Saturday, 7 January 2017

Tagged Under:

Mwanamke wa Kitanzania Akamatwa na Mzigo wa Madawa ya Kulevya Tumboni

By: Unknown On: 23:19
  • Share The Gag


  • INDONESIA: Mwanamke Mtanzania akamatwa akiwa na Wanigeria wawili wakijaribu kuingiza mihadarati. Mnigeria mmoja ameuawa akijaribu kutoroka. Mtanzania huyo alikamatwa siku ya jumatano katika Jiji la Jakarta.

    Baada ya upekuzi Mtanzania huyo akutwa na gramu 138 za Crystal Methamphetamine, kete nyingine 66 za Crystal Methamphetamine alikuwa amezimeza na gramu 3 za bangi alizoficha kwenye nguo yake ya ndani.

    Wakati huo huo, polisi nchini Namibia wanadai kukamata watu 135 kati ya Novemba 1 na Disemba 2016 kwa tuhuma za dawa za kulevya aina ya Mandrax, Cocaine, Crack Cocaine, Heroin na Bangi. Kati ya waliokamatwa na dawa hizo wapo Watanzania watano.

    Credit; Udaku Special

    0 comments:

    Post a Comment