KAMPUNI ya Money- Gram inayotoa huduma za kutuma pesa duniani na
kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania zimetangaza kwamba sasa wateja wa
Vodacom wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M-Pesa
kutoka nje.
Kwa sasa, kuna watumiaji wa huduma ya M-Pesa zaidi ya milioni saba
nchini Tanzania ambao hufanya miamala ya zaidi ya trilioni mbili kila
mwezi. Ushirikiano huo mpya utawawezesha Watanzania wanaoishi nje ya
nchi kutuma fedha moja kwa moja kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini ambao
ni wateja wa M-Pesa kwa njia rahisi, inayofaa, salama na haraka zaidi.
Hatua hiyo itafungua uwezekano wa kukuza utumaji pesa kuja Tanzania,
ambao kwa sasa ni umefikia dola za Marekani bilioni 1.2. Uzinduzi huo
ulifanyika wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam, ambapo pia ulihudhuriwa na Herve Chomel, Makamu wa Rais wa
MoneyGram Upande wa Mauzo Kanda ya Afrika na Jacques Voogt, Ofisa Mkuu
wa wa Idara ya biashara ya huduma za M-Pesa wa Vodacom Tanzania.
“Kampuni ya MoneyGram inafurahi sana kufanyakazi na Vodacom katika
kutoa huduma ya haraka, uhakika na salama kwa mamilioni ya wateja
watakaotuma na kupokea pesa,”
Imeandikwa na Mwandishi Wetu
Imechapishwa: 26 Agosti 2015
Thursday, 27 August 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment