Tuesday, 28 March 2017

Serikali Kutengeneza Mwongozo Wa Kuwarudisha Shule Waliopata Mimba

By: Unknown On: 08:08
  • Share The Gag
  • Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
    Serikali imejipanga kutengeneza mwongozo wa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba wakiwa masomoni ili kuhakikisha wanapata elimu hadi kufikia ngazi za juu.

    Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori alipokuwa akifungua warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia jinsia katika elimu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako.

    Manori amesema Serikali ya Tanzania inajitahidi kuzingatia jinsia katika utoaji wa elimu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari uwiano wake ni moja kwa moja japo kuwa idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba hivyo lengo la warsha hiyo ni kuwasaidia wadau kuweka mipango ya elimu inayozingatia usawa wa kijinsia.

    “Serikali yetu imejipanga kuhakikisha wasichana wanapata elimu hadi ngazi za juu lakini mpango huo unakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mimba na ndoa za utotoni hivyo ili kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ngazi za juu za elimu tuko kwenye mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya wanafunzi waliopata mimba wakiwa bado wanasoma kupata nafasi ya kuendelea na masomo,”alisema Manori.

    Mkurugenzi Msaidizi amezitaja changamoto zingine zinazowapelekea wanafunzi wa kike kuacha shule zikiwemo za umaskini, mazingira rafiki ya kusomea, mila na desturi zinazomkataza msichana kupata nafasi ya kusoma pamoja na kukosa muda wa kujisomea kwa sababu ya kufanya kazi nyingi wanaporudi majumbani.

    Manori ametoa rai kwa Watanzania kuelewa kuwa kila mtoto ana haki na wajibu wa kupata elimu bila kujali jinsia pia ameiasa jamii kuacha kuwaozesha wasichana wenye umri chini ya miaka 18 ili waweze kufikia malengo yao waliyojipangia.

    Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen ameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha mipango ya elimu nchini inaangalia usawa wa kijinsia kwa kuwa ni njia moja wapo itakayochochea maendeleo ya elimu kwa watoto wa kike.

    “Warsha hii imeandaliwa kwa ajili ya wadau wote kutoa mawazo yao juu ya changamoto za usawa wa kijinsia zinazoikumba sekta ya elimu pamoja na kuwapa fursa wadau hao kushauriana kuhusu mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto hizo ili kuinua sekta ya elimu sio tu kwa Tanzania bali kwa Afrika nzima,”alisema Haldorsen.

    Haldorsen ameongeza kuwa mfumo wa elimu umetambua uhusiano uliopo kati ya elimu na usawa wa kijinsia ndio maana wadau wa masuala ya elimu wa Serikali kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika wameamua kuungana kwa pamoja kujadili juu ya tathmini, mpangilio na ufuatiliaji wa elimu unayozingatia jinsia.

    Tanzania imekua nchi ya kwanza kuendesha warsha hiyo ya siku tatu iliyoshirikisha maafisa waandamizi wa Serikali wanaoshughulikia mipango ya elimu kutoka nchi za Mozambique, Zambia, Malawi, Uganda, Zanzibar na Tanzania Bara.

    Imeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI).


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Thursday, 23 March 2017

    VIDEO: Nape Akidhibitiwa na Polisi Arudi Ndani ya Gari Baada ya Mkutano wake Kupigwa Marufuku

    By: Unknown On: 10:59
  • Share The Gag
  • Mtazame hapo chini Mbunge Nape akiamriwa kurudi ndani ya gari mara tu alipofika katika Hoteli ya Protea kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.
    Rais Magufuli leo ametengua uteuzi wa Nape na Kumteua Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo.
     
    ==>Tazama video hapo chini
     
    Creted; Mpekuzi Blog 

    Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Bandarini Na Kuzuia Makontena 20 Yenye Mchanga Wa Madini Uliokuwa Usafirishwe Nje Ya Nchi

    By: Unknown On: 10:49
  • Share The Gag
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.

    Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.

    Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP - Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

    “Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

    Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.

    Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.

    Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.

    Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.

    Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.

    Gerson Msigwa
    Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
    Dar es Salaam

    23 Machi, 2017


    ==

    Creted; Mpekuzi Blog 

    Gwajima: Mimi ndo chanzo cha Nape Nnauye Kutumbuliwa na Rais

    By: Unknown On: 10:43
  • Share The Gag
  • Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya  kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.

    Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema    Mkuu wa Mkoa alivamia  ofisi za  Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.

    "Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.

    Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog

    VIDEO: Msanii Harmorapa Alivyotimua Mbio Baada ya Polisi Kutoa Bastola Kumdhibiti Nape Nnauye

    By: Unknown On: 10:40
  • Share The Gag
  • Leo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Nape Nnauye na nafasi yake amepewa Dr. Mwakyembe.
    Baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na waandishi wa habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.

    Saa chache baadae Nape Nnauye alifika eneo hilo lakini alizuiwa na askari huku wakimrudisha ndani ya gari.
    Katika sakata hilo, Askari mmoja aliamua kutoa bastola na kuielekeza kwa Nape. Msanii Harmorapa alikuwepo jirani na Nape wakati tukio hilo likitokea...
    ==>Mshuhudie hapo chini alivyotimua mbio baada ya bastola kutolewa
    Creted Mpekuzi Blog