December
30 2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT
Wazalendo Zitto Kabwe alitoa taarifa kuhusu madeni anayodaiwa, kiwango
cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo benki, posho pamoja
na mali zote anazomiliki.
Kupitia
ukurasa wake wa facebook ametoa ufafanuzi akidai baadhi ya wabunge
wenzake hawajafurahishwa namna alivyoweka na hivyo ameeleza kuwa….
- Mshahara wa mbunge kwa mwezi ni tshs 4.6 milioni kabla ya kodi, baada ya kukatwa kodi ya mapato mbunge hubakia na tshs 3.2 milioni kwa mwezi. Hivyo Mshahara ni tshs 38.4 milioni kwa mwaka.
- Mbunge hulipwa pia tshs 8.2 milioni kila mwezi kama posho ya kazi za Ubunge (mafuta ya kutembelea Jimbo, matengenezo ya gari, malipo ya watumishi wa Ofisi ya Mbunge kama vile Dereva, mhudumu wa ofisi na Katibu wa Mbunge). Hii ndio inapelekea mapato ya jumla ya tshs 99 milioni kwa mwaka niliyoweka kwenye taarifa ya rasilimali na madeni.
- Mbunge pia hulipwa posho za kujikimu na posho za vikao ( kwa wale wanaochukua posho hizi). Hizi hutolewa kulingana na mahudhurio ya vikao.
Aidha
zitto ameongeza kuwa kuweka wazi tamko la mali na madeni kwa sasa sio
takwa la kisheria bali ni uamuzi binafsi wa Mbunge ama Kiongozi mwengine
wa umma.
"Mimi
ninatakiwa na katiba ya chama changu kuweka wazi tamko la mali na
madeni kwa mujibu wa azimio la Tabora linalohuisha azimio la Arusha.
" Hivyo, ichukuliwe kuwa kuweka kwangu wazi tamko husika ni kutekeleza
matakwa ya katiba ya chama ambacho Mimi ni mwanachama na sio kuwashtaki
wenzangu kwa wananchi. Mimi naamini kwamba uwazi ni moja ya silaha
madhubuti ya kupambana na ufisadi. Nimewasilisha muswada bungeni kutaka
uwazi huu liwe sharti la sheria za nchi yetu"- Zitto
Credit;Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment