Askofu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni
sababu kubwa ya kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na
Michezo Nape Nnauye.
Akizungumza
leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha
Efm,Gwajima amesema Mkuu wa Mkoa alivamia ofisi za Clouds kwa lengo
la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume
iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.
"Labda
niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha
kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia
Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.
Gwajima
alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi
huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu
yanayoikumba tasnia ya habari.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment