JESHI
la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo
vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na sifa.
Kauli
hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa
Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama
cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es
Salaam jana.
"Kuanzia
sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva
kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali
na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.
Mpinga
alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E
2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo
zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na
kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa
na madereva.
Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havina sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.
Mwenyekiti
wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya
Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya
changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na
usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za
watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya
serikali pekee.
Mkolla
alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili
kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe
zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.
Credit Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment