Kampuni ya mafuta nchini humo imesema kuwa kiasi cha fedha kitatumika kuimarisha viwanda vya ndani.
    Licha ya kuwa miongoni kwa nchi za Afrika zinazozalisha mafuta kwa kiasi kikubwa,Nigeria inaingiza kiasi kikubwa cha mafuta kutoka nje kutokana na viwanda vyake vingi kutufanya kazi.
    Nchi hiyo pia inakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo ikiwemo Boko Haram wanaotaka kupata sehemu kubwa ya utajiri wa mafuta.

    Chanzo BBC.

    Rais wa zamani matatani Argentina

    By: Unknown On: 21:19
  • Share The Gag
  • Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi
    Polisi nchini Argentina wanasaka mali za Rais wa zamani wa nchi hiyo Cristina Fernandez de Kirchner.
    Upekuzi unafanyika katika jimbo la kusini la Santa Cruz,kwa amri ya mahakama.
    Fernandez anadaiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini humo.
    Hii ni kwa mara ya pili familia ya Rais huyo wa zamani kuvamiwa kwa sababu hiyo.
    Mwaka jana Hoteli pamoja na baadhi ya majengo yalifanyiwa upelelezi mkali na wana usalama wa nchi hiyo.
    Fernandez anamtuhumu Rais wa sasa Mauricio Macri kuwa anafanya mchezo mchafu wa kisiasa juu yake.

    Chanzo BBC.

    Misikiti na makanisa yafungwa Lagos

    By: Unknown On: 21:19
  • Share The Gag

  • Mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria umefunga makanisa 60 na misikiti 20 katika jitihada za kupunguza kelele.
    Karibu hoteli kumi na klabu kadha nazo zilifungwa
    Mji wa Lagos una karibu watu milioni 10 huku, honi za magari, maombi kutoka misikitini na nyimbo makanisani vikitawala mji huo.
    Mwezi Agosti utawala ulifunga maeneo 22 baada ya wenyeji kulalamika kutokana na kele zilzokuwa zikitoka maeneo hayo.

    Chanzo BBC.

    Waziri Mkuu: Serikali Itatoa Waraka Juu Ya Ukusanyaji Mapato Kupitia Mawakala

    By: Unknown On: 21:18
  • Share The Gag
  • WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.

    Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

    Alisema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. 
    “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.

    Alisema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

    Alisema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

    “Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.

    Alisema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

    “Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.

    Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.

    Alisema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

    “Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.

    Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.

    IMETOLEWA NA:
    OFISI YA WAZIRI MKUU,
    S.L. P. 980,
    DODOMA.
    ALHAMISI, JUNI 30, 2016


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

    Mlipuko wa bomu wawaua watu 18 Somalia

    By: Unknown On: 05:25
  • Share The Gag
  • Mlipuko wa bomu Somalia
    Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
    Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.
    Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
    Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi lililokuwa karibu.
    Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.

    Chanzo BBC.

    Wednesday, 29 June 2016

    By: Unknown On: 01:12
  • Share The Gag
  • Sijui nianzaje ila dunia imeisha, Zamaradi anamuhoji shoga anaitwa Kaoge, Pamoja ni ngumu kuaangalia ila kunafunzo la kujifunza kwa kinji watoto wetu wa kiume tunavoweza kuwalea watoto wetu. 
     Mashoga wanaongezeka kwa kua waaribifu ni wengi na wengi ni watu wazito. Shoga anatamani kuzaa anataka kupandikiza na yupo kwenye harakati za kubeba mimba 
     Alikua anaitwa mwanamke tangu mdogo na baba yake na mitaani alikua anaitwa gody ka demu, Kiukweli wanaume tusifumbie macho ili swala malezi ya karibu zaidi tangu utoto ndio tunaweza kupiga vita USHOGA. Na si matusi kipigo na unyanyapaaji
    By: Unknown On: 01:12
  • Share The Gag
  • Sijui nianzaje ila dunia imeisha, Zamaradi anamuhoji shoga anaitwa Kaoge, Pamoja ni ngumu kuaangalia ila kunafunzo la kujifunza kwa kinji watoto wetu wa kiume tunavoweza kuwalea watoto wetu. 
     Mashoga wanaongezeka kwa kua waaribifu ni wengi na wengi ni watu wazito. Shoga anatamani kuzaa anataka kupandikiza na yupo kwenye harakati za kubeba mimba 
     Alikua anaitwa mwanamke tangu mdogo na baba yake na mitaani alikua anaitwa gody ka demu, Kiukweli wanaume tusifumbie macho ili swala malezi ya karibu zaidi tangu utoto ndio tunaweza 
     
    Credit; UDAKU SPECIAL  vita USHOGA. Na si matusi kipigo na unyanyapaaji

    England yapata kocha wa muda

    By: Unknown On: 01:08
  • Share The Gag
  • Gareth Southgate,kocha wa muda wa England
    Chama cha soka nchini England kinajiandaa kumtangaza Gareth Southgate kuwa kocha wa muda wa timu yake ya taifa katika mwanzo wa kampeni za kuwania kufuzu kombe ka dunia.
    Zoezi la kumsaka kocha mpya litaanza baada ya michezo ya awali ya kufuzu kufanyika.
    Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzuluMtendaji mkuu wa FA Martin Glenn,amesema kuwa kupatikana kwa kocha mpya kunaweza kuchukua miezi kadhaa,huku pia akimtaja meneja wa Arsenal,Arsene Wenger ambaye anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake kama moja ya chaguo lao.
    Roy Hodgson alijiuzulu baada ya kushindwa na Iceland katika mchuano wa Euro Roy Hodgson alijiuzulu baada ya kukifundisha kikosi cha England kwa miaka mitatu kufuatia kichapo dhidi ya timu ndogo ya Iceland mjini Nice siku ya Jumatatu.

    Chanzo BBC.

    Muhimbili Kuna Kitengo cha Kuhudumia Mashoga..Shoga Maarufu Afunguka Kupitia Take One ya Zamaradi

    By: Unknown On: 01:05
  • Share The Gag

  • Hii nimeisikia jana kupitia kijana mmoja shoga aliyekuwa akihojiwa katika kipindi kimoja kwenye tv. Alijiweka bayana sana na hakuficha jambo, kitu kilichonistaajabisha kwa uwazi wake. Hata changudoa si rahisi kujianika kiasi kile.

    Akasema Muhimbili wana kitengo chao cha kuhudumiwa. Kwamba hupewa mafuta ya ky, kondom, sabuni, hasa za kusafishia kinywa baada ya blow job, n.k. Hiki kitengo mbona kipo katika taasisi nyeti kiasi hiki? Serikali waliridhia vipi kuweko kwa kitengo hiki pale? Ni nani wafadhili?

    Mbona huwa hatusikii kikitangazwa kama vitengo vingine vya waathirika wa ukimwi na madawa ya kulevya? Kwa huu unyeti wake na aina ya huduma wanazotoa hapo ni wazi kwamba ushoga si jambo jema kabisa. Kwamba ushoga ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine tajwa hapo juu.

    Lakini kinachonishangaza kuhusu huu ugonjwa wa ushoga, mbona wanawapa vitendea kazi kama mafuta na kondom kuliko kuwaelimisha waache ushoga?

    Kingine nilichobaini ni kuwa ushoga huooooo umeanza kuchomoza hadharani na kwa staili yake. Baada ya miaka mitano tutauona ushoga ni jambo la kawaida nchini kama hali ikiachwa hivi.

    Nimalizie tu kwa kumnukuu huyo shoga aliposema, mboga saba... ya nane pilipili. Yaani mtoto wa kiume asidekezwe sana na wazazi kwani kufanya hivyo kutamuingiza katika majanga kama vile ushoga. Hiyo ni tafsiri yangu

    Credit;UDAKU SPECIAL

    TAKURURU Waendelea Kuchunguza Waliopokea Pesa za ESCROW..Mkurugenzi Asema Wasizani Wapo Salama

    By: Unknown On: 01:04
  • Share The Gag

  • Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema watu waliopokea mgawo wa fedha zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, hawako salama kwani anaendelea kuchunguza nyaraka.

    Amesema uchunguzi wa sakata hilo la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo unahitaji umakini mkubwa, ukikamilika wote watakaobainika watachukuliwa hatua.

     Mawaziri wawili (Profesa Sospeter Muhongo na Profesa Anna Tibaijuka), waliwajibika kutokana na sakata hilo, viongozi wa kamati za Bunge (Andrew Chenge, William Ngeleja na Victor Mwambalaswa) kuvuliwa madaraka, wanasiasa kufikishwa mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi na watumishi wengine kufikishwa mahakamani.

    Chenge na Profesa Tibaijuka waliwajibishwa kutokana na kuonekana wameingiziwa Sh1.6 bilioni kila mmoja kwenye akaunti zao, Ngeleja (Sh40.4 milioni), wakati Mwambalaswa aliwajibika kutokana na mgongano wa kimaslahi.





    Credit; UDAKU SPECIAL

    Tuesday, 28 June 2016

    Taarifa ya Lugumi Yapigwa Kalenda Tena Bungeni

    By: Unknown On: 22:07
  • Share The Gag

  • Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.

    Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.

    Sakata hilo linahusisha utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.

    Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.

    Baada ya sakata hilo kuibuliwa, wabunge walitaka liwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea mjini Dodoma, lakini PAC ikaunda kamati ndogo ambayo sasa inatakiwa iwasilishe ripoti ya uchunguzi wake.

    Hadi jana asubuhi ripoti ya kamati hiyo ndogo, iliyoundwa na wajumbe tisa, ilikuwa bado haijawasilisha ripoti yao.

    Hata hivyo, Aeshi ambaye pia ni mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), alisema alitarajia kukabidhiwa ripoti hiyo na kamati ndogo jana na baada ya hapo kazi ya uchambuzi wa kamati nzima itaanza.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    Kujitoa EU: Uingereza Yawatoa hofu Watanzania

    By: Unknown On: 21:57
  • Share The Gag
  • Siku chache baada ya Uingereza kuamua kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), Balozi wa nchi hiyo nchini amesema wataendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania ili kuhakikisha uwekezaji haupungui.

    Akijibu swali kuhusu athari zozote zitakazojitokeza kwa Tanzania baada ya Uingereza kujitoa EU, Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alisema jana kuwa haitapunguza uwekezaji, misaada wala vita dhidi ya rushwa na uhalifu wa kimtandao.

    “Uhusiano wetu utaendelea kuwa imara kama ulivyokuwa awali,” alisema Melrose.

    Balozi Melrose alisisitiza kuwa Uingereza itaendelea kuwa mwanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato), Umoja wa nchi saba zilizoendelea zaidi duniani (G7), umoja wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani (G20) na Jumuiya ya Madola na kushirikiana na Tanzania.

    Tangu Juni 23 Uingereza ilipopiga kura ya maoni kujitoa EU, umetokea mtikisiko mkubwa kati ya England na washirika wake Wales, Scotland na Ireland Kaskazini.

    Kura hiyo ya maoni imesababisha Waziri Mkuu, David Cameron kutangaza kujiuzulu kwa kushindwa kwake kushawishi nchi hiyo kubaki EU.

    Mtikisiko mwingine mkubwa umejitokeza katika masoko ya hisa ambapo tangu Alhamisi iliyopita yameporomoka na kupoteza Dola za Marekani trilioni mbili.

    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa alisema soko lake na mengine Uingereza ni miongoni mwa nchi nne zenye mchango mkubwa wa kifedha kwa EU.

    Takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka jana pekee ilichangia Pauni 12.9 bilioni (zaidi Sh37.5 trilioni).

    Kiasi hicho ni kikubwa kwa Sh10 trilioni ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka ujao wa fedha, 2016/2017.

    “DSE haijaunganishwa sana na masoko ya nje lakini tunao wawekezaji wengi kutoka Uingereza,” alisema Moremi na kubainisha kuwa, mabadiliko yanaweza yakaonekana Soko la Hisa la Johanessburg (JSE), Afrika Kusini.

    Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Viwanda na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda kwamba Serikali imejipanga vipi kukabiliana na athari zitakazojitokeza baada ya Uingereza kujitoa alisema ni mapema sana kwa wizara yake na Tanzania kwa ujumla kutetereka kwa namna yoyote kwa sasa kwa kuwa uhusiano mkubwa uliopo ni ule wa kiuwekezaji.

    “Uwekezaji siyo suala la siku moja,” alisema na kufafanua kuwa mikataba ambayo ilishatiwa saini ni lazima itekelezwe kama makubaliano yalivyofanywa. “Masoko ya hisa ndiyo yanayoweza kuathirika kwa muda huu mfupi,” aliongeza.

    Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Kamote alisema muda huo wa utekelezaji wa maadhimio ya kujitoa ni mrefu na huenda hatua za haraka zikachukuliwa kabla athari za kiuchumi hazijasambaa duniani kote.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Hifadhi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tz

    By: Unknown On: 21:55
  • Share The Gag
  • Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania
    Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
    Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
    Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
    Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
    Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
    Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
    Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika. Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
    Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
    ''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

    Chanzo BBC.

    CCM Yawalima Barua Wabunge Wake.....Sasa Watakiwa Kujieleza Kamati Kuu

    By: Unknown On: 21:49
  • Share The Gag

  • Kamati Kuu ya CCM imeagiza Kamati ya Wabunge wa chama hicho kuwapa barua za kujieleza wabunge wao wasiohudhuria, wanaochelewa na wanaondoka kabla ya vikao vya Bunge kuahirishwa. 
    Tayari maagizo hayo yamefanyiwa kazi na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jasson Rweikiza ambaye amewalima barua wabunge hao. 

    Katika barua yenye kichwa cha habari “Maagizo ya Kamati Kuu ya CCM” aliyopewa mmoja wa wabunge wa CCM inaonyesha wametakiwa kujieleza kwa nini siku nyingine walifika wamechelewa na mara kadhaa walitoka mapema kabla kuahirishwa kwa Bunge. 
    “Mwenendo huu ni kukiuka kanuni za Kamati ya Wabunge wote wa CCM hasa kanuni ya 41. Tafadhali andika maelezo kwa nini Kamati Kuu isichukue hatua? Maelezo yanifikie  kabla ya Juni 25 mwaka huu,” ilisema sehemu ya barua ya mmoja wa wabunge walioandikiwa. 
    Alipoulizwa Rweikiza kuhusiana na barua hiyo alisema haitambui na kwamba imeghushiwa. 

    “Kanuni zipo zinazoongoza vikao vya Bunge, zipo pia zinazoongoza wabunge wa CCM. 

    "Wakitaka kuondoa wabunge wa CCM wanazijua sana, isipokuwa hatujafikia hatua ya kufundishana kwa kuanza kuandikiana barua,”alisema. 
    “Wanajua mbunge hawezi kuondoka bila kwenda kwa Spika na kuomba ruhusa au kujulisha kwenye chama kwamba anatoka, wanajua,” alisema Rweikiza na kusisitiza kwamba hata taarifa zinazoonyesha kuna wabunge wanaotakiwa kujieleza kwake ni majungu tu. 
    Japokuwa Rweikiza ameikana barua hiyo, wabunge kadhaa wa CCM walioomba majina yao yasitajwe wamekiri kwamba barua hizo zimetolewa na kwamba wanabanwa kwa kutakiwa kujisajili mara mbili; kitabu cha Bunge na cha CCM. 
    Katika ukurasa wake wa Facebook uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema wabunge wa CCM wanalalamikia kulazimishwa kuingia bungeni kwa kuwa Bunge halina ladha. 
    Pia, Msigwa alisema wabunge hao wa CCM wanadai Naibu Spika Dk Tulia Ackson hafuati kanuni na taratibu na kwamba wametakiwa kujieleza Kamati Kuu ya CCM. 
    Aidha, baadhi ya wabunge wa CCM walionekana kukerwa na utaratibu wa kujisajili sehemu mbili yaani Bunge na CCM mara mbili kwa siku. 
    “Kuna haja gani ya kutia dole (kusaini kwa utaratibu wa kieletroniki) halafu tena tuje tusaini kwenye makaratasi ya CCM?,” alihoji mmoja wa  wabunge. 
    Alisema ili kusaini karatasi hizo inawapasa wabunge kwenda upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani ambapo wabunge waliokabidhiwa kazi ya kuzitunza karatasi hizo hukaa kama kambi mbadala baada ya wabunge wa upinzani kususia vikao vinavyoendeshwa na Dk Tulia.
    “Wengine tunaheshima zetu hatuwezi kwenda upande wa upinzani kufuata makaratasi ya kusaini. Kwanza Bunge lenyewe halina mvuto unakuja hapa watu wawili ndio wanapewa nafasi ya kuchangia mjadala na baada ya hapo wanapitisha,” alisema. 
    Mbunge mwingine wa CCM alisema haoni haja ya kuwepo ndani ya Bunge kwa sababu hawapewi nafasi ya kutosha ya majadiliano na hivyo bora kutokuwepo ndani ya ukumbi muda wote. 
    “Mimi saa hizi naingia ndani ya ukumbi wa Bunge nasaini natoka naenda zangu kantini (ya Bunge) kuangalia mpira maana hata nikikaa ndani sitopata nafasi ya kuchangia,” alisema mbunge huyo. 
    Alisema haoni haja ya kusaini mara mbili kwa sababu CCM wanaweza kutumia usajili wa Bunge kufahamu wabunge waliopo na wasiohudhuria kwa wakati wanaouhitaji. 

    Alisema orodha hiyo haina mashiko kwa sababu wanazo namba za wabunge wote kama kuna jambo ambalo wanahitaji basi wanaweza kuwataarifu. 
    “Hata mimi nimepewa barua ya kujieleza lakini si kwamba ni mtoro bali tunakuwa na majukumu mengine ya kibunge nje ya Bunge,” alisema. 
    Hatua hiyo inakuja wakati wabunge 118 wa vyama vinavyounda Ukawa, wakiwa wamesusia vikao vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ya kuongoza vikao kibabe na kutofuata kanuni. 
    Hii ni wiki ya nne tangu Dk Tulia aanze kuendesha vikao vya Bunge peke yake bila kupokewa na wenyekiti wa Bunge kama ilivyokuwa kabla hajatofautiana na kambi rasmi ya upinzani


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Ajali ya basi yaua watano

    By: Unknown On: 21:48
  • Share The Gag

  • Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi

    WATU watano wamekufa baada ya basi aina ya Super Sami, mali ya Kampuni ya Super Sami lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza, kugonga jiwe na kupinduka katika barabara ya Mwanza-Shinyanga eneo la Mabuki wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
    Basi hilo lenye namba za usajili T499 BCB, likiendeshwa na dereva William Elias maarufu kama Massa (44) ambaye ni mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, lilipata ajali hiyo saa saba usiku wa kuamkia jana.
    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema baada ya kugonga jiwe dereva alishindwa kulimudu na kupinduka na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo dereva, msaidizi wake na majeruhi 13.
    Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva aliyekuwa kwenye mwendokasi hali iliyosababisha basi hilo kugonga jiwe lililokuwa barabarani na kushindwa kumudu basi hilo lililoserereka na kupinduka.
    Aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Massa ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, Vaileth Odede (21) mkazi wa Mwanza, mwanamume mmoja na wanawake wawili wenye umri kati ya miaka 25-30 ambao hawajatambulika.
    “Majeruhi watano kati ya 13 wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu, na wengine wanane wanatibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi,” alisema Kamanda Msangi.
    Aliwataja majeruhi wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Misungwi kuwa ni Sophia Miraji (25), Kibilo Mwacha anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40, Boniphace Charles (38-40) na Frank Munyuni (30).
    Majeruhi wengine ni Stanley Zacharia (25), Sia Dauson (28), Hellen Luheke( 30-35), Michael Leonard (30-35), Kudra Ibrahim ambaye ni mtoto wa miaka miwili na miezi 10, Zamda Issa (24), Marietha Christopher (26), Elizabeth Simon (40) na Dickson Msamba (22).

    Chanzo HabariLeo.

    Watu 36 wauawa Uturuki

    By: Unknown On: 21:46
  • Share The Gag
  • Polisi wakiokoa wahanga 

    Watu 36 wauawa Uturuki

    • Dakika 37 zilizopita
    Watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa
    Image copyright
    Image caption Polisi wakiokoa wahanga
    Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea..

    Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.
    Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.
    Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo.
    Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
    Uturuki imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka pande mbili,kwanza kutoka kwa kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi jirani ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda dola yao.

    Chanzo BBC>


    Monday, 27 June 2016

    RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Sita

    By: Unknown On: 23:50
  • Share The Gag
  • Mtunzi:  Enea Faidy
     
    Ilipoishia sehemu ya  Tano ( kama hukuisoma bofya hapa).
    Eddy alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka kumwambia kitu muhimu....

    Endelea...
    Doreen alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy.. 

    Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi kuziteka hisia za Eddy haswa. Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
     
    "Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.
    "Naam"
    "niambie basi.."
    "ah!.. Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya chini ili majirani wasiweze kusikia.
    "Eddy! we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa Dorice.
    "Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "
    "Na Dorice je?"
    "habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"
    "mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.
    "Nikubalie Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.
    "Okey! nakubali kuwa na wewe!"
    "Oh my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani walikuwa darasani.
    "Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."
    "sharti gani tena?" Eddy alishtuka
    "upo tayari?"
    "ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"
    "good.. nafurahi sana"
    "Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.
    "usijali nitakuambia baadae..."
    Alisema Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara aliachia tabasamu.

    ==>Endelea Nayo  <<Kwa Kubofya Hapa>>


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Trafiki Aliyetukanwa na Mke wa Waziri Apandishwa Cheo

    By: Unknown On: 23:30
  • Share The Gag

  • Deogratius Mbango, askari wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki) ambaye hivi karibuni alitukanwa na mke wa waziri wa serikali ya awamu ya tano (jina kapuni), baada ya kulikamata gari lake kwa kuvunja sheria za barabarani, hatimaye amepandishwa cheo ikiwa ni maagizo ya Rais Dk. John Magufuli.

    Habari kutoka chanzo cha uhakika, zinasema kuwa askari huyo ambaye alilikamata gari la mke wa waziri huyo baada ya kuvuka sehemu ya waendao kwa miguu eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, amepandishwa hatua moja mbele, kutoka koplo hadi sajenti.

    Kitendo hicho cha kulikamata gari hilo, bila kujali utambulisho na matusi ya mwanamke aliyedai kuwa mke wa waziri, kilimfanya Rais Magufuli kumsifu na kumuona kuwa jasiri kazini kwake, hivyo kuliagiza jeshi la Polisi kumpa promosheni mara moja.

    Juzi Jumapili, Uwazi lilimkuta trafiki huyo akiongoza magari maeneo ya Makumbusho katika lango la kuingilia daladala akiwa na cheo kipya cha usajenti.

    Alipoulizwa kuhusu kuula huko, Mbango alikiri kutokea kwa jambo hilo na kumshukuru Mungu pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kumkumbuka, huku pia akilishukuru gazeti hili kwa kukumbushia katika toleo lake Na 993 lililoripoti juu ya kutotekelezwa kwa amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Credit; UDAKU SPECIAL

    Atakayempachika Mimba Mwanafunzi Kifungo cha Miaka 30 Jela

    By: Unknown On: 23:11
  • Share The Gag

  • BUNGE limepitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 ya mwaka 2016 ambayo pamoja na mambo mengine, imeongeza adhabu kwa watu wanaowapa mimba au kuoa ama kuolewa na mwanafunzi, sasa watafungwa jela miaka 30.

    Sheria hiyo ilipitishwa jana bungeni mjini Dodoma baada ya Muswada kuwasilishwa Juni 24, mwaka huu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambao baadhi ya wabunge walipata fursa ya kuuchangia.

    Muswada huo ulilenga kufanya marekebisho katika sheria 21 kwa lengo la kuondoa mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo na umepitishwa kuwa sheria.

    Sheria zilizopendekezwa kurekebishwa na sheria hiyo ni pamoja na ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu; Kudhibiti Usafirishaji Haramu wa Binadamu; Kanuni za Madai; Usajili wa Makandarasi; Elimu; Ajira na Mahusiano Kazini na Sheria ya Taasisi za Kazi.

    Muswada huo uliowasilishwa bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju unatamka adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela katika marekebisho ya Sheria ya Elimu kwa watakaompa mimba, kumuoa au kuolewa mwanafunzi.

    Awali adhabu iliyotamkwa katika sheria hiyo ya elimu ni mshitakiwa akibainika kuwa na kosa kutozwa faini ya Sh 500,000 na iwapo ni kosa la pili anatozwa faini ya Sh 500,000 au kifungo kisichozidi miaka mitatu.

    Akiizungumzia sheria hiyo inayosubiriwa kusainiwa na Rais John Magufuli, Masaju alisema inawalinda watoto wote chini ya miaka 18 walioko na wasio shuleni na kuwa kosa hilo likifanywa na mtoto atahukumiwa kwa mujibu wa sheria ya mtoto.

    Kifungu cha 60 A (i) kimeeleza kuwa itakuwa kinyume cha sheria katika mazingira yoyote yale kwa mtu yeyote kumuoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya sekondari au ya msingi na atakayekiuka atafungwa jela miaka 30.

    Katika Sheria ya Taasisi za Kazi inataka mwajiri anapokiuka masharti ya sheria ya kazi, ikiwa ni pamoja na kuchelewesha michango ya waajiriwa, kutoza faini na Ofisa wa Kazi ya papo kwa hapo isiyopungua Sh 100,000.

    Wakichangia muswada huo, wabunge wameonesha furaha yao juu ya Sheria ya Elimu inayohusu adhabu ya miaka 30 jela. Hata hivyo, pamoja na furaha hiyo, baadhi ya wabunge wametoa angalizo la kutaka kupimwa kwanza DNA kabla ya kutoa hukumu huku wengine wakitaka kuwapo kwa nyongeza ya viboko.

    Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu (CCM) alipongeza marekebisho hayo na kutaka adhabu ya miaka 30 iongezwe na kuchapwa viboko 12 kila mwezi mpaka aliyehukumiwa anamaliza kifungo kutokana na wahalifu hao kuwa na mazoea ya kuzoea gereza.

    Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgalu (CCM) alisema pamoja na serikali kuja na marekebisho hayo pia waangalie namna ya kukabiliana na utoro shuleni ili kuwafanya wanafunzi kupata elimu.

    Kwa upande wake, Mbunge wa Njombe Kusini, Edward Mwalongo (CCM) alitaka sheria imtake anayekutwa na kosa hilo kuacha fedha za fidia ambazo mama atazitumia wakati mwanaume akiwa jela.

    Akijibu hoja ya kutumika kwa vipimo vya vinasaba (DNA), Masaju alisema kwa sasa utaratibu wa vipimo hivyo utatumika mahakamani na waendesha mashitaka kuhakikisha hawaachi shaka kwenye ushahidi kutokana na Tanzania kutokuwa na uwezo wa kumpima DNA mtoto akiwa tumboni.

    Kuhusu Sheria ya Taasisi za Kazi, Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Chakoma (CCM), alitaka adhabu hiyo kuongezwa ili sheria kuleta tija na kutaka kazi ya kutoza faini hiyo isifanywe na Ofisa wa Kazi kama ilivyotamkwa katika sheria badala yake ifanywe na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA) kutokana na mifumo mizuri ya ufuatiliaji.

    Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alisema serikali imekuja na sheria hiyo ili kuwabana waajiri wanaochelewesha michango ya waajiriwa na kuwa katika kutekeleza sheria waziri ataweka makundi na kuwa kampuni zenye kipato kikubwa adhabu yao itakuwa kubwa zaidi.

    Credit; UDAKU SPECIAL