Monday, 8 August 2016

Wahamiaji 21 wazikwa Libya

By: Unknown On: 21:20
  • Share The Gag
  • Wahamiaji 21 waliozama wameripotiwa kuzikwa na wakazi wa mji wa Libya baada ya miili yao kukutwa ikielea ufukweni.
    Mamlaka nchini humo zinasema zililazimika kuchukua hatua ya kuondoa maiti zilizokuwa zinazagaa.
    Bahari ya Mediterranea inayotumika na wahamiaji kwenda ng'ambo Miili hiyo ilikaa siku tatu katika pwani ya Al- Maya, kaskazini mwa Tripoli .
    Mohammed Garbaj amekuwa akijaribu kuwaokoa wahamiaji wanaozama Wenyeji wa eneo hilo walijawa na hofu ya maiti hizo kusababisha magonjwa ndipo wakalazimika kuzizika.

    Chanzo BBC.

    Trump ajikita kuboresha uchumi wa Marekani

    By: Unknown On: 21:09
  • Share The Gag
  • Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump amebadilisha mwelekeo wa kampeni zake na kujikita kwenye masuala ya uchumi baada ya wiki ngumu ya kuanza kampeni za uchaguzi.Trump akiwa mjini Detroit ameahidi kuibua uchumi wa Marekani kwa mwendo wa kasi kwa kufuta kodi za mashirika endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi Novemba.
    Amesema nafasi nyingi za kazi zitatengenezwa kwa mabadiliko hayo ya mfumo wa kodi sanjari na makubaliano mapya ya mkataba wa kibiashara wa kanda ya Marekani ya Kaskazini.
    Trump amesema kupunguza kodi ndio itakuwa kitovu cha mipango yake ya kuhuisha uchumi wa Marekani, iwapo atashinda katika uchaguzi wa Novemba.
    Katika hotuba yake kubwa ya sera za uchumi aliyoitoa mjini Detroit, huku akikatishwa mara kwa mara na kelele za waandamanaji,Trump amesema kiwango cha kodi kwa wafanya kazi kitakuwa kidogo mno hivyo kuzalishwa kwa mamilioni ya kazi. Amesema anataka kufungua ukurasa mpya kwa uchumi wa Marekani.
    Nae mgombea urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton akihutubia mkutano mjini Florida, amekosoa mikakati ya bwana Trump na kusema katu haitasaidia idadi kubwa ya wamarekani, lakini inasaidia watu ambao tayari wap juu.
    Wakati huo huo, msuguano mkali umeendelea baina ya Maafisa hao akiwemo mkurugenzi wa zamani wa CIA na mawaziri wawili wa mambo ya ndani, wametoa taarifa inayo mtuhumu Trump kwa kukosa uwezo, haiba na uzoefu wa kuhudumu kama rais wa Marekani. Wamebashiri kuwa huenda akawa Rais asiye na uwezo kwenye historia ya Marekani tangu taifa hilo kuanzishwa.
    Trump na Clinton kwa pamoja wanakosoa ushirikiano wa kibiashara wa Pacific Katika kujibu mapigo Trump amesema watu hao ni miongoni mwa watawala wa Washington ambao wanapaswa kulaumiwa kwa kuifanya dunia kuwa sehemu hatari ya kuishi.
    Trump anajitahidi kurudi kwenye ushindani baada ya wiki ambayo iliishia kumpa mpinzani wake wa chama cha Democratic, Hillary Clinton, uongozi wa wazi kwenye kura za maoni.

    Chanzo BBC.

    Vyuo Vya Udereva Visivyo Na Sifa Mbioni Kufungwa

    By: Unknown On: 21:07
  • Share The Gag

  • JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na  sifa.

    Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam jana.

    "Kuanzia sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.

    Mpinga alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.

    Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havina sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

    Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.

    Mkolla alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.


    ==

    Credit Mpekuzi Blog 

    Mafisadi fedha za miradi kukiona

    By: Unknown On: 21:05
  • Share The Gag

  • Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akihutubia.

    MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano, itapambana kwa nguvu zote na vitendo vya ufisadi kwenye fedha, zinazoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
    Amesema serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, kudhibiti matumizi yasiyo lazima na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa, zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

    Alisema hayo jana wakati akifunga maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane kitaifa katika Uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa niaba ya Rais John Magufuli.
    Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja hivyo, Makamu wa Rais alisema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia, iwapo tu vitendo vya ufisadi katika fedha zinazoelekezwa kwenye maendeleo utakoma.
    Alisema pia hayo yatawezekana endapo wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati, kudai risiti, kufanya kazi kwa bidii na kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

    “Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka, jinsia, dini au itikadi za vyama vyenu.”
    Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Samia alisema maadhimisho ya Nanenane ni moja ya juhudi za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa, ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi kote nchini.
    Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa kipaumbele sekta za kilimo, mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.

    Aliwaeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.
    Alifafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maofisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.

    Matarajio ya wananchi
    Akizungumzia matarajio ya wananchi, Samia alisema serikali inajua wananchi wana matarajio makubwa ya uongozi wao hivyo itahakikisha inaboresha huduma na uchumi wa Watanzania wote.
    “ Tunajua mna matarajio makubwa na uongozi wa awamu ya tano, basi niwaahidi kuwa serikali yenu itahakikisha inaimarisha huduma na uchumi kwa usawa bila kuwa na upendeleo wa mikoa mnayotoka, itikadi ya dini na siasa,” alisema.
    Aidha alisema ni vyema uongozi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanaendeleza mashamba katika mikoa yao wayatumie kuwaelimisha wananchi njia bora za kilimo. Pia aliwataka wananchi kusaidia juhudi za serikali katika kuleta maendeleo kwa kulipa kodi, kupambana na rushwa na wafanyakazi wazembe na wavivu.
    “Ningependa kuwaomba wananchi kuiunga mkono mikakati ya serikali ambayo ina lengo la kuwaletea mabadiliko chanya. Watanzania wote mnatakiwa kulipa kodi kama inavyotakiwa ili kufanikisha malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2020, alisema.
    Kwa upande wa ufugaji, Samia alisema serikali inaboresha wataalamu wa mifugo ambapo wenye elimu ya Diploma wameongezeka kutoka 2,451 mwaka 2015 hadi 2,500 mwaka huu, wakati wale wenye Cheti wameongezeka kutoka 1,034 mwaka 2015 hadi 1,466 mwaka 2016 huku 1,471 wakihitimu Shahada mwezi Juni mwaka huu.

    Alisema mpaka Juni mwaka huu kulikuwa na upungufu wa wataalamu 8,725 nchi nzima.
    Kwa upande wa uvuvi, Samia alisema idadi ya mabwawa imeongezeka kutoka 21,300 mwaka 2014/2015 hadi 22,500 mwaka 2015/2016.
    Alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020, ajira kwa vijana inaongezeka hadi kufikia asilimia 40 na kuwataka vijana kuchangamkia fursa za ajira zinazojitokeza.
    Atembelea banda la TSN
    Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais aliipongeza Kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers Limited (TSN) kwa kuwawezesha wananchi kupata taarifa sahihi kupitia magazeti yake, likiwamo gazeti mtandao.
    TSN ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, HabariLeo, HabariLeo Jumapili, SpotiLeo na gazeti mtandao linalopatikana kwa anwani ya www. dailynews.co.tz na www.habarileo. co.tz.

    Alitoa pongezi hizo baada ya kutembelea banda la TSN kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Pia alivutiwa jinsi TSN inavyoendesha gazeti mtandao na kuahidi kuwa atajiunga na huduma ya gazeti mtandao haraka iwezekanavyo.
    “Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya nami nitajiunga na magazeti mtandao ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo,” alisema huku akitaka kujua kama huduma hiyo ni ile ya kupata ukurasa wa mbele na nyuma pekee.

    Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa TSN, Prosper Mallya alimwambia Makamu wa Rais kuwa magazeti mtandao yana kurasa zote kama ilivyo kwa magazeti ya kawaida, lakini yanauzwa kwa nusu bei.
    “Daily News mtandao inauzwa kwa Sh 500, HabariLeo kwa Sh 400 na SpotiLeo inauzwa kwa Sh 250, bei ambazo ni nusu ya bei za magazeti ya kawaida,” alisema.

    Mratibu wa Toleo Maalumu katika Magazeti ya TSN, Dativa Minja alimwambia Makamu wa Rais kuwa TSN imekuwa ikiandika habari, makala mbalimbali na uchambuzi katika masuala ya kilimo, ufugaji na uvuvi na kuwa wakulima wananufaika kwa kusoma magazeti hayo.

    Chanzo HabariLeo.

    BAVICHA Waunga Mkono Oparesheni UKUTA........Wasema Maandalizi Yote Yamekamilika, Wasisitiza Kutorudi Nyuma Septemba Mosi

    By: Unknown On: 00:22
  • Share The Gag

  • BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), limetangaza kuunga mkono operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta (Ukuta) iliyotangazwa hivi karibuni na Kamati Kuu ya chama hicho.

    Aidha, Bavicha wamemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwamba hana mamlaka ya kuzuia operesheni hiyo kwa kuwa wanaifanya kisheria na yeye siyo msajili wa vyama vya siasa.

    Makonda aliagiza Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya Ukuta, Ijumaa wakati akizungumza na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika kambi ya Ukonga.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi, alisema maandalizi ya kuunga mkono operesheni hiyo yamekamilika kwa nchi nzima.

    “Kauli ya Mkuu wa Mkoa (wa Dar es Salaam) ya kusema kwamba polisi wahakikishe Ukuta haujengeki, haitekelezeki kwa sababu yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo na wala si msajili wa vyama vya siasa hadi atoe kauli hiyo,” alisema Katambi.

    “Zipo kesi nyingi zinazoonyesha wakuu wa mikoa kufanya kazi ambazo haziwahusu, hivyo kauli yake tutaipima kisheria,” alisema na kuongeza:

    “Yeye akitaka aendelee kusema chochote akijisikia, lakini sisi tunamwambia kwamba mikutano yetu iko pale pale na tutaifanya nchi nzima.”

    Katika mazungumzo yake na FFU, Makonda alisema askari wanafahamu sheria, hivyo wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo.

    Aidha, aliwataka polisi hao kutosubiri maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais John Magufuli ameshaagiza kutofanyika kwa maandamano ya Ukuta yaliyopangwa kuwa Septemba mosi.

    Makonda aliliagiza jeshi hilo kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwapo kitu kinaitwa Ukuta ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

    Lakini Mwenyekiti wa Bavicha jana alisema: “Tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ajiandae kutuma jeshi lake kulinda mikutano yetu.”

    Kuhusu onyo la Rais Magufuli aliloitoa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida kwamba Chadema isimjaribu kwa Ukuta, Katambi alisema chama hicho hakimjaribu.

    Alisema Chadema itafanya maandamano nchi nzima kwa sababu kwa njia hiyo wanamsaidia kutoa mawazo yao kama vyama vya siasa kwa ajili ya kumsaidia kuendesha shughuli zake vizuri zaidi.

    “Hatuna shida ya kumjaribu Rais, na wala si kwamba tunamchukia, na wala hatuna sababu ya kupinga uwapo wake, na hata ukiulizwa sasa kwamba Rais wako ni nani, lazima useme ni John Magufuli,” alisema Katambi.

    “Tunapotoa dosari na kasoro tunamsaidia kuendesha nchi yake na watu walio chini yake.”

    “Sisi kama vyama vya siasa tuna haki, tunajua yeye ndiye Rais, kama sisi hatukuweza kupata nafasi ya hiyo, haimaanishi kwamba ni vita, isipokuwa kupitia vyama vyetu, tuna sehemu ya kutoa mawazo yetu katika kuifanikishia serikali yake kuongoza vema pamoja na watu wake wa chini tena kwa mujibu wa sheria na inamsaidia yeye kuwa bora zaidi.
    “Kwa hiyo kauli ya Rais sisi hatuna tatizo nayo.”

    Katambi alisema taratibu zote za kisheria katika kutekeleza mikutano hiyo zitafuatwa.

    Kamati Kuu ya chama hicho ilisema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia nchini.


    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    Rais wa Sao Tome na Principe asusia uchaguzi

    By: Unknown On: 00:14
  • Share The Gag
  • Rais Pinto da Costa amesema haamini uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki Katika hatua ya kushangaza, kiongozi wa visiwa vya Sao Tome na Principe, mojawapo ya mataifa madogo zaidi barani Afrika, amesusia awamu ya pili ya uchaguzi nchini humo.
    Rais Manuel Pinto da Costa amesema uchaguzi huo hauwezi kuwa wa haki na akawahimiza wafuasi wake kutoshiriki.
    Aliwataka wafuasi wake kutoshiriki uchaguzi huo wa Jumapili baada ya kupata chini ya robo ya kura zilizopigwa katika duru ya kwanza.
    Rais huyo alipata 24.8% ya kura zilizopigwa katika awamu hiyo ya kwanza tarehe 17 Julai naye mpinzani wake Evaristo Carvalho akapata 49.8%. Alisema uchaguzi huo wa kwanza ulikumbwa na udanganyifu.
    Wafuasi wa Evaristo Carvalho Taarifa zinasema wengi wa wafuasi wake walisusia uchaguzi huo wa kwanza.
    Bw Carvalho, ambaye alikuwa spika wa bunge na pia waziri mkuu, anaonekana kuhakikishiwa ushindi.
    Bw Pinto da Costa ameongoza kwa miaka mitano.
    Sao Tome na Principe Awali, aliongoza taifa hilo wakati wa utawala wa chama kimoja kuanzia 1975 hadi 1991 alipofanikisha kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
    Taifa hilo, ambalo lilitawaliwa na Ureno, linajumuisha visiwa viwili vikubwa Sao Tome na Principe pamoja na visiwa vingine vidogo.


    Chanzo BBC.

    Sunday, 7 August 2016

    Sikia Mkwara Huu wa Banana Zorro

    By: Unknown On: 23:47
  • Share The Gag

  • Mkali kunako muziki wa kizazi kipya, Banana Zoro amejigamba kuwa hahofii kuimba bila kutumia vyombo kwani uwezo wake kwenye muziki ni mkubwa haswaa.

    Akiongea hivi juzi Banana amesema wasanii wengi wanashindwa kuimba bila kutumia vyombo kwasababu hawajitumi katika kazi hiyo. “Mimi naweza kuimba bila kupiga vyombo au midundo na watu wakaelewa nini ninafanya kwani nipo kwenye muziki muda mrefu na najua ninachokifanya” alimalizia.


    Credit; UDAKU SPECIAL