Ule
wimbo unaosikika mtaani wa ‘pesa kupotea mifukoni’ haumhusu Bosi wa
WCB, Diamond Platinumz anayeendelea kuzihesabu ‘deals’ kubwa zaidi za
matukio ambayo dunia nzima inayaangalia kwa macho yote.
Siku
chache baada ya kutumbuiza kwa ustadi mkubwa kwenye tuzo za CAF jijini
Abuja nchini Nigeria, Diamond amealikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa
Kombe la Mataifa ya Africa 2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.
Chibu
Dangote amewapa habari hiyo njema mashabiki wake kupitia mitandao ya
twitter na Instagram, kwa kupost taarifa ya show yake hiyo iliyowekwa
kwenye akaunti maalum ya AFCON 2017.
“GABON!!!
You know we gat to make a World History on the 14th January right?? See
you this this Coming Weekend then…👈 #WcbWasafi” aliandika.
Ingawa
Tanzania haipo miongoni mwa nchi zinazoshiriki kombe hilo kubwa zaidi
la soka barani Afrika, mwaka huu bendera itapeperushwa kupitia tasnia ya
Muziki na kuiacha alama ya Tanzania kwenye mashindano hayo.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment