Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump
amebadilisha mwelekeo wa kampeni zake na kujikita kwenye masuala ya
uchumi baada ya wiki ngumu ya kuanza kampeni za uchaguzi.Trump akiwa
mjini Detroit ameahidi kuibua uchumi wa Marekani kwa mwendo wa kasi kwa
kufuta kodi za mashirika endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo
mwezi Novemba.
Amesema nafasi nyingi za kazi zitatengenezwa kwa mabadiliko hayo ya
mfumo wa kodi sanjari na makubaliano mapya ya mkataba wa kibiashara wa
kanda ya Marekani ya Kaskazini.
Trump amesema kupunguza kodi ndio itakuwa kitovu cha
mipango yake ya kuhuisha uchumi wa Marekani, iwapo atashinda katika
uchaguzi wa Novemba.
Katika hotuba yake kubwa ya sera za uchumi
aliyoitoa mjini Detroit, huku akikatishwa mara kwa mara na kelele za
waandamanaji,Trump amesema kiwango cha kodi kwa wafanya kazi kitakuwa
kidogo mno hivyo kuzalishwa kwa mamilioni ya kazi. Amesema anataka
kufungua ukurasa mpya kwa uchumi wa Marekani.
Nae mgombea urais
kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton akihutubia mkutano mjini
Florida, amekosoa mikakati ya bwana Trump na kusema katu haitasaidia
idadi kubwa ya wamarekani, lakini inasaidia watu ambao tayari wap juu.
Wakati huo huo, msuguano mkali umeendelea baina ya
Maafisa hao akiwemo mkurugenzi wa zamani wa CIA na mawaziri wawili wa
mambo ya ndani, wametoa taarifa inayo mtuhumu Trump kwa kukosa uwezo,
haiba na uzoefu wa kuhudumu kama rais wa Marekani. Wamebashiri kuwa
huenda akawa Rais asiye na uwezo kwenye historia ya Marekani tangu taifa
hilo kuanzishwa.
Katika kujibu mapigo Trump amesema watu hao ni
miongoni mwa watawala wa Washington ambao wanapaswa kulaumiwa kwa
kuifanya dunia kuwa sehemu hatari ya kuishi.
Trump anajitahidi
kurudi kwenye ushindani baada ya wiki ambayo iliishia kumpa mpinzani
wake wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, uongozi wa wazi kwenye
kura za maoni.
Chanzo BBC.
Monday, 8 August 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment