Monday, 9 January 2017

Tagged Under:

Arusha: Lema 'Aendelea Kuongoza' Akiwa Mahabusu

By: Unknown On: 21:06
  • Share The Gag

  • Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) ambaye yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo anaendelea kutenda na kumudu kazi zake akiwa mahabusu. Taarifa za kuaminika zinaonesha kuwa Lema huombwa mawazo, maelekezo na ushauri kabla ya kufanyika jambo lolote Arusha.

    Mambo yote yafanyikayo kwa kujadiliwa au kuamriwa na Baraza la Madiwani la Arusha ambalo linadhibitiwa na CHADEMA yanahusisha mawazo na melekezo ya Mbunge Lema. Taarifa zinaonesha kuwa Lema yu katika afya njema na mwenye ari kubwa ya kutenda kazi.

    Lema, Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Arusha Mjini aliyeweza kutetea kiti chake cha Ubunge, anahusishwa na kuhusika na kila jambo jimboni Arusha katika kulipanga, kulijadili na kuliamua. Lema anatajwa kuwa ni mmoja wa Wabunge machachari wa upinzani nchini.

    Yuko mahabusu baada ya kukosa dhamana katika mahakama huko Arusha katika kesi zake mbili za jinai. Bado Lema anapambania kupata dhamana huku akiendelea na kesi zake za jinai.

    Mwafaaaaaaa!

    Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

    Credit; Udaku Special

    0 comments:

    Post a Comment