Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Chato mkoani
Geita, Shilinde Nicolaus (18) umeopolewa Ziwa Victoria baada ya kuzama
Januari 28 saa tisa alasiri alipokuwa akivua na wenzake.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema mwili huo
ulipatikana juzi baada ya jitihada za wavuvi wa eneo hilo kwa
kushirikiana na wananchi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Muungano lilipotokea tukio hilo,
Kapembe Charles alisema kijana huyo na wenzake ambao walinusurika,
walipata ajali hiyo baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba kisha
kuzama.
Charles alisema katika tukio hilo wenzake wawili, Daud Deus na Mgonyolo
Hamis wote wakazi wa Kijiji cha Kitela walinusurika baada ya kuogelea
hadi nchi kavu.
Mmoja wa wanafunzi hao, Daud Deus alisema wakati wakiendelea kuvua, kulikuwa na upepo mkali uliosababisha mtumbwi wao kuzama.
“Mimi na Hamis tulifanikiwa kuogelea kwenye majani yaliyoota ndani ya maji, kisha tukaokolewa na wavuvi,” alisema Deus.
Credit; Udaku
0 comments:
Post a Comment