SERIKALI
wilaya ya Nzega mkoani Tabora imepiga marufuku wabunge na madiwani wa
vyama vyote, kutofanya mikutano ya hadhara nje ya maeneo yao
waliyochaguliwa.
Imechukua hatua hiyo ili kuepusha uchochezi wa kisiasa, ambao unaweza kujitokeza na kuhatarisha amani.
Mkuu
wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla amesema viongozi hao wanapaswa
kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao ya uchaguzi.
Amesema
mbunge ama diwani, haruhusiwi kufanya mikutano nje ya eneo lake na
endapo atabainika, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu, ikiwa ni pamoja
na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Amesema
serikali imetoa agizo hilo ili wananchi waweze kupata taarifa za
maendeleo na sikuendelea kutoa lugha za kukashifu viongozi wa serikali.
Ngupulla
aliongeza kuwa serikali haijakataza mikutano ya siasa, bali viongozi
hao wanapaswa kufanya siasa safi katika maeneo yao na si kutoka nje ya
maeneo yao, kwani wanaweza kuhatarisha amani ya nchi.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment