Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema mabadiliko makubwa ya kisiasa
yanayotokea duniani katika kipindi hiki hayawezi kuzuiliwa na mifumo
iliyopo.
Akizungumza
jana na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mateves katika Halmashauri ya Arusha
Vijijini, Lowassa alisema nguvu kubwa ya mabadiliko inayoonyeshwa na
Chadema itawaletea wananchi maendeleo.
Lowassa
ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015, chama chake kilipata kura nyingi kwenye maeneo mengi
licha ya kutokuwa washindi na kwamba wamejipanga katika uchaguzi wowote
utakaofanyika kuhakikisha kinashinda kwa kishindo.
“Ninazindua
kampeni za uchaguzi huu mdogo nikiwa na imani kubwa kwa Chadema. Nina
imani kuwa mgombea wa chama hiki atatekeleza anayoyaahidi na kuondoa
kero zenu na ndiyo maana Chadema inaungwa mkono zaidi nchini,” alisema Lowassa.
Alisema
katika mpango wa kukiimarisha chama hicho, wajumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema wanazunguka nchi nzima kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.
Katika
harakati za kuhakikisha kwamba upinzani unaibuka na ushindi katika
chaguzi ndogo zote zilizopangwa kufanyika Januari 22, Lowassa alisema
leo atakuwa Zanzibar katika uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge wa
Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan na baada ya hapo
ataelekea Bukoba katika kampeni za Ukawa.
Uchaguzi
wa Kata ya Mateves unafanyika baada ya Mahakama kuagiza urudiwe
kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi ulipita ambao mgombea
wa CCM alitangazwa mshindi.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment