Wapiga kura nchini Thailand wameidhinisha katiba mpya ambayo itaruhusu jeshi kuendelea kuongoza taifa ilo.
Kampeni zote za kupinga uamuzi huo zikiwa zimezuiliwa na serikali ya kijeshi pasipo kutoa ufafanuzi wa kutosha.
Matokeo
ya kura zilizopigwa yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wapiga
kura wanaunga mkono mabadiliko ya katiba. Huku asilimia hiyohiyo ndiyo
itakayohusika kumchagua waziri mkuu.
Nchi ya Thailand inaongozwa kijeshi baada ya kufanya
mapinduzi miaka miwili iliyopita. Jeshi linaamini kuwa katiba mpya
itaimarisha nchi hiyo kufuatia misukosuko ya kisiasa iliodumu kwa
takribani miaka kumi.
Chanzo BBC
Sunday, 7 August 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment